Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo ya Biashara Kutoka Benki ya TIB Joseph Chilambo akizungumza na Wajasiriamali katika Mkutano uliondaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake (TWCC) Jijini Dar es SalaamWanawake Wafanyabiashara waliojitokeza katika Mkutano wa Mwezi Kwa Wafanyabiashara Wanawake na Kundi la Vijana ulioandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake nchini (TWCC) Uliofanyika Jijini Dar es Salaam
Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo ya Biashara wa Benki ya TIB Joseph Chilambo akisikiliza Kwa Makini Mawazo yanaowasilishwa na Wafanyabiashara Wanawake na Vijana katika Mkutano wa Mwezi uliondaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake (TWCC) uliowakutanisha Watoa huduma kwa Wajasiriamali wakubwa na wadogo Jijini Dar es Salaam
BENKI
ya Maendeleo ya TIB ilishiriki katika mkutano wa kifungua kinywa wa
Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) uliowakutanisha
Wajasiriamali wanawake kutoka mikoa yote ya Tanzania.
Hafla hiyo
iliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam, ilitoa jukwaa muhimu kwa wanawake kuweka mtandao
na kuongeza uelewa kuhusu fursa mbalimbali za biashara na fedha.
Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo ya Biashara wa TIB Joseph
Chilambo aliwasilisha huduma mbalimbali za fedha za uwekezaji ambazo
benki hiyo inatoa wanawake wanaomiliki biashara ndogo na za kati. Bw.
Chilambo alisisitiza kujitolea kwa benki hiyo kwa makampuni ya biashara
yanayomilikiwa na wanawake .
"Kusaidia SMEs ndio msingi wa
majukumu yetu, ndiyo maana tunajivunia kuunga mkono mpango huu muhimu
kwa SME zinazoongozwa na wanawake.
Hizi ni pamoja na vifurushi
vya mkopo vinavyobadilika, programu za kujenga uwezo, na huduma za
ushauri zinazolenga kuimarisha ukuaji wa biashara na uendelevu.
Benki
inasalia kujitolea kukuza ukuaji, kuimarisha biashara zinazomilikiwa na
wanawake, na kuendeleza uwezeshaji wa kiuchumi kote nchini.
Hata
hivyo amesema Benki hiyo imeweka Kiasi cha Shilingi Bilioni 30 kwa
ajili ya Wajasiriamali Wanawake Kukopeshwa ili kukuza mitaji yao ya
Biashara.
Pia amesihi Wanaotaka Kufungua Viwanda na Biashara
kubwa kuweza kufika katika Benki hiyo huku vigezo kikubwa ili aweze
kukopeshwa ni pamoja na Biashara hiyo iwe Imesajiliwa na cheti cha Brela
na Mradi ambao umeandikiwa mpango wa Biashara hiyo.
Huku
mrejesho wa mkopo huo unaweza kuwa kwa Mwezi au Mwaka kulingana na
Biashara yenyewe na namna fedha inayoingia kupitia biashara hiyo huku
Wafanyabiashara wadogo na Wakubwa wanaweza kukopesheka.
Ametoa
wito kwa Wafanyabiashara kujitahidi kutunza hesabu za kibiashara ili
Benki inayowakopesha iwe rahisi kuwa na Taarifa sahihi ya Kiwango
kinachoingiza kupitia biashara hiyo.
Kwa Upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake nchini (TWCC) Mwajuma
Hamza amesema Mkutano huo mahususi kuwakutanisha Wajasiriamali pamoja na
Wadau wa Biashara ili kurahisisha mifumo ya utunzaji fedha pamoja na
Kukuza Mitaji kwa Wajasiriamali wadogo na Wakati.
Hata hivyo
ameongeza kuwa Watoa Huduma kupitia Mkutano huo wataweza kujua pesa
zinazotengwa kwa ajili ya kuwakopesha Wajasiriamali hao ziongezwe
Kutokana na ukubwa wa Biashara zao.
Pia ametoa wito kwa
Wajasiriamali Wanawake waweze kutambulika kisheria biashara zao,kukuza
Majina yao pamoja na kupata tenda za serikalini kwani Chama hicho
kinawapa fursa Wanawake kushirki Mikutano mbalimbali inayoandaliwa nchi
nzima lengo ni kuwakutanisha Wanawake Wajasiriamali wote kutambulika na
Kupata Mikopo ya Kibenki kiurahisi.
Comments