Monday, April 10, 2006

Safari ya Mtwara hapa katika picha ya juu ni Mavuji, Kilwa huko Lindi wakati picha ya chini tupo katika mtumbwi wa injini kuelekea Mingoyo


9 comments:

John Mwaipopo said...

Huo mtumbwi hamkuuzidi nguvu kweli?

mzee wa mshitu said...

Mwaipopo,

Hatukuuzidi nguvu. Huu si najua ni dizaini ya ile mitumbwi mikubwa wanayooiita boti, ila ilikuwa kasheshe tulivyofika katika matuta ya mchanga ilibidi kuingia katika mtumbwi mdogo ambao kanuni yake ni lazima ukae hakuna kusimama.

boniphace said...

Wewe mwanangu angalia kila mtu humo mtumbwini anawaza kupoteza maisha tu. Hkauna life jackets na tunasafiri kwa majaliwa ya mola tu. EE bwana hii yanikumbusha safari za kuelekea Irungwa na ukara. Sijui kama sasa hivi naweza kuwa na ujasiri wa kupanda boti hizo ambazo naziita mitumbwi tu.

mzee wa mshitu said...

Boni

Sijui kama utaweza kuwa na ujasiri huo kwa sasa, wakati ule uliweza kumudu kupanda sababu ulikuwa ukiona kila kitu sawa hivi sasa utapanda mtumbwi na mitazamo elfu moja na moja.

Wacha yale ya Ukara na Irungwa ni baab kubwa maana ukiwa humo lazima uwe na makokoro ili kwenda kutega furu na sato wachache waliobakia na hata vitegemezi vyao.

ARUPA said...

hivi wewe charahani hauogopi maji? kwa kweli mimi siwezi kupanda mtumbwi kwani sisi morani heri uliwe na simba kuliko samaki aibu!

mwandani said...

Bwana Charahani unaijua mitaa yote inazunguka visiwa vya ukerewe... Unanikumbusha nilikotoka

mzee wa mshitu said...

Ndugu yangu Nambiza

Naifahamu vyema miji karibu yote inayozunguka katika kisiwa cha Ukerewe kuanzia Muriti, Bukindo
Bukongo, Igalla, Ilangala, Kagunguli, Murutunguru, kwao mama yangu Namagondo, Nansio, Kisorya mpaka Bugorora upo hapo ndugu yangu.

Mpaka kule wanapokula jimfulu na jinsatu pamoja na bhusima wakitumia. Upo hapo ndugu yangu. Au nikukumbushe zaidi

Kazonta usiogope maji mbona nyinyi mnasafiri na ng'ombe wenu toka kule umasaini hadi kwao kina Mwaipopo na hamuogopi wanyama wakati(joke).

Rama Msangi said...

Maisha haya bado yangalipo Tanzania hata baada ya miaka karibu 50 sasa ya uhuru wa NJI hii. Halafu unajua nini ndugu yangu Charahani? Hapo likitokea janga basi wenye hako ka-usafiri na Sirikali kwa pamoja watakurupuka na kutoa tamko eti la kuvibana vyombo vya usafiri viwe na vifaa vya kuokoa watu pindi ajali ikitokea. Kawimbo haka umeanza kukasikia lini? Na hadi leo hii naamini hakajapata tuzo yoyote ile, sidhani kama kamefanikiwa kuwaingia watu akilini. Mbona ulikuwa hujabeba hata kapochi kakuwekea tule tusamaki tudogodogo tunakopenda kuruka ruka angani ukatuletea?

mzee wa mshitu said...

Msangi

Unayosema ni ya kweli kabisa, lakini umesahau kimoja nacho ni ule wimbo wa Tume, ambazo nazo zinakula fedha nyingi za umma ambazo ni kodi za wananchi walalahoi na wavuja jasho wa taifa hili na si za wakwepa kodi na majambazi.

Begi nilikuwa nimeliweka hapo katikati kama unavyoona watu waliokaa katikati.