Friday, May 09, 2008

ATC anga kwa anga, ndege kwa ndege


Cheki muonekano mwanana wa kadege ka shirika letu la ATC, kanabeba watu kama 170 hivi ni matata kweli kwa kiwango cha bongo, lakini kwa wenzetu ni sawa na kadege kwa kwenda kununulia nyanya, angalau na sisi tunajitahidi.

Siku Serengeti walipopongezwa kwa ushindi




Wachhezaji wa timu ya taifa Stars wakijiburudisha na muziki ulokuwa ukiporomoshwa na bendi ya Kalunde band ya deo mwanambilimbi usiku wa jana kwenye hafla iliyoandakiwa na serengeti breweries ya kuwapongeza taifa staaz kwa kuifunga Uganda Cranes na kuwapa moyo kwa mchezo wa marudiano jijini Kampala wiki ijayo. Serengeti Breweries ilitoa dola 100 kwa kila mchezaji na dola 150 kwa kila kiongozi wa timu hiyo kwa kuifunga Uganda Cranes. Picha ya Mdau Deus Mhagale

Thursday, May 08, 2008

Chenge aanza ziara ya kudanganya watu kwao



Frederick Katulanda, Bariadi wa Mwananchi

LICHA ya aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge kuwaomba radhi Watanzania kwa kudai kuwa Sh1.2bilioni anazodaiwa kuzificha katika Kisiwa cha Jersey ni vijisenti, jana alirudia tena usemi huo wakati akihutubia mamia ya wakazi wa Bariadi mjini.

Chenge aliwaambia wananchi waliofika kumsikiliza kuwa hawezi kunywa sumu na kuacha vijisenti vyake nyuma.

"Mnyantuzu, kamwe siwezi kunywa sumu ili nife na kuacha vijisenti vyangu nyuma..." alisema Chenge.

Akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Bariadi jana, Chenge alisema kuwa amesikitishwa sana kuzushiwa kuwa amefariki dunia na kusema kwamba hawezi kujiua na kuviacha vijisenti vyake.

Akizungumza kwa Lugha ya Kisukuma Chenge alisema: "Bhadugu bhane wakayomba niachile olwa sumu, bhadugu Mnyantuzu ong'wa sumu, oleka vijisenti byakwe?". Alikuwa ana maanisha kuwa, akiwa kama Msukuma Mnyantuzu hawezi kufa kwa kujiua na kuacha vijisenti vyake. Hebu cheki Mwananchi Uone mambozzz.

Wednesday, May 07, 2008

Mugongo mugongo


Nimepita katika blogu ya dada Shamim hakika imetimia, kila siku mie hupita pale lakini leo nimepita nimekuta mambo makini hebu mcheki HAPA KWAKE Uone mambozzz.

Tuesday, May 06, 2008

Mtoto kizimbani


Mtoto aliyekutwa na kichwa cha mtoto aliyekatwa na akiwa na mamake wakisubiri kufikishwa mbele ya pilato kisutu kujibu tuhuma za mauaji.

Monday, May 05, 2008

Waziri Mkuu Pinda Yuko Msumbiji



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wakati alipotembelea ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji
akiwa nchini humo kuhudhuria mkutano wa umoja wa maendeleo ya Elimu Barani Afrika leo. Picha na Ofisi ya Wazieri Mkuu

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimana na Rais wa Msumbiji, Armando Emílio
Guebuza kabla ya mazungumzo yao jijini Maputo 5/5/2008. Mheshimiwa Pinda yuko
Maputo kuhudhuria mkutano wa umoja wa maendeleo ya elimu kwa nchi za Afrika
unaofanyika Maputo. Picha na Ofisi ya Waziri mkuu

50 Cent in Tanzania


Gari aina ya Range Rover vogue T689 AMW ambalo amepanda 50 Cent leo alipowasili likikatiza katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam.Picha ya Father Kidevu.



50 cents ametua dar na wanamuziki wake wa kundi la Gunit na kupokewa na umati wa mashabiki uwanja wa ndege wa julius nyerere terminal I akiwa ndani ya ndege ya kukodi akitokea sauzi, jana kafanya vitu vyake vya uhakika pale Diamond Jubilee, ila washikaji wa habari wanalalamika utaratibu haukuwa bomba hata kidogo. Picha za Reuters, Muhidin Issa Michuzi

MTUHUMIWA WA “KUFUTA MADENI” YA MIKOPO AKIRI KOSA, AHUKUMIWA KIGOMA

KIGOMA, Septemba 4, 2026 — Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma imemhukumu Nicholaus Komba Mahitana maarufu kama Abdallah Mahimbo baad...