Maandalizi Kikao cha Bunge la Bajeti









JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


BUNGE LA TANZANIA



Simu Na. 022 2112065


Fax Na. (255) 022 2112538


E-mail: tanzparl@parliament.go.tz


(Barua zote za kiofisi ziandikwe kwa (KATIBU WA BUNGE)



Unapojibu tafadhali taja:





Ofisi ya Bunge


S.L.P. 9133


DAR ES SALAAM








Kumb. EB.155/172/01/300 31 Mei, 2011





YAH: WANAHABARI KWA AJILI YA BUNGE LA BAJETI


____________________




Tunayo furaha kukujulisha kuwa, Mkutano wa Nne wa Bunge la kumi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatarajiwa kuanza rasmi mjini Dodoma tarehe 7 Juni, 2011. Mkutano huu utakuwa wa Bajeti hivyo macho na masikio ya watu wengi yatakuwa yameelekezwa Dodoma kwa ajili ya kupata kile ambacho Serikali imekiandaa na kitakachopitishwa na Bunge kwa ajili ya mwaka wa fedha 2011/12.



Kama ilivyo kawaida tunategemea chombo chako kitatuma Wanahabari Dodoma kwa ajili ya habari za Mkutano huo.



Ofisi ya Bunge kila mara imekuwa ikitamani kupata toka kwako Wanahabari wenye uzoefu na uelewa wa kutosha juu ya masuala ya Bunge zikiwemo kanuni na taratibu zinazotawala chombo uendeshaji wa chombo hiki.



Aidha, ili kuwa na uratibu mzuri wa shughuli za utoaji Habari za Bunge, mwaka 2008 Wanahabari waliamua kuunda umoja wao kwa ajili ya kuwaunganisha katika shughuli hizi. Umoja huo uitwao Bunge Press Association of Tanzania (BUPAT) pamoja na mambo mengine unalenga kuwajengea uwezo Wanahabari na uwelewa mpana wa masuala ya Bunge.



Ni nia ya Ofisi ya Bunge kuuendeleza umoja huo ili hatimaye kujenga kada ya Wanahabari waliobobea katika utoaji wa Habari za Bunge. Katika kutekeleza azima hii, ofisi inaandaa mpango wa mafunzo utakaojumuisha semina, warsha na ziara za mafunzo katika Mabunge mbali mbali kwa Wanahabari husika.



Ni kwa misingi hiyo basi tumeona ni vyema tukapata ushirikiano wako katika hili na hivyo kukuomba kuwa kuanzia sasa unapoteua Wanahabari kwa ajili ya kwenda Bungeni wakidhi vigezo vifuatavyo:




  1. Wawe wamehudhuria Mikutano angalau mitatu

  2. Wawe na Press card inayotolewa na Idara ya Habari – Maelezo

  3. Wawe nadhifu, waadilifu na wenye nidhamu


Ili kutuwezesha kufanya maandalizi ipasavyo (vitambulisho, nyaraka, n.k) tutashukuru ukitupatia majina ya Wanahabari watakaohusika angalau siku nne kabla ya kuanza Mkutano wenyewe.



Tunatanguliza shukurani zetu za dhati kwa ushirikiano wako katika jambo hili.



Pamoja na salaam toka ofisi za Bunge.






J.S. Mwakasyuka


Kny: KATIBU WA BUNGE


Comments