Thursday, March 04, 2010

RAIS KIKWETE AHAMA KITUO CHA KUPIGIA KURA, AJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA MSOGA


MSIMAMIZI wa uandikishwaji daftari la kudumu la wapigakura, Msoga Diana Frederick akiwapa vitambulisho vipya vya kupiga kura, Rais Kikwete na Mama Salma baada ya kujiandikisha kwenye daftari jana.

RAIS Jakaya Kikwete akijiandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura kwenye kituo kipya cha kupiga kura kijijini kwake Msoga, Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani. Kushoto ni Msimamizi wa kituo hicho, Diana Frederick. Kituo cha zamani cha Rais Kikwete kilikuwa Bwilingi, Kata ya Chalinze, wilayani Bagamoyo. Picha na Bashiri Nkoromo.

Wednesday, March 03, 2010

CCJ wapata usajili wa muda



Msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa jana alihitimisha safari ya miezi miwili ya CCJ kusaka usajili wa muda,kwa kukipa chama hicho usajili wa muda.

CCJ chama ambacho kimesababisha mtikisiko ndani ya CCM kimekuwa kikifuatilia usajili wa muda katika Ofisi ya Msajili kwa karibu miezi miwili sasa tangu kuwasilisha maombi yao Januari 20, mwaka huu.

Viongozi wake wametangaza jana kwamba, wanatarajia kukamilisha kazi ya kuzunguka nchi na kupata idadi ya wanachama 200 katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu baada ya kupata hati hiyo badala ya miezi sita.

Mwenyekiti wa CCJ Richard Kiyabo, alitumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi wa tuhuma mbalimbali dhidi ya chama hicho na kusema hakina uhusiano wowote na Idara ya Usalama wa Taifa kwani mpango huo una lengo la kukivuruga ili kionekane ni chama pandikizi.

Kiyabo alifafanua kwamba, CCJ ni chama tofauti na vingine vya upinzani kwani kimejipanga vema kuhakikisha kinakidhi mahitaji ya msingi ya kidemokrasi kwa Watanzania.

"CCJ siyo chama cha Idara ya Usalama wa Taifa, ni chama cha usalama wa maisha ya Mtanzania, ni chama makini tofauti na vingine vya upinzani kwa hiyo kuna tofauti kubwa," alisisitiza.

Mwenyekiti huyo ambaye alikuwa akibebwa juu pamoja na katibu wake Renatus Muabhi na baadhi ya wanachama waanzilishi, alisema lengo, nia na madhumuni ya CCJ ni kushiriki uchaguzi wa Oktoba.

Tuesday, March 02, 2010

Uzinduzi Precision Air



Precision Air employees open Champaign during the launching of the new plane ATR 42 in Dar es Salaam yesterday. PHOTO/SILVAN KIWALE.

Mwanamke jasiri wa mwaka



U.S. Ambassador Alfonso E. Lenhardt today, March 2, 2010, presented the 2010 Tanzanian Woman of Courage award to Ananilea Nkya for her efforts to promote equality, opportunity, and justice for Tanzanian women and girls. Nkya is a journalist by profession and has been the Executive Director of the Tanzania Media Women Association (TAMWA) since 2001. In addition to the award, the Ambassador granted one million Tanzanian shillings to TAMWA in support of its scholarship program for women seeking university journalism degrees. (Photo courtesy of the American Embassy)

Monday, March 01, 2010

Breaking Newss watu 24 wafa ajali ya basi

Habari tulizozipata hivi punde zinasema kuwa 24 wamekufa papo hapo na wengine 56 wamejeruhiwa katika ajali ya basi iliyotokea jana jioni eneo la mpaka kati ya Nzega na Igunga mkoani Tabora.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 10: 15 jioni katika vijiji vya Kitangili na Migua baada ya basi aina ya Scania lililokuwa likitoka Arusha kwenda Mwanza kupinduka.

Waliokufa ni wanaume 14, wanawake sita na watoto wanne huku majeruhi ni wanaume 35, wanawake kumi na watoto 7 huku majeruhi wanne wamepelekwa katika Hospitali ya Bungando mkoani Mwanza kwa matibabu zaidi.

Mganga wa wilaya ya Nzega, Dk John Mwombeki alisema maiti pamoja na majeruhi hao wapo katika hospitali ya Nzega. Taarifa zaidi tutawaleteeni baadaye.

Abiria 49 wanusurika ajali ya ndege


Ndege ya ATCL imetua Mwanza asubuhi ikiwa na abiria 49, matairi ya nyuma yalitoka na kutua salama, lakini tairi la mbele lilipuka, Bahati nzuri mvua kubwa ilikuwa inanyesha, kwa hiyo ikawa ndio fire brigade, Milango iligoma kufunga kwa muda mrefu na gari la zima moto likaja baada ya dakika 20. Habari zaidi tunasubiri.

Balaa la mvua Kibaha



Wakazi wa Kibaha kwa mathias wakiokota bati kumpa fundi kwa ajili ya kuezeka nyumba zao ambazo ziliezuliwa kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali. Picha na Sanjito Msafiri.

RAIS SAMIA AZINDUA TUME YA UCHUNGUZI KWA AJILI YA KUIMARISHA AMANI, HAKI NA UWAJIBIKAJI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Wajumbe wa Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Wahusi...