Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akisalimiana na Rais wa Urusi Vladimir Putin katika hafla ya jioni iliyoandaliwa kwa ajili ya viongozi, wanaoshiriki Mkutano wa tatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika. Halfa hiyo imefanyika katika Ikulu ya Kremlin, Moscow nchini Urusi.
Dkt. Mwigulu amemuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo unaofanyika Oktoba 28 na 29, 2026, wenye lengo la kuwakutanisha viongozi wa Afrika na Urusi kwa ajili ya kujadili masuala ya kiuchumi, usalama, Sayansi na Teknolojia pamoja na masuala mengine ya kijamii.


No comments:
Post a Comment