Tuesday, August 31, 2010

Mkapa ayawakia mataifa ya Magharibi


Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa (kushoto) akimsikiliza Katibu Mtendaji wa African Forum Dk John Tesha mara baada ya kumaliza mkutano wa marais wastaafu na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam jana uliokuwa unaelezea mikakati ya maboresho ya ardhi barani Afrika.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa (kushoto) akitoa ufafaunuzi jana jijini Dar es salaam kwa wanahabari mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Marais wastaafu wa Afrika uliokuwa unajadili juu ya maboresho katika sekta ya ardhi barani Afrika. Kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es Salaam.

Pingamizi la Chadema latinga kwa JK


Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, akiwa ameshika nakala ya pingamizi dhidi ya mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete, wakidai mgombea huyo amekiuka kanuni za sheria ya gharama za uchaguzi baada ya kuiwasilisha kwa msajili wa vyama vya siasa jana jijini Dar es Salaam. Picha na Zacharia Osanga

**********************************************************************
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeteketeza azma yake ya kumwekea pingamizi mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.

Taarifa zimeeleza kuwa chama hicho kiliwasilisha pingamizi hilo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini jana saa 7:30 mchana.

Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika, ndiye aliyewasilisha pingamizi hilo.

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa alipoulizwa hakutaka kukubali au kukataa kuliona pingamizi hilo na akasema atazungumzia suala hilo leo.

Awali Chadema ilipanga kuweka pingamizi hilo la kutaka Kikwete azuiwe kugombea urais, Agosti 27 mwaka huu, lakini, ilisitisha kwa kile ilichoeleza kuwa inasubiri mambo mengi zaidi ambayo wangeyaingiza kwenye pingamizi hilo.

Chama hicho awali kilitaka kuweka pingamizi hilo kwa kile kilichoeleza kuwa Rais Kikwete amekiuka Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa kutangaza nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi kwenye kampeni.

"Tulishindwa kupeleka pingamizi hilo jana kwa sababu tumesikia kwamba huku anakoendelea na kampeni zake, mgombea huyo ameendelea kufanya makosa mengine ambayo tutataka tuyaingize kwenye pingamizi hilo," alisema Mnyika mwishoni mwa wiki. Habari hii imeandikwa na Geofrey Nyang’oro. SOURCE: MWANANCHI.

Monday, August 30, 2010

Kampeni za mzee Ndessa


Umati mkubwa wa wafuasi wa Chadema na Wananchi wa Jimbo la Moshi mjini waliofurika viwanja vya Manyema katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni wa mgombea Ubunge wa chama hicho,Philemon Ndesamburo

Mgombea Ubunge Jimbo la Moshi mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Philemon Ndesamburo akihutubia wananchi wa Jimbo hilo waliojitokeza wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho juzi katika viwanja vya Manyema.

Sunday, August 29, 2010

Madee afunika Mbeya......

Mwanamuziki nguli wa kikundi cha muziki wa kizazi kipya cha Tip Top Connection chenye maskani yake mitaa ya Manzese jijini Dar es Salaam, Madee akiimba wakati wa uzinduzi wa huduma ya Tigo Pesa katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mwishoni mwa wiki. Picha kwa hisani ya Tigo.

Oliver Mtukudzi ndani ya bongo



Mkongwe wa muziki kutoka Zimbabwe, Oliver Mtukudzi maarufu ‘Tuku’ akifanya onyesho la muziki usiku wa kuamkia jana jijini Dar es Salaam. Onyesho hilo lililoanza Ijumaa usiku na kumalizika jana liliandaliwa na wananchi wa Zimbabwe wanaoishi hapa nchi na kudhaminiwa na makapuni mbalimbali ikiwemo Mwananchi Communications Ltd. Kushoto ni mpiga tumba, Namatayi Mabariki Chipanza. Picha na Salhim Shao

Friday, August 27, 2010

Kenya waidhinisha katiba mpya


Mbwembwe za kijeshi
Rais Mwai Kibaki akiapa.
Mashirika ya haki za binadamu yameilaumu serikali ya Kenya kwa kumruhusu Rais Omar Hassan al-Bashir kuitembelea Kenya ambako atahudhuria sherehe ya nchi hiyo ya kuidhinisha katiba mpya.Kiongozi huyo anatakiwa na Mahakama ya Kimataifa (ICC) kwa mashtaka 10 ya uhalifu, ikiwemo uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari yanayodaiwa kufanyika huko Darfur.

Yeye ni kiongozi wa kwanza aliye madarakani kutuhumiwa na mahakama hiyo ya the Hague. Kenya ni moja ya nchi zilizotia saini mkataba wa mahakama ya ICC ujulikanao kama sheria ya Rome unaoitaka kisheria kumkamata na kumkabidhi kwa mahakama hiyo.

Hata hivyo, uamuzi wa mara mbili uliofanywa na Umoja wa Afrika, uliwaamuru wanachama wake wasimkamate Rais huyo wa Sudan, hata hivyo ulikosea tu kusema kama kuna hatua itakayochukuliwa dhidi ya nchi yoyote itakayokiuka maagizo hayo na kutii amri ya ICC.

Shirika rasmi la habari nchini Sudan (SUNA) limesema katika taarifa fupi kuwa Rais Bashir atasafiri kwenda Nairobi akifuatana na mshauri wake Mustafa Ismail, waziri wa mashauri ya kigeni Ali Karti na mkurugenzi mtendaji wa idara ya ujasusi Muhammad Atta Al-Mawla.

Hii ni ziara yake ya pili katika moja ya nchi wanachama zilizotia saini mkataba wa Rome baada ya kuzuru Chad mwezi uliopita. Licha ya ziara hiyo alipuuza mwaliko wa kuhudhuria mkutano wa kilele wa nchi wanachama wa IGAD mjini Nairobi mwaka huu.

Shirika la Human Rights Watch limesema kuwa ziara yake itaweka doa sherehe za kuidhinisha katiba iliyosubiriwa kwa hamu kwa kumpokea kiongozi huyo.source BBC.

Tuesday, August 24, 2010

Ufisadi misaada ya wahisani wapatiwa dawa


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi,Ramadhan Khijjah akioyesha kwa wadau mbalimbali chapisho linaloelezea jinsi ya kupata taarifa kwa njia ya tovuti zinatoa ufafanuzi wa Mfumo wa Usimamizi wa Misaada ( Aid Management Platform System) inayotolewa na wahisani mbalimbali kwa Tanzania. Mfumo huo utawawezesha wadau mbalimbali kupata taarifa sahihi ya misaada yote inayotolewa na wahisani kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania.picha ya Maelezo

MRADI WA TACTIC KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MAGARI JIJINI MWANZA

  * Sekta ya uvuvi nayo yaguswa. Mwanza.  Ujenzi wa Barabara ya Buhongwa-Igoma yenye urefu wa Km 14 kwa kiwango cha lami inayojengwa katik...