Saturday, July 28, 2018

NHC YASAINI MKATABA NA HALMASHAURI MPYA YA WANGING'OMBE ILIYOPO MKOANI NJOMBE

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akitiliana saini mkataba wa ujenzi wa jengo la Utawala na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Athony Emmanuel Mawata huku wakishuhudiwa Mkuu wa Huduma za Sheria wa Shirika la Nyumba laTaifa, Martin Mdoe  Utiaji saini makubaliano hayo umefanyika leo asubuhi katika Ofisi za Halmauri hiyo na kuhudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Emmanuel Kirundo na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Athony Emmanuel Mawata na watumishi waandamizi wa Halmashauri hiyo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akipeana mkono na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Athony Emmanuel Mawata baada ya kusaini mkataba huo.
Picha ya pamoja ya viongozi hao.

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) leo limesaini mkataba na Halmashauri ya Wilaya Mpya ya Wangingómbe iliyopo Mkoani Njombe ya Ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri hiyo wenye thamani ya shilingi bilioni 2.7.

Utiaji saini makubaliano hayo umefanyika leo asubuhi katika Ofisi za Halmauri hiyo na kuhudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Emmanuel Kirundo na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Athony Emmanuel Mawata na watumishi waandamizi wa Halmashauri hiyo.
Akizungumza wakati wa utiaji saini huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi alisema ujenzi wa jengo hilo unaotarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja utaanza ndani ya wiki mbili kuanzia sasa.
“Ni jengo litakalokuwa na ofisi nyingi za viongozi na wataalamu wa Halmashauri na pande zote mbili tuko tayari kutekeleza majukumu ya kimkataba,”alisema.
Akizungumza wakati wa utiaji saini huo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Emmanuel Kirundo alisema wameamua kulikabidhi Shirika hilo dhamana ya ujenzi wa jengo hilo kubwa lenye nafasi ya kutosha kutokana na uwezo lililo nao Shirika hilo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Athony Emmanuel Mawata
 alisema wamepitia michakato mingi katika kumtafuta mkandarasi bora atakayejenga jengo hilo na hatimaye wakafikia hatua ya kukabidhi ujenzi wa jengo hilo kwa NHC kutokana na ubora wa kazi zilizokwishawahi kufanywa na Shirika hilo.

No comments: