Tuesday, July 24, 2018

TANZANIA YATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA MKUTANO WA 37 WA SHIRIKA LA MAKAZI AFRIKA 2018

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi ambaye alikuwa Mwenyekiti akiwa na wenyeviti wenza wa Mkutano wa 37 wa Shelter Afrique wakiongoza ajenda mbalimbali zilizowasilishwa katika Mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Windsor jijini Nairobi Kenya.

Kaimu Mkurugenzi wa Nyumba wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Pius Tesha, akipitia na kusikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zinajadiliwa na Wajumbe kutoka nchi 44 za Afrika waliohudhuria Mkutano huo uliofanyika katika Jiji la Nairobi nchini Kenya.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi, akifuatilia ajenda mbalimbali zilizowasilishwa katika Mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Windsor jijini Nairobi Kenya.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi, akifuatilia ajenda mbalimbali zilizowasilishwa katika Mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Windsor jijini Nairobi Kenya.

Tanzania imeteuliwa kwa kauli moja na wajumbe wa Mkutano wa 37 wa Makazi Afrika (Shelter Afrique) kuwa Mwenyekiti wa Mkutano wa 37 wadhifa ambao atautumikia kwa mwaka mmoja na kukabidhi madaraka katika mkutano utakaofanyika mwezi Julai 2019 Jijini Rabat, Morocco. Mkutano huo ambao una wanachama kutoka nchi 44 za Afrika walikutana katika jiji la Nairobi nchini Kenya ili kujadili changamoto za hali ya makazi kwa watu wa nchi hizo ili kuona namna ya kutatua changamoto hizo kwa kutumia uzoefu wa kila nchi mwanachama. 

Aidha, katika Mkutano huo ambapo Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi, iliteuliwa kuwa Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo wa 37. 

Tanzania ilijiunga na Shelter Afrique mwaka 2003 na Mkutano wa 32 wa Shelter - Afrique uliofanyika N’djamena, Chad mwaka 2013 ulipitisha Azimio Namba GM/2013/005 la kuongeza Hisa kwa kila nchi mwanachama kwa lengo la kukuza mtaji wa kampuni hiyo na kuiwezesha kuweka nguvu zaidi katika masuala ya uendelezaji nyumba barani Afrika.

Shirika la Nyumba la Taifa limenufaika na mtaji huo ambapo mwaka 2002 lilikopeshwa Dola za Kimarekani 1.5 milioni na kuzitumia kujenga nyumba 212 eneo la Boko Jijini Dar es Salaam na mwaka 2011 lilikopeshwa fedha kiasi cha Dola za Kimarekani 14.5 milioni mkopo uliotakiwa kurejeshwa katika kipindi cha miaka 10 na mkopo huo ulitumika kujenga nyumba za gharama nafuu zipatazo 558 katika maeneo mbalimbali nchini. Pamoja na kuikopesha NHC, Shelter Afrique imewekeza kiasi cha Dola za Kimarekani 27,500,000/= katika miradi mbalimbali ya ujenzi wa nyumba nchini Tanzania.

No comments: