Saturday, November 22, 2025

🔴🔴TABORA ZOO YAENDELEA KUNG'ARA KAMA KITOVU CHA ELIMU, BURUDANI NA UTALII WA NDANI










Na Mwandishi wetu, Tabora.

Bustani ya Wanyamapori Tabora (Tabora Zoo) imeendelea kujipambanua kama kivutio muhimu cha elimu na burudani jijini Tabora, hasa katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ambacho kimeonekana kuvutia wageni kwa wingi kutoka ndani na nje ya mkoa.

 Mnamo Novemba 21, 2025 Hifadhi hiyo ilipokea kundi la wanafunzi kutoka Chuo cha Ufugaji Nyuki Tabora (Beekeeping Training Institute – Tabora Branch) ambao  walitembelea Hifadhi hiyo kwa ajili ya ziara ya mafunzo, hatua inayodhihirisha jinsi bustani hii inavyozidi kuwa kitovu cha elimu ya vitendo kwa wanafunzi na wadau wa mazingira.

Uwepo wa wanafunzi hao umeongeza hamasa kwa vijana kutoka vyuo mbalimbali nchini ambao kwa sasa wanachagua Tabora Zoo kama sehemu ya kujifunza masuala ya uhifadhi, mienendo ya wanyamapori, na ekolojia kwa ujumla.

 Kadri mwamko wa utalii wa ndani unavyozidi kuongezeka, Tabora Zoo imeendelea kuwa chaguo namba moja kwa wanafunzi, familia na watalii wanaotafuta mahali pa kujifunza, kupumzika na kufurahia vivutio halisi vya maliasili. 

Kwa kasi hii, bustani hiyo inaendelea kuwa moja ya maeneo muhimu yanayochangia kukuza uelewa wa mazingira na kuimarisha utalii wa ndani katika Mkoa wa Tabora.

No comments:

🔴🔴TABORA ZOO YAENDELEA KUNG'ARA KAMA KITOVU CHA ELIMU, BURUDANI NA UTALII WA NDANI

Na Mwandishi wetu, Tabora. Bustani ya Wanyamapori Tabora (Tabora Zoo) imeendelea kujipambanua kama kivutio muhimu cha elimu na burudani jiji...