Friday, October 06, 2006

Mambo ya mgawo hayo



Mpitanjia akipita kwa uangalifu katika jenmereta zinazofua umemekuingiza katika maduka yaliyopo mtaa wa Mchikichi Kariakoo jijini Dar es salaam, wateja katika maduka hayo wanadai kuna makelele mengi yanayotokana na jenereta hizo. Unapofika katikati ya jiji unaweza kuliita jiji la Dar es Salaam, jiji la makelele kila mtaa ni tak tak tak !!!!

6 comments:

mloyi said...

Nimekupata live leo, bado upoo?

Kelele zimezidi sasa, juzi niliona kwenye jarida la Jitambue wanaelezea jinsi kelele za jenereta zinazoweza kuua mtu, lakini sisi bado tunayapenda.
Mateso aliyokuwa wanapewa Saadam na na wafungwa wa Guantnamo Bei nawamarekani yaliyofanya Dunia iyapigie ilikuwa ni kupigiwa makelele makali sana, bado sisi tunajikita kwenye hiyo hali ya makelele.
Kwani hakuna jenerta zisizo na kelele?

mzee wa mshitu said...

yesss kaka Mloyi unalosema ni la kweli kabisa wenzetu wamekimbia kabisa haya makelele kiasi kwamba hata magari, majenereta sijui kila kitu kinachopiga kelele hakitakiwi. Tunapaswa tukimbilie katika hizo nishati mbadala, kwani kwa mfano mtu anayenunua jenereta akitumia solar pannels atakosa nini kama si mazoea tuu!!!

MICHUZI BLOG said...

Charahani!

Umesema kweli, lakini ah! Tufanyeje? Mi nadhani ni kuvumilia huku tukipiga kelele kifanyike cha kufanyika ili tuache kuwa tegemezi wa umeme wa chupa ya chai (therma?). Vinginevyo hongera kwa habari za picha, ni rahisi kusoma na kutoa maoni.

mzee wa mshitu said...

Michuzi!!!

Nafurahi sdaana mzee kwa mheshimiwa kama wewe kutembelea kibanda changu hiki , nashukuru saana kmwa ushauri wako na ninaendelea kufanyia kazi.

Hongera sana na wewe kwa jinsi ulivyoweza kutuhabarisha hasa hili tukio la karibuni la hawa ndugu zetu Walter Mazula na Vonetha Nkya kwa jinsi ulivyoenda nalo tanngu Marekani hadi mazishi hongera sana ingawa bado tuko katika majonzi.

NDABULI said...

Hapo sidhani kuna utaratibu wa kujikinga na hatari(safety precautions) hapo moja ikileta mushkeli ikalipuka sijui kama hapo kama wamjetayarisha kwa hilo,kwa kuwa na vitu kama kizima moto(fire extinguisher)na vitu kama hivyo. Hongera mzee kwa kutuhabarisha

Simon Kitururu said...

Hii Kali!