Ikiwa ni siku ya nne ya zoezi la uandikishaji wananchi katika Daftari la Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro leo Oktoba 14, 2024 amejiandikisha katika daftari hilo Mtaa wa Mjimwema Manispaa ya Songea.
Akizungumza na baadhi ya wananchi waliojitokeza katika eneo hio Mhe. Ndumbaro amewahamasisha vijana na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika maeneo kujiandikisha, ili wapate fursa ya kugombea na kuchagua viongozi wanaowataka katika mitaa yao.
Aidha
Mhe. Ndumbaro amekagua uandikishaji katika mitaa mingine miwili mtaa wa
Merikebo Kata ya Bombambili na Mtaa wa Matarawe kati Kata ya Matarawe
ambapo zoezi hilo linaendelea vizuri, na litahitimishwa Oktoba 20,2024
kote nchini.
Comments