Friday, July 21, 2006

Thursday, July 20, 2006

Tuesday, July 18, 2006

Ruaha Mkuu umekauka



Pichani unaweza kuona mawe yaliyochomoza yaliyokuwa mapito ya maji ya mto Ruaha Mkuu, Iringa. Mto huu unazidi kupungua sijui kama mgao wa umeme utakwisha picha hii ni ya Julai 16.

Madhari kavu



Tandala sio mbali na ilipo Ruaha National Park, huku ni wanyama tu. Zote hizi tunazo bado tunalia umasikini.

MGUSO WA UBINADAMU: SCARLET NA ATHMAN, TASWIRA YA UPENDO USIO NA MIPAKA


Waweza kujenga nyumba rahisi kama hii ingawa tatizo ni moto hebu tafadhalini naombeni kapsheni.


Katika kijiji kidogo cha Tosamaganga, Iringa, ndani ya ukuta wa kawaida wa Kituo cha Watoto Yatima cha Ipamba, simulizi ya kugusa moyo inaendelea kuandikwa kimya kimya. Hivi karibuni, kamera ilinaswa wakati mfanyakazi wa kujitolea raia wa Ujerumani, Scarlet Stirieber, alipokuwa akimnywesha uji mtoto mdogo yatima aitwaye Athman. Ni taswira ndogo, lakini yenye ujumbe mkubwa: upendo hauna mipaka ya lugha, utaifa wala rangi.

Athman ni mmoja wa watoto 200 wanaolelewa katika kituo hicho—watoto waliopoteza wazazi wao mapema, lakini ambao bado wana ndoto, tabasamu, na kiu ya kupendwa. Katika uso wa Scarlet, Athman anaona mama, dada, mlezi, na rafiki. Na kwa Scarlet, huduma hiyo si kazi ya huruma tu, bali ni wito wa moyo – kujenga ulimwengu wenye utu hata kwa njia ndogo kama kikombe cha uji.

Kituo cha Ipamba kinajitahidi kadri ya uwezo wake kutoa matunzo, lishe na malezi kwa watoto hawa, huku kikikabiliwa na changamoto nyingi za rasilimali. Hata hivyo, kupitia watu kama Scarlet, kinapata sababu ya kuendelea kusimama – sababu inayotokana na matumaini na mshikamano wa kibinadamu.

Katika dunia inayoendelea kukumbwa na migawanyiko, taswira ya Scarlet na Athman ni ukumbusho kwamba kila tendo la upendo, hata dogo, linaweza kuwa mabadiliko makubwa kwa maisha ya mtu mmoja. Na kwa watoto wa Ipamba, kila tabasamu ni ahadi ya kesho iliyo na mwanga.  (Picha na Yahya Charahani)

Tuesday, July 04, 2006

Mkapa aula Zimbabwe, Ulaya

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa. (Picha ilipigwa na Suleiman Kimaro wa Wizara ya Mambo ya Nje)

NEW YORK, UN

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Kofi Annan amejitoa katika juhudi za upatanishi wa kutatua mgogoro nchini Zimbabwe na nafasi yake imechukuliwa na Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa.

Uteuzi wa Mkapa ambaye alikuwa rais wa serikali ya awamu ya tatu ya Tanzania, kuchukua nafasi hiyo ya Annan, umefanywa baada ya kupata baraka za Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe.

Kutokana na uamuzi huo, Annan sasa hatafanya ziara ya kuitembelea Zimbabwe kama ilivyokuwa imeripotiwa awali.

Serikali za Afrika Kusini na Uingereza hivi karibuni zilieleza kuwa Annan angeweza kutoa mchango mkubwa katika kumaliza mgogoro za wa kiuchumi na na kisiasa unaoikabili Zimbabwe.

Annan alikutana na Rais Mugabe mjini Banjul, Gambia wiki iliyopita wakati wa mkutano wa wakuu wa serikali na nchi wanachama wa Muungano wa Afrika (AU) na kusema kuwa Mugabe alimweleza kuwa Mkapa ameteuliwa kuwa mpatanishi.

"Sote tumekubali kuwa Mkapa apewe nafasi na sehemu ya kufanyia kazi hii," Annan ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa, AFP.

Alipoulizwa iwapo bado ana mipango ya kufanya ziara nchini Zimbabwe, Annan alijibu kwa kusema: "Haiwezekani kuwepo wapatanishi wawili."

Mugabe alimbana Annan kuitembelea Zimbabwe mwaka jana, baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi (UN-Habitat), Anna Tibaijuka kuwasilisha ripoti iliyokosoa operesheni ya Zimbabwe ya kubomoa nyumba na kuwaondoa wafanyabishara waliodaiwa kujenga katika maeneo yasiyoruhusiwa katika miji mbalimbali, ukiwamo Harare.

Mei mwaka huu, Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini, alisema UN ilikuwa na mchango muhimu katika kutatua mgogoro wa kisiasa na kiuchumi nchini Zimbabwe, na kwamba ziara iliyokuwa imependekezwa kufanywa na Annan nchini Zimbabwe ingesaidia kuboresha uhusiano kati ya Zimbabwe na nchi za magharibi.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, alisema anaamini kuwa kuhusishwa kwa Annan kungesaidia kupatikana kwa mafanikio kwa wananchi wa Zimbabwe.

Afrika Kusini ilikwisha kueleza kuwa inaguswa sana na athari zilizokuwa zinaikabili Zimbabwe ambayo ni jirani yake.

