Friday, April 28, 2006

Kijiji cha Mwananchi kimewaka moto

Haya tena wanablogu wenzangu kumekucha tena safari hii nawaleteeni wanablogu wawili matata kweli kweli. Wa kwanza huyu ni bosi wangu katika masuala ya spoti afahamika sana kama Angetile Osiah au Mzee wa Ujerumani, amebobea katika fani hii wengine hupenda kumwita kisima cha fikra michezoni, nadhani hata kuwa mgeni kwenu waweza kumtembelea kwa kubofya hapa. Na mwingine ni mwanamama huyu, Mzanzibari ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii, ni hazina tosha ya fikra za kisiasa na kijamii, aweza kukusisimua kwa kuipata vyema historia ya Zanzibar na maeneo mengine, jinale Hawra Shamte, waweza kumpata kwa kubonya hapa. Haya mambo yanazidi kuwa mambo bloguni.

3 comments:

Egidio Ndabagoye said...

Poa sana kaka kwa kutuletea "hivyo Vichwa" bloguni

boniphace said...

Yahya lazima nikuletee zawadi ya tende maana unanivalisha nguo sasa kila nipitapo.

Reggy's said...

Mzee wa mshitu naona Waziri wa Teknolojia (MK) kashakutembelea. Huyu bwana achana naye anajenga nyumba za Tanzania akiwa UK, "Kinana apewe sifa' Amen

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AMWAKILISHA WAZIRI WA FEDHA KATIKA KONGAMANO LA 16 LA MWAKA LA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI – ARUSHA

Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Mhandisi Mshamu Ali Munde, amemwakilisha Waziri wa Fedha katika ufunguzi wa Kongamano la 16 la Mwaka la Wa...