MAHAKAMA YAMUACHIWA HURU MBOWE, YEYE AELEZEA JINSI ALIVYOCHUKULIWA NA NDEGE HADI ARUSHA


HATIMAYE Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, ameachiwa huru jana kwa dhamana na mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, huku wafuasi wake waliokuwa wamefurika mahakamani hapo wakimbeba juu kwa furaha nje ya mahakama hiyo.

Hatahivyo,mahakama hiyo pia imemkataa mdhamini wake wa awali Julius Margwe, kuendelea kumdhamini ,na kukubali mdhamini mwingine baada ya kuwa na shaka na mwenendo wa mdhamnini huyo,ambapo Diwani wa kata ya Elerai wa CHADEMA,John Bayo alijitokeza na kuwa mdhamini mpya wa Mbowe.

Akizungumza Mahakamani hapo Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Charles Magesa, alisema kuwa kutokana na mdhamini huyo kukiuka masharti ya kuhudhuria mahakamani hapo, ikiwa ni pamoja na mdhamini huyo kukabiliwa na kesi katika Mahakama ya Mwanzo Maromboso, hivyo mahakama imeamua kutoa nafasi kwa mdhamini mwingine.

Alisema kuwa mbali na kueleza uongo Mahakamani hapo kuwa alikuwa akifika mahakamani hapo, bado mahakama haina sababu naye sababu tayari ana kesi ya jinai ambayo hatma yake haifahamiki.

Kuhusu Mbowe Hakimu huyo alikiri kuwa ni kweli mahakama iliruhusu washitakiwa wabunge wahudhurie kikao cha bunge la bajeti na ila kutokana na kukosekana kwa mdhamini wake, ndiyo sababu walitoa amri ya kukamatwa kwake.

“Ila sasa mtaendelee na vikao vyenu vya bunge kama tulivyosema awali, ila wadhamini wenu lazima waje mahakamani kila kesi itakapotajwa na tunaondoa amri ya kukamatwa na sasa utaendelea na dhamana yako ya awali,” alisema Magesa.

Comments