Matukio mbalimbali wakati wa sherehe za kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli mkoani Arusha tarehe 22 Novemba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 22 Novemba 2025, amehudhuria na kuongoza sherehe za kutunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, mkoani Arusha.
Katika hafla hiyo, Mhe. Rais Samia aliwasili katika viwanja vya chuo hicho na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Jeshi, kabla ya kusimama kwa heshima wakati Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Akiendelea na ratiba ya sherehe, Mhe. Rais alikagua Gwaride rasmi la kumaliza mafunzo, linalojumuisha Maafisa Wanafunzi wa kundi la 06/22 (Shahada ya Sayansi ya Kijeshi), kundi la 72/24-Regular, pamoja na wahitimu wa mahafali ya sita ya Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Kijeshi.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali, ndugu, jamaa na marafiki wa wahitimu wakishuhudia hatua muhimu kwa maafisa wapya wanaojiunga rasmi katika kulitumikia Taifa kwa uadilifu, uzalendo na nidhamu ya kijeshi.
#Tanzania #JWTZ #TMA #Monduli #UlinziNaUsalama #Kamisheni2025












No comments:
Post a Comment