Friday, November 03, 2017

TRA IKISHIRIKIANA NA MSAMA AUCTION MART YAENDELEZA MSAKO YA KUWABAINI WAKWEPAJI KODI KATIKA KAZI ZA SANAA

Mamalaka ya Mapato nchini (TRA), Msama Auction Mart kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wameendelea na zoezi la kupita Duka kwa Duka, Mlango kwa Mlango kusaka wezi wa kazi za Sanaa na wakwepaji wa Kodi hapa nchini.

Zoezi hilo linaloendelea kwa nchi nzima, hapo jana liliendeshwa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Kamishna wa Kodi za Ndani - TRA, Elijah Mwandumbya amesema wameamua kufanya zoezi hilo ili kujiridhisha katika maduka ambayo yanafanya biashara za kazi za Wasanii.

Mwandumbya amesema kuwa lengo la zoezi hilo ni kuhakiksha wanaofanya biashara hizo wanalipa Kodi shahiki, na kuhakikisha Stempu za Kodi zimatumika katika kila CD; "Kwa maana Stempu mbili kwa CD moja yaani Stempu moja kwenye Kasha la CD hiyo na nyingine kwenye CD yenyewe", amesema. 

Pia kuhakikisha wale wanaofanya biashara za kazi za Wasanii wanavibali vya kufanya biashara hizo, ikiwa sambamba na kuwachukulia hatua stahiki ili kuhakikisha Wasanii hao wanapata haki zao katika kila kazi ambayo inauzwa sokoni.Amesema huo ni muendelezo wa Kampeni ambao unafanywa nchi nzima kutokana na kazi hiyo iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda miezi kadhaa iliyopita.

"Kwa kazi za Wasanii wa kigeni upo utaratibu wakufuata katika Taasisi pamoja na Kampuni mbalimbali ili kuuza kazi za Wasanii hao", amesema Mwandumbya.



Mkurugenzi wa Msama Auction Mart Alex Msama akiwa sambamba na wafanyakazi wake kwa kushirikia na Jeshi la Polisi wakikamata vifaa vinavyotumika kurudufu kazi za wasanii (muziki),jana katika moja ya Mtaa Kariakoo jijini Dar
Kamishna wa Kodi za Ndani - TRA, Elijah Mwandumbya akikagua moja ya CD ya filamu za hapa nchini,kubaini kuwa kama ina stika za TRA ama la,akiwa sambamba na Mkurugenzi wa Msama Auction Mart Alex Msama ambao wamepewa dhamana ya kushirikiana na TRA kupapambana na maharamia wa kazi za wasanii wakiwemo na wale wanaokwepa kodi
Ukaguzi ukiendelea kufanyika katika maduka yanayouza CD za Filamu,kubaini kuwa zinalipiwa ushuru na zina stika kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Baadhi ya Watuhumiwa na mafurushi yao ya CD zinazodaiwa kutolipiwa kodi na kukosa STIKa za TRA wakiwa nchini ya Ulinzi mara baada ya kufikiwa kituo cha polisi kati,jana jioni jijin Dar.

No comments: