Saturday, June 13, 2009

Uzinduzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT) Dar

















Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), kimezindua tawi la chuo hicho Dar es Salaam ambalo linatoa Shahada ya Uzamili na Uzamivu wa Mawasiliano ya Umma. Tawi hilo lilianza kutoa mafunzo mwaka jana.


Akizindua chuo hicho sambamba na jarida la mawasiliano barani Afrika linaloandaliwa na wanafunzi wa chuo hicho, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alisema lengo la Chuo kikuu hicho ni kujenga jiji la Mungu kwa kutoa elimu yenye ubora wa hali ya juu pia akasema lengo kubwa ni kuwafikia watanzania popote walipo.

Jamaa akatwa uume



Gaspa Denis mkazi wa Ilboru akiwa anaugulia maumivu katika hospitali ya Mt. Meru mara baada kupondwa uume na baadaye kukatwa na vitu vyenye ncha kali na mtu ambaye bado hajafahamika kwajina. (Picha na Hemed Kivuyo)

Friday, June 12, 2009

Balozi mpya wa Marekani nchini


Rais Obama amteua Alfonso Lenhardt (pichani) kuwa Balozi wa Marekani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Barack Obama amemteua Mheshimiwa Alfonso E. Lenhardt kuwa Balozi wake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa mfumo unaotumiwa na Serikali ya Marekani, Rais huteua Mabalozi kwa mashauriano na hatimaye kupata ridhaa ya Bunge la Seneti la Marekani.

Toka Mwezi Mei 2004, Mheshimiwa Lenhardt amekuwa Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Kitaifa la Kuzuia Uhalifu (National Crime Prevention Council - NCPC) ambalo ni taasisi isiyo ya Kiserikali na isiyozalisha faida. Pia alikuwa Makamu wa Rais wa Kundi la Makampuni ya Shaw akishughulikia Uhusiano na Serikali. Tarehe 4 Septemba 2001 aliteuliwa kuwa Mpambe wa Bunge (Sergeant-at-Arms) wa 36 wa Bunge la Seneti la Marekani na kuwa Muamerika wa Kwanza mwenye asili ya Kiafrika kuhudumu katika wadhifa huo ndani ya Bunge la Marekani. Aidha, alihudumu kama Makamu wa Rais na Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Baraza linaloshughulikia Wakfu Mbalimbali (Council on Foundations).

Mheshimiwa Lenhardt alistaafu kutoka katika Jeshi la Marekani hapo August 1997 akiwa na cheo cha Meja Jenerali, baada ya kulitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 30 katika ngazi mbalimbali za uongozi. Wadhifa wake wa mwisho jeshini ulikuwa ni Mkuu wa Kamandi ya Uajiri, yenye makao makuu yake huko,Fort Knox, KY, ambao aliongoza na kusimamia taasisi iliyojumuisha zaidi ya watu 13,000 waliokuwa katika zaidi ya vituo vya kazi 1,800. Aidha, aliwahi kudumu kama Afisa Mwandamizi wa Polisi Jeshi (Senior Military Police Officer) katika oparesheni zote za kipolisi na masuala ya usalama katika Jeshi la Marekani sehemu mbalimbali duniani.

Mheshimiwa Lenhardt ambaye alizaliwa katika jiji la New York, ana Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Sheria kuhusu Makosa ya Jinai kutoka katika Chuo Kikuu cha Nebraska, Shahada ya Pili ya Sanaa Katika Utawala kutoka katika Chuo Kikuu cha Central Michigan na Shahada ya Pili ya Sayansi ya Utawala katika Sheria kutoka katika Chuo Kikuu cha Serikali cha Wichita. Aidha, Mheshimiwa Lenhardt ni mhitimu wa awamu ya 94 Katika Chuo cha Kitaifa cha Mafunzo ya Usalama cha FBI; programu ya Viongozi wa Upepelezi wa Makosa ya Jinai ya Jeshi la Marekani . Aidha ni mhitimu wa Chuo cha Kitaifa cha Mafunzo ya Kivita (the National War College) na Chuo Kikuu cha Mambo ya Kijeshi na Usalama (National Defence University).

Kuhusu Uteuzi wa Mheshimiwa Lenhardt na mabalozi wengine, Rais Obama alisema, "Wamarekani watafaidika sana kwa kuwa na watumishi hawa waliotukuka, wake kwa waume, kama wawakilishi wao nchi za nje. Vipaji, uzoefu na kujitoa kwao kikamilifu kutakuwa na mchango mkubwa sana tunapoendelea kuimarisha ubia kati ya Marekani na mataifa mbalimbali duniani kote na kukabiliana na changamoto kubwa za karne ya 21. Ninashukuru kwa utumishi wao na nina shauku kubwa ya kufanya kazi na kila mmoja wao."

