Friday, June 06, 2008

mkutano wa Sullivan wafungwa


Mke wa Co-Chairman of Leon H. Sullivan, Ambassador Andrew Young, Carolyn
akiwa kava kofia yenye mchoro na maandishi yam lima Kilimanja jana wakati
alipokuwa kitembelea mabanda ya maonyesho ya Sullivan. Picha na Edwin
Mjwahuzi


Rais wa Zanzibar mh. Amani Karume akifunga rasmi mkutano wa siku nne wa sullivan hoteli ya Ngurdoto mountain usiku huu, na kuwakaribisha wageni toka marekani visiwani leo ijumaa kwa hafla maalumu ambayo amewaandalia kwenye hoteli ya zamani kempinski.

Thursday, June 05, 2008

Obama ashinda uteuzi wa kugombea urais





Seneta wa jimbo la Illinois nchini Marekani Barack Obama ametangazwa mshindi katika mchuano wa kuwania kuteuliwa kuwa mgombea wa urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Demokratik uchaguzi ambao umepangwa kufanyika hapo mwezi wa Novemba mwaka huu.

Obama amejishindia wajumbe wengi wanaohitajika ili kuweza kupata idhini ya chama katika siku ya mwisho ya uchaguzi wa awali wa kuwania uteuzi kwa tiketi ya chama katika mchuano mkali uliodumu kwa miezi mitano dhidi ya seneta wa jimbo la New York Hilary Clinton.

Licha ya kujipatia idadi mkubwa wa wajumbe Clinton amegoma kukubali kushindwa na Obama.

Katika hotuba kwa wafuasi wake mjini New York amesema bado hakufanya uamuzi juu mustakbali wake wa kisiasa.

Uwezekano wa Obama kushinda urais wa Marekani kwa wengi unaonekana kuwa unaweza kuboresha uhusiano wa kigeni wa Marekani uliodhoofika kwa muda mrefu.

Tuesday, June 03, 2008

Sullivan leo






Mwenyekiti wa Mfuko wa Leon H. Sullivan, Balozi Andrew Young akizungumza kwa nyakati tofauti na Rais Mstaafu wa Nigeria Olesegun Obasanjo, Jakaya Kikwete wa Tanzania wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nane wa Sullivan mkoani Arusha juzi Usiku. Picha zingine inaonyesha wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini. Picha na Edwin Mjwahuzi.


Sunday, June 01, 2008

Sumaye akwepa ufisadi

Frederick Sumaye, aliyekua Waziri Mkuu wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kwa
miaka kumi, leo amemtolea uvivu bosi wake wa zamani, Ben Mkapa kwa kukataa
kumtetea "kwa mambo binafsi" akisema kama ni utendaji wa serikali, anaamini
kia mtu anajua serikali ya awamu ya tatu ilifanya kazi nzuri, lakini wapo
watu binafsi mmoja mmoja waliofanya makosa na kwa kuwa wanachunguzwa
watahukumiwa kwa makosa yao na si serikali nzima....

Akatoa mfano wa ununuzi wa rada, ujenzi wa barabara, ununuzi wa ndege, uwekezaji na mengineyo kuwa ni mambo ambayo yana manufaa kwa taifa, lakini kupitia maamuzi hayo mema wako watu ambao walifanya uhalifu kama vile kula rushwa na kuhujumu uchumi
watu ambao alisema wanastahili kuhukumiwa kwa makosa yao binafsi baada ya
kuchunguzwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Alipoulizwa kwanini hamtetei Mkapa alisema, "Kama angekua anatuhumiwa kama
kiongozi wangu ningemsaidia kujibu, lakini jamani mambo binafsi mimi siwezi
kumsemea, Kwani mimi ni mtoto wake?... Si alisema kule Lupaso? Naona
hakumridhika,mbona hata Bush anaweza kwenda katika ranchi yake
kuzungumzia mambo?"

Akasema yeye anajiamini kuwa ni safi mbali ya kuwapo maneno machafu dhidi
yake, akirejea sababu ya kuzungumza na waandishi leo, ambako alikua mualikwa
katika mkutano wa uongozi wa gazeti la Tanzania LEO (Limekufa) ambao ulifika
kumuomba radhi kwa habari yao ya kwamba ana trilioni kumi nje ya nchi na
akaunti zake zimezuiwa na JK.
cheki
MWANAHABARI ANAVYOSEMA

Holiday Inn Hotel


Huu ndo mwonekano mpya wa Hoteli ya Holiday Inn pale karibu na International house nadhani sasa unaweza kuona jina hilo jipya ikimaanisha jua la kusi. Picha hii ni ya mdau Fedelis Felix aliyoinasa juzi wakati wakiizindua upya, sijui ni mtindo ule ule wa ukwepaji kodi au ni mambo ya product development.

Mkutano wa Sullivan






Washiriki wa Mkutano wa Sullivan wakiwasili katika uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mara baada ya kuwasili tayali kwa mkutano utakaoanza kesho , picha nyingine ni ya Co-chairman of The Leon Sullivan Foundation, Ambassador Andrew Young akijibu maswali kutoka kwa mwandishi wa habari wa hapa nchini mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro akitokea marekani kwaajili ya mkutano wa Sullivan utakaoanza jumatatu. Picha na Edwin Mjwahuzi na Athumani Hamisi

Baraka Obama

US Democratic presidential candidate and US Senator Barack Obama (D-IL) speaks to the press about his decision to leave his home church Trinity in Chicago in Aberdeen, South Dakota May 31, 2008. REUTERS/Rick Wilking (UNITED STATES) US PRESIDENTIAL ELECTION CAMPAIGN 2008 (USA)

MTUHUMIWA WA “KUFUTA MADENI” YA MIKOPO AKIRI KOSA, AHUKUMIWA KIGOMA

KIGOMA, Septemba 4, 2026 — Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma imemhukumu Nicholaus Komba Mahitana maarufu kama Abdallah Mahimbo baad...