Thursday, July 19, 2018

WAZIRI LUKUVI AONGOZA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA SHELTER AFRIQUE- KENYA


Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Vangimembe  Lukuvi ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa 37 wa Makazi Afrika (Shelter Afrique) ulioanza leo jijini Nairobi akizungumza na wanachama wa mkutano huo (hawapo pichani). Mkutano huo ambao una wanachama kutoka nchi 44 za Afrika wanakutana katika nchini humo ili kujadili changamoto za hali ya makazi kwa watu wa nchi hizo ili kuona namna ya kutatua changamoto hizo kwa kutumia uzoefu wa kila nchi mwanachama.

 Mambo mbalimbali yanajadiliwa katika mkutano huo ikiwa ni pamoja na kuondoa changamoto ya Rasilimali Fedha inayozikabili nchi nyingi wanachama wa Umoja huo na kushindwa kuwapatia wananchi wa Afrika makazi bora na nafuu. 

Kwa ujumla changamoto za nchi za kiafrika katika kuwapatia wananchi wa kawaida makazi nafuu zinafanana na kilio kikubwa katika nchi wanachama, ambazo ni  kuwepo makazi holela hata baada ya nchi hizo kujikomboa kutoka ukoloni mkongwe.

Tanzania ni nchi mojawapo Mwanachama wa Shelter Afrique kati ya nchi 44 za barani Afrika ilijiunga na Shelter Afrique mwaka 2003 na Mkutano wa 32  ambao ulifanyika N’djamena, Chad 2013, uliopitishwa na Azimio Namba GM/ 2013/005 la kuongeza Hisa kwa kila nchi mwanachama kwa lengo la kukuza mtaji wa Kampuni hiyo na kuiwezesha kuweka nguvu zaidi katika masuala ya uendelezaji nyumba barani Afrika. Mkutano wa mwaka huu unafanyika Jijini Nairobi katika hoteli ya Windsor.

Aidha, katika Mkutano huo ambapo Tanzania iliwakilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi, Mkurugenzi wa Nyumba wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Pius Tesha, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Utoaji Mikopo kwa Benki na Taasisi za fedha kwa ajili ya mikopo wa nyumba Tanzania (TMRC), Oscar Mgaya Pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Maendeleo ya Biashara wa NHC William Genya.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Nyumba wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Pius Tesha huku wajumbe wengine wakishuhudia.
Ujumbe wa Tanzania Mkutano wa 37 wa Makazi Afrika (Shelter Afrique) ukifuatilia mkutano huo wa leo wa kwanza kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Utoaji Mikopo kwa Benki na Taasisi za fedha kwa ajili ya mikopo wa nyumba Tanzania (TMRC), Oscar Mgaya, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi, Mkurugenzi wa Nyumba wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Pius Tesha na Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Maendeleo ya Biashara wa NHC William Genya.



 Ujumbe wa Tanzania Mkutano wa 37 wa Makazi Afrika (Shelter Afrique) ukifuatilia mkutano huo wa leo wa kwanza kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Utoaji Mikopo kwa Benki na Taasisi za fedha kwa ajili ya mikopo wa nyumba Tanzania (TMRC), Oscar Mgaya, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi, Mkurugenzi wa Nyumba wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Pius Tesha na Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Maendeleo ya Biashara wa NHC William Genya.


 Ujumbe wa Tanzania Mkutano wa 37 wa Makazi Afrika (Shelter Afrique) ukifuatilia mkutano huo wa leo.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Vangimembe  Lukuvi akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi nchini Kenya jana.
Waziri wa Ardhi na Upimaji wa Kenya, Mama Farida Karoney akijadiliana masuala mbalimbali na ujumbe wa Tanzania kwenye makao makuu ya wizara hiyo nchini Kenya. Mheshimiwa Waziri Lukuvi alifanya ziara ya kikazi katika Wizara ya Ardhi na Upimaji nchini Kenya jana tarehe 18 Julai, 2018 ambapo pamoja na mambo mengine Waziri alitaka  kujua mifumo ya upimaji, ugawaji, umiliki na utawala wa ardhi wa nchini Kenya.

Waziri wa Ardhi na Upimaji wa Kenya, Mama Farida Karoney akijadiliana jambo na Waziri Lukuvi kwenye makao makuu ya wizara hiyo nchini Kenya.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Vangimembe  Lukuvi akizungumza kwenye mkutano wa alipofanya ziara ya kikazi katika Wizara ya Ardhi na Upimaji nchini Kenya jana (18 Julai, 2018) ambapo pamoja na mambo mengine Waziri alitaka  kujua mifumo ya upimaji, ugawaji, umiliki na utawala wa ardhi wa nchini Kenya.




No comments: