Friday, January 19, 2007

Masikini tulie tuu hatuna chetu!

UNAWEZA kutuita jina lolote unalotaka, na kisha ukatudharau na kutupachika kila unaloona linafaa. Mara sisi ni wavivu wa kufikiri, mara eti mikopo ipo ila tumelala hatuichukui. Ebo tutaichukuaje wakati hali yenyewe ndiyo hii. Nasikitika nazungumzia sisi masikini.

Masikini katika ardhi yetu hii ya mama yetu Tanzania, tutaendelea kuwa masikini hata iweje na mipango yote inayoanzishwa wala haiwezi kutulenga kamwe, bali itakuwa inawalengeni ninyi wenye unafuu wa maisha.

Na itawafanya muwe matajiri wa kufuru kwa mgongo wetu, na siyo mgongo wetu tu, bali hata jasho letu la damu na machozi yetu, na hamtakaa mkajua tunateseka vipi hadi na nyinyi muwe kama sisi jambo ambalo haliwezekani. Soma zaidi kwa kubonya hapa:

1 comment:

Anonymous said...

Inasikitisha kuona pengo kati ya matajiri na mafukuru linakuwa kama tofauti kati ya usiku na mchana.Bado kazi ni ngumu.

RAIS SAMlA AFANYA MAZUNGUMZO NA MJUMBE MAALUM WA RAIS TSHISEKEDI

  Dar es Salaam, 26 Machi 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan , amekutana na kufanya mazungu...