Balozi Mahalu kizimbani

ALIYEKUWA Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, kwa makosa sita ya uhujumu uchumi, wizi na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh2 bilioni.

Balozi Mahalu alitiwa mbaroni na maafisa wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa (Takuru) pamoja na watu wengine wawili waliokuwa maofisa wa Ubalozi wa Tanzani nchini humo ambao nao wanaohusishwa na tuhuma hizo. Wengine ni Steward Migwano ambaye alikuwa Mtunza Fedha na Grace Martin ambaye alikuwa Afisa Utawala ubalozini hapo.

Watuhumiwa hao walifikishwa katika mahakama hiyo ya Kisutu asubuhi ya leo wakiwa kwenye gari la Takuru aina ya Toyota Landcruiser lenye namba za usajili T385 ALK na kusomewa mashtaka hayo yanayohusiana na upotevu wa Euro 2,065,827.60 wakati wakiwa maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Italia. Euro ni sawa na Sh1,692.74.

Comments