SHIRIKA LA NYUMBA LINAPENDA KUWAJULISHA WAPANGAJI WOTE KWAMBA KUANZIA TAREHE 01 JULAI, 2011 OFISI YA SHIRIKA LA NYUMBA ILIYOKO UPANGA ITAHAMISHIWA PLOT NO. 568/48 MTAA WA SAMORA, JENGO LA MATSALAMAT, GHOROFA YA KWANZA.
AIDHA HUDUMA ZOTE ZINAZOHUSU WAPANGAJI ZITATOLEWA KWENYE OFISI MPYA KUANZIA JULAI 01, 2011. WATEJA WATAENDELEA KULIPIA KODI YA PANGO KWENYE OFISI ZETU ZILIZOPO MTAA WA NKRUMAH.
TAWI LA UPANGA NI KUBWA KULIKO MATAWI YOTE YA SHIRIKA NA LINAHUDUMIA WAPANGAJI WENGI HIVYO NI VYEMA KUWA NA OFISI AMBAYO WATEJA WETU WATAPA HUDUMA ZENYE UBORA ZAIDI.
TUMEONA NI VYEMA KUWAARIFU WAPANGAJI WETU MAPEMA ILI KUWAONDOLEA USUMBUFU USIOKUWA WA LAZIMA.
KWA KUONA UMUHIMU WA SUALA LA MAKAZI SHIRIKA LIMEONA NI VYEMA KUTUMIA KIKAMILIFU THAMANI YA ARDHI ILIYOPO KATIKA ENEO HILI ILI KUWEZA KUWAPATIA WANANCHI MAKAZI ZAIDI.
JENGO LITAKALOJENGWA HAPA LITAKUWA NA SEHEMU ZA KUISHI TAKRIBAN 200 HIVYO WATU 1000 WATANUFAIKA KUISHI KATIKA ENEO HILI LITAKALOKUWA NA MIUNDOMBINU MUHIMU NA HUDUMA ZINGINE ZA KIJAMII KAMA VILE MADUKA, SEHEMU ZA KUCHEZA WATOTO, SEHEMU ZA KUEGESHA MAGARI NA KADHALIKA. HII NI KATIKA KUTEKELEZA AZMA YA KILIBADILISHA KABISA ENEO LA UPANGA.
KWA SASA ENEO LA UPANGA LINA WAPANGAJI 4,772 NA MAKUSANYO YA MWEZI NI ZAIDI YA SHILINGI BILIONI MOJA AMBAPO NI KARIBU ASILIMIA 40 YA MAKUSANYO YA KODI KATIKA MIKOA YOTE.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA
Comments