Zimbabwe hivi sasa inakabiliwa na athari kubwa za kiuchumi ikiwa ni pamoja na kiwango cha juu cha mfumuko wa bei ambao ni zaidi ya asilimia 1,000 kwa mwaka na wananchi wengi wa nchi hiyo wameikimbilia nje, hasa Afrika Kusini.

Nchi nyingi za magharibi zinadai kuwa matatizo ya kiuchumi ya Zimbabwe yamesababishwa na sera mbovu za Mugabe. Hata hivyo, kwa upande wake, Mugabe anazishutumu nchi hizo kuwa zinahujumu uchumi wa nchi yake kwa lengo la kumwondoa madarakani kutokana na mpango wake wa mageuzi ya ardhi.

Wednesday, June 28, 2006

Suala si waliokopa tu, bali fedha zote za umma zafaa kurejeshwa

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu nchini HESLB imeamuru eti wahitimu wote walionufaika na mikopo tangu mwaka 1994/95 hadi sasa, wajitokeze na kuanza kuirejesha ili iweze kutumika kuwako pesha wengine, vinginevyo itawachukulia watu hao hatua za kisheria.

Agizo au tuseme kauli hii kimsingi siipingi maana ni nia yangu kuona Watanzania wengi tunasoma katika elimu ya juu, ingawa inachekesha kidogo kwa watu wapenda nchi wanaofikiri kwa kiwango hata cha kawaida tu.

Inachekesha kwa sababu kwanza, imetolewa kivitisho kama vile ina ugomvi na wakopaji, wakati hili ni suala la kawaida kueleweshana na kukumbushana.

Hivi inakuwaje unabagua wafaidika wa fedha za umma kwa makundi, eti hawa ndiyo wanaostahili kulipa na wengine uwaache, wakati unaowaacha ndiyo pengine waliotumia fedha nyingi kuliko hawa wa kipindi hiki, na ndiyo wenye uwezo mkubwa.

Suala la kurejesha fadhila za serikali si tatizo, wala siyo kitu cha ajabu, kosa ni kubagua watu na kujiondoa, maana wakati ule wakati bunge lilipokuwa likitunga sheria, kila mhitimu aliyekuwemo na aliyeona ‘kikombe’ kinamwelekea alikwepesha na badala yake wakaweka vigezo vilivyowakwepa wote.

Vipi waliosoma kuanzia miaka iliyopita tuchukulie hapa karibu tu kuanzia mwaka 1973 hao hawakuchukua fedha ya nchi? Walisomea pesa za nani na kwanini wasirejeshe?

Cha msingi hapa kingekuwa ni kuanzisha utaratibu ambao utawabana watu wote ambao kwa namna moja au nyingine walionufaika na fedha za umma, iwe na kukopa au kusomeshwa bure.

Natambua kuwa bodi za mikopo si mfumo mpya duniani, ni mfumo wa kawaida kabisa katika nchi nyingi. Bodi kama hizi hutoa dhana ya kulipia gharama za masomo ya wanafunzi na katika mfumo wa Ukabaila, hili halina swali.

Lakini kinachofanyika katika nchi zilizoendelea mathalani Marekani ni kuunda vituo vinavyohusiana na masuala ya msaada wa kifedha katika kila chuo. Vituo hivyo hutoa taarifa kwa kila mwanafunzi anapoomba kudahiliwa na chuo hicho.

Kama anataka kuomba mkopo pia basi hupewa fomu moja kwa moja kutoka katika chuo alichoomba na kisha kuzijaza sambamba na fomu ya kuomba udahili.

Mwanafunzi anapokubaliwa kujiunga na chuo anakuta masuala yake yanayoambatana na fedha yamekamilika na kazi yake inakuwa kuingia darasani na kupambana kutafuta ujuzi.
Kuendelea kuendekeza masuala kama haya ni kutaka kusababisha maandamano na upungufu wa amani katika jamii.

Kwa mtindo huu waliotunga sheria wanaweza kujiona wajanja kwa kuwalipisha baadhi na kujikwepa wao lakini naamini ipo siku nao wataingizwa tu katika mkumbo huu.

Kitu kingine ni kama serikali inataka ufanisi basi iepukane na hatari inayoweza kutokea kama haiwi makini kubaini matatizo yanayoikabili elimu ya juu nchini na badala yake inaishia kukaba baadhi na kuacha wengine.

Friday, June 09, 2006

Wamjua kijana mwenye fikra za kiuanamapinduzi

KILA kukicha teknolojia ya habari na mawasiliano inazidi kujipenyeza ndani ya jamii yetu na kwa hakika kuzidi kukineemesha kijiji chetu kilichokuwa na kaya chache sana, nyingi zikiwa mbalimbali mno. Lakini tofauti na mwaka jana na mwaka ulee sasa kijiji chetu kimesheheni miji mingine sasa ni mighorofa mikubwa jana katika pitapita yangu nimebahatika kupita katika kaya ya ndugu yangu wanamwita Steve Biko ni kijana machachari sana huyu katika masuala ya kuutetea uafrika na utanzania kwa ujumla, fikra zake ni za kiuanamapinduzi. Waweza bonya hapana kutazama nini alichoweka maana kama ujuavyo fikra za kiuanamapinduzi ni uanamapinduzi kweli!

RAIS DKT. MWINYI AFIKA MBWENI KUTOA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU MAMA FATMA KARUME

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi , akitoa pole kwa Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti...