Na Mwandishi wa NCAA, Karatu.
Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) Bw. Abdul-Razaq Badru ameeleza kuwa kusimamia na kuendeleza uhifadhi ni jukumu la msingi kwa mamlaka hiyo kwani uhifadhi ndiyo moyo katika ustawi wa utalii na maendeleo ya jamii.
Akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika ofisi za makao makuu Karatu Arusha leo tarehe 7 Novermba, 2025 Kamishna Badru amesisitiza kuwa, usimamizi madhubuti wa rasilimali za wanyamapori, Misitu na Malikale zilizopo hifadhi ya Ngorongoro ni jambo la kufa na kupona na kueleza watumishi hao kuwahudumia wageni wanaotembelea hifadhi kwa wakati, ukarimu, uadilifu na nidhamu ili kuendelea kulinda chapa ya Ngorongoro (Brand) kama eneo bora la utalii wa kifahari (Premium Safari Destination)
“Jukumu la msingi kwa kila mtumishi wa Ngorongoro ni Uhifadhi kisha mengine yanafuata, uhifadhi na ulinzi wa rasilimali ni jambo la kufa na kupona, hivyo nawasisitiza kuhakikisha kila mmoja anakuwa mlinzi wa rasilimali hizo.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo Naibu Kamishna anayeshughulikia uhifadhi,utalii na maendeleo ya jamii Joas Makwati ameeleza kuwa idadi ya watalii imeendelea kuongezeka ambapo robo ya kwanza iliyoishia Septemba 2025 zaidi ya watalii 350,000 wametembelea Ngorongoro.
Kwa upande wake Naibu Kamishna anayeshughulikia huduma za shirika Aidan Makalla amewataka watumishi kuwa wazi kuchangia maendeleo ya mamlaka kwa kuendelea kutoa ushauri,maoni na Mtazamo katika majukumu ya taasisi ili kuhakikisha huduma zinaendelea kuwa bora na endelevu.




No comments:
Post a Comment