Friday, November 03, 2017

UZALENDO KWANZA WAUNGANA NA MSAMA AUCTION MART KUTOKOMEZA KAZI FEKI ZA WASANII NCHINI.

Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza,alipokuwa akizunguma nao mapema leo jijini Dar,
,wakiunga mkono kampuni ya Msama Auction Mart pamoja  na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kazi nzito wanayoifanya ya kukamata Walanguzi wa kazi za wasanii hapa nchini.
Baadhi ya Wasanii mbalimbali wa filamu hapa nchin walipokuwa wakifuatilia mkutano huo mapema leo jijini Dar.

pichani kati ni Mwenyekiti wa kikundi cha Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,wakiunga mkono kampuni ya Msama Auction Mart pamoja  na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kazi nzito wanayoifanya ya kukamata Walanguzi wa kazi za wasanii hapa nchini,kulia ni Mkurugenzi wa 
Kampuni ya Msama Auction Mart ,Alex Msama.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart ,Alex Msama akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na waandishi mapema leo,namna wanavyoshiriki zoezi la kukamata kazi feki za Wasanii,sambamba na wakwepa kodi kupitia kazi wasanii.

Kikundi cha Uzalendo Kwanza ikishirikiana na Kampuni ya Msama Auction Mart wameamua kuungana kwa pamoja katika kutokomeza kazi Feki za Wasanii hapa nchini.

Uzalendo Kwanza kupitia kwa Mwenyekiti wake, Steve Nyerere wameungana na Msama Auction Mart pamoja na kushukuru juhudi zinazofanywa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kazi nzito wanayoifanya yakukamata Walanguzi wa kazi hizo.

Steve Nyerere amesema wafanyabiashara katika Maduka Makubwa ya Filamu vifaa vya Soka wanafanya biashara hizo lakini hawalipi Kodi, hivyo wanawapongeza Msama Auction na TRA kuunga mkono  jitihada zakutokomeza wizi huo.

"Wamejiajiri katika Taifa la Watanzania, wakipata faida kubwa, Kodi na Mapato makubwa yangepatikana", amesema Steve.Ameongeza kusema kuwa "Msama hatoshi, TRA peke yake hatoshi; Mhe. Rais hatoshi kama Wasanii wenyewe hatutounga mkono jitihada hizi".

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama amesema kuwa anawashukuru Wasanii wa Tanzania kwa kuunga mkono juhudi hizo za kukomboa kazi zao.

Pia amesema kuwa Zoezi hilo haliko jijini Dar es Salaam tu, zoezi hilo ni la nchi nzima."Popote ulipo kila mahali tutafika kuhakikisha unauza kazi halali zenye Stika za TRA", amesema Msama.

Hata hivyo amewataka Wafanyabishara hao wanaofanya biashara ya kazi za Wasanii wa Tanzania kufuata taratibu ili kufanya biashara salama.
Post a Comment