Sunday, November 16, 2025

KAMISHNA WA UHIFADHI TANAPA AFANYA ZIARA YA KIKAZI KITUO CHA MALIKALE – MTWA MKWAWA, IHINGA, IRINGA




Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), CPA Musa Nassoro Kuji,  amefanya ziara ya kikazi katika Kituo cha Malikale cha Makumbusho ya Mtwa Mkwawa, kilichopo Kalenga, mkoani Iringa, ikiwa sehemu ya utaratibu wa kawaida wa kukagua na kuimarisha utendaji katika vituo mbalimbali vya urithi wa taifa.

Akiwa katika ziara hiyo, Kamishna Kuji alipata fursa ya kukutana na familia ya Mtwa Mkwawa inayoongozwa na Mtwa Abdu Adam Sapi Mkwawa – Mfwimi II, Chifu wa sita wa ukoo wa Mtwa Mkwawa (Kabila la Wahehe).

 Mazungumzo yao yalijikita katika njia bora za kuimarisha usimamizi wa Makumbusho ya Mtwa Mkwawa, kuendeleza mahusiano na jamii inayouzunguka, pamoja na kuhakikisha historia, tamaduni na asili ya kabila la Wahehe zinaendelea kuhifadhiwa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Kamishna Kuji ameahidi ushirikiano wa karibu kati ya TANAPA, viongozi wa ukoo pamoja na jamii, ili kuhakikisha kituo hicho muhimu cha kihistoria kinaendelea kuwa rejea na fahari ya utamaduni wa Mtanzania.


#tanapaupdates #MtwaMkwawaMuseum #MalikalezaTANAPA #TanzaniaParks #tumerithishwatuwarithishe

No comments:

KAMISHNA WA UHIFADHI TANAPA AFANYA ZIARA YA KIKAZI KITUO CHA MALIKALE – MTWA MKWAWA, IHINGA, IRINGA

Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), CPA Musa Nassoro Kuji ,  amefanya ziara ya kikazi katika Kituo cha Malikale ch...