Kwa taarifa zaidi kuhusu tangazo la uteuzi huu kutoka Ikulu ya Marekani tembelea tovuti: http://www.whitehouse.gov/the_press_office/President-Obama-Announces-More-Key-Administration-Posts-6-11-09/

Thursday, June 11, 2009

Bajeti ya uchaguzi


Waziri wa fedha na mipango Mustafa Mkullo akiingia bungeni leo na mkoba wake tayari kusoma bajeti ya mwaka 2009/2010. Ameishaisoma bajeti ambayo kwa kiaasi kikubwa imemegwa na Rais jakaya Kikwete kiufupi nachoweza kusema ni bajeti ya uchaguzi ameanza kuisoma toka saa kumi kamili za hapa kwetu. bajeti hiyo itaanza kujadiliwa Jumatatu

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Sukita mzee John Kapinga azikwa

Mke wa rais mama Salma Kikwete akiweka shada la maua juu ya kaburi la ndugu John Kolos Kapinga wakati wa mazishi ya aliyekuwa mkurugenzi wa SUKITA ndugu John Kolos Kapinga yaliyofanyika nyumbani kwake eneo la Kimara stop over jijini Dar es salaam.
Mapadre wa kanisa Katoliki Parokia ya Mavurunza wakiongozwa na Paroko wa kanisa hilo Erasto Nyoni wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu John Kolos Kapinga.Marehemu Kapinga alizikwa jana jioni nyumbani kwake eneo la Kimara stop over, Dar es salaam.
Mke wa marehemu John Kapinga akiweka udongo kwenye kaburi la mumewe marehemu Kapinga wakati wa mazishi yaliyofanyika jana jioni eneo la Kimara stop over jijini Dar es salaam.
Ndugu , jamaa na watoto wa aliyekuwa Mkurugenzi wa SUKITA marehemu John Kolos Kapinga wakiwa mbele ya kaburi la John Kapinga wakiongozwa na mke wa marehemu mama Revy Kapinga (wa pili kulia mstari wa mbele)

Mama Revy Kapinga akiweka shada la maua juu ya kaburi la mumewe marehemu John Kolos Kapinga wakati wa mazishi yaliyofanyika jana jioni eneo la Kimara stop over jijini Dar es salaam.Picha zote zimepigwa na mdau Aron Msigwa wa MAELEZO- Dar.

Wednesday, June 10, 2009

Eti Zain kuuzwa kwa wafaransa

Taarifa nyingi zimesambaa sasa ya kwamba kampuni maarufu ya simu za mkononi ambayo imeshajibadili majina mara mbili hivi iko mbioni kuuzwa kwa kampuni ya kifaransa ya mtandao wa mawasiliano ya simu za viganjani kampuni hiyo inaelezwa kuyameza mambo yote ya Zain
Soma kinagaubaga taarifa hapa upate habari hizi kwa kina.

JK amnusuru Waziri Mkulo


Rais Jakaya Kikwete amehutubia taifa kupitia kwa wazee wa Mkoa wa Dodoma na wabunge. Amezungumzia zaidi msukosuko wa uchumi duniani kwa mapana yake na hali ya uchumi kwa ujumla; na overview ya bajeti. Kwa namna fulani, ni kama ame-pri-empty hotuba ya bajeti ya Waziri wa Fedha ya kesho. Ameibua kitu kipya cha serikali kudhamini madeni ili kupunguza makali ya uchumi wa dunia. Mdau kanitumia SMS akihoji, je, hiyo si EPA nyingine? Reuters wameandika hivi na Hotuba Kamili Hii Hapa.

Wakati huo huo, Kurugenzi ya Mwasiliano Ikulu imesema yafuatayo: Mambo makuu katika Hotuba ya Rais, Dodoma, – jumatano, Juni 10, 2009.

1. Rais ameelezea hali ya mtikisiko wa uchumi duniani, chimbuko la mtikisiko huo na athari za hali hiyo kwa uchumi wa Tanzania. Athari hizo ni kama ziafuatazo:

(a) Bei na mahitaji ya bidhaa za Tanzania kwenye masoko ya kimataifa yamepungua.
(b) Mahitaji na bei za madini ya vito vimepungua kwenye masoko ya kimataifa
(c) Mahitaji ya mazao ya kilimo ya Tanzania kama vile maua na mboga yamepungua kwa asilimia 25
(d) Viwanda vya ngozi, nguo, nyuzi na mavazi pia vimeathirika na hivyo kuathiri pia upatikanaji wa ajira nchini
(e) Sekta ya utalii ambayo ndiyo kubwa kwa uingizaji wa fedha za kigeni pia imeathirika kwa watalii wanaokuja nchini kupungua
(f) Mapato ya Serikali pia yamepungua na hivyo kuathiri mapato ya ndani na mapato ya fedha za kigeni
(g) Uwekezaji kutoka nje umepungua pia na baadhi ya makampuni yaliyokuwa yanataka kuja kuwekeza Tanzania, ama yameahirisha ama yamefuta mipango yao ya uwekezaji. Mifano ni mradi wa uwekezaji katika nickel pale Kabanga, Ngara, Kagera na miradi ya umeme, saruji, mbolea na aluminium smelter mkoani Mtwara
(h) Hali ya ajira nchini imekuwa mbaya zaidi kwa sababu ya matatizo hayo ya uchumi na hadi Aprili, mwaka huu, kiasi cha watu 48,000 walikuwa wamepoteza ajira
(i) Vile vile kasi ya kukua kwa uchumi wa Tanzania inakadiriwa kuwa itapungua kutoka kwenye asilimia 7.4 kama ilivyobashiriwa mwaka huu hadi kufikia asilimia 5 hadi 6.

Soma kinagaubaga taarifa hapa au upate habari hizi kwa kina.

RAIS SAMIA AZINDUA TUME YA UCHUNGUZI KWA AJILI YA KUIMARISHA AMANI, HAKI NA UWAJIBIKAJI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Wajumbe wa Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Wahusi...