Friday, February 23, 2018

UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA GEITA WAFIKIA ASILIMIA 35

Kaimu Meneja wa Wakala wa majengo mkoani Geita Mhandisi Glads Jefta  akielezea maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Rufaa.
Kaimu Meneja wa Wakala wa majengo mkoani Geita Mhandisi Gladys Jefta  akionesha michoro ya ramani ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa.
      
Kaimu Mganga mfawidhi Mkoa wa Geita, Dkt Joseph Odero akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali Teule ya mkoa wa Geita Bw Simon Rweyemamu pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita wakati walipofika kwa ajili ya kuona maendeleo ya ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Geita. 

Michoro ya ramani ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita.

Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali Teule ya mkoa wa Geita Bw ,Simon Rweyemamu akizungumza na  Kaimu Meneja wa Wakala wa majengo mkoani Geita Mhandisi Gladys Jefta  wakati alipofika kwaajili ya kuona maendeleo ya ujenzi wa Hospitali hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali Teule ya mkoa wa Geita Bw ,Simon Rweyemamu pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya mji,Leornad Bugomola  wakikagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Rufaa.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Geita.Leornad Kiganga Bugomola akikagua ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali Teule ya mkoa wa Geita Bw ,Simon Rweyemamu,akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua iliyopo kwa sasa ya ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita.
Kaimu Mganga mfawidhi Mkoa wa Geita,Dkt Joseph Odero  akizunguma juu ya changamoto ambazo zipo kwa sasa kutokana na hospitali iliyopo kuwa ndogo.


Na,Joel Maduka,Geita.
 
 
Hospitali ya rufaa Mkoani Geita inayojengwa Mtaa wa Magogo kata ya Bombambili mjini Geita inatarajiwa kuhudumia wagonjwa zaidi ya elfu moja wa nje na zaidi ya 480 watakaokuwa wakilazwa.
 
Akizungumza na waandishi wa habari walioambatana na Mwenyekiti wa bodi teule ya hospitali hiyo, Kaimu Meneja wa Wakala wa majengo mkoani Geita Mhandisi Gladys Jefta alisema katika hatua ya kwanza ya ujenzi wanaendelea na ujenzi wa majengo manne na wanatarajia kukamilisha baada ya miezi 9 ambapo umefikia asilimia 35.
 
“Tunatarajia  hospitali hii itakapokamilika itahudumia idadi ya wagonjwa wa nje zaidia ya elfu moja na wa kulazwa mia nne na themanini na tunaamini   ndani ya muda wa miezi mitatu ambayo tumeomba  kuongezewa tutakuwa tumekamilisha ujenzi,”alisema Mhandisi Gladys.
 
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali Teule ya mkoa wa Geita Bw ,Simon Rweyemamu alisema matarajio walitarajia Hospitali hiyo ingekamilika ndani ya miezi 9 lakini kukosekana kwa umeme na maji ndio sababu zilizokwamisha mradi huo kwa kuwa Mkandarasi amekuwa akinunua maji kutoka nje na wakati mwingine kutumia mafuta kwa ajili ya jenereta.
 
Kaimu mganga mkuu wa Mkoa wa Geita Dr Joseph Odero alisema hospitali ya rufaa ya sasa ambayo ilikuwa ya wilaya ni ndogo kwa kuwa ina uwezo wa kuhudumia wagonjwa  150 hadi 200 na wale wa kulazwa 200 hadi 250
na kwamba  hali ya wagonjwa kwa sasa ni kuanzia 300 hadi 350 hivyo kukamilika kwa hospitali hiyo ya rufaa kutasaidia kukabiliana na changamoto ya wingi wa wagonjwa.
 
Mradi wa ujenzi  wa hospitali ya rufaa kwa sasa umefikia asilimia 35 kwa hatua ya kwanza ambayo inatarajia kugharimu kiasi cha Sh Bilioni 5.9
Post a Comment