Friday, January 31, 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA WAZIRI NA MANAIBU WAZIRI IKULU DAR

01Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri na Manaibu Waziri waliokuwa wakiapisha Ikulu Dar es Salaam wakati alipokuwa akiwasili katika hafla hiyo. Picha na OMR02Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Ummy Mwalimu, kuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR03Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha George Boniface Tuguluvala Simbachawene, kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR04Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Kaika Saning’o Telele, kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR05Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR06.Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakia katika picha ya pamoja na Waziri na Manaibu Waziri walioapishwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR
07Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wapya na wa zamani wa Ofisi yake, baada ya kuapishwa wapya katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Kutoka (kulia) ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Muhangwa Kitwanga, ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano)Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu na aliyekuwa Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Terezya Huvisa, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR

Thursday, January 30, 2014

NAIBU WAZIRI WA MAJI AZURU DAWASA NA DAWASCO

IMG_0417Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, akisaini Kitabu cha Wageni katika Ofisi za DAWASA. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA, Said El Maamry na Kulia ni Mkurugenzi wa DAWASA, Archad Mutalemwa.IMG_0464Mkurugenzi wa DAWASA, Archad Mutalemwa akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala na katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA, Said El Maamry.IMG_0480Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, akizungumza katika mkutano alipotembelea DAWASA.IMG_0560Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Jackson Midala akimwonyesha ripoti ya DAWASCO, Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO.IMG_0587Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Jackson Midala akimwonyesha ripoti ya DAWASCO, Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO.
………………………………………………………………………..
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala jana alitembelea DAWASA na DAWASCO kuzungumza na uongozi wa taasisi hizo nchini zenye dhamana ya kusimamia huduma za maji katika mkoa wa Dar es Salaam na miji midogo ya Kibaha na Bagamoyo.
Mhe. Makala ametembelea taasisi hizo na kuzungumza na menejimenti na bodi za taasisi hizo ili kufahamu maendeleo na utendaji wa taasisi hizo katika kuleta matumaini ya huduma bora za maji katika mkoa wa Dar es Salaam na mji midogo wa Kibaha na Bagamoyo.
“Tuna chanagamoto ya upatikanaji wa maji, lakini kama Serikali ni jukumu letu kuhakikisha tunalipatia ufumbuzi ”, alisema Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala.
“Hatuna budi kuweka mikakati sahihi na kutekeleza kwa kasi miradi inayoendelea ili wananchi wapate maji na waliopewa dhamana ya usimamiaji watekeleze kwa wakati”, alisema Naibu Waziri.
Pia, Mhe. Makala amedhamiria kutatua tatizo sugu la wizi wa maji na kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wahusika na akasisitiza wahusika lazima wachukuliwe hatua kali.
Aliongeza suala la upotevu wa maji liwe ni ajenda ya kudumu ili kuhakikisha linakwisha na kuziasa DAWASA na DAWASCO zisiwe chanzo cha matatizo, bali watafute ufumbuzi wa tatizo la maji.
Mkurugenzi wa DAWASA, Archad Mutalemwa alisema DAWASA imeweka mikakati ya upanuzi wa mitambo na mifumo ya maji, ujenzi wa bwawa la Kidunda na kuthibiti maji yanayopotea kuhakikisha inaboresha huduma zake.
Aidha, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Jackson Midala alisema mikakati waliyojiwekea ni kupunguza madeni wanayodai wateja wake, kufunga mita kwa wateja wote na kuongeza uzalishaji ili kuongeza ufanisi wa mamlaka hiyo.
Hii ni mara ya kwanza tangu Mhe. Makala ateuliwe kuwa Naibu Waziri wa Maji kutembelea taasisi hizo zinazotoa huduma ya maji jijini Dar miji midogo wa Kibaha na Bagamoyos.
Ziara hiyo itaendelea kwa Naibu Waziri wa Maji kutembelea miradi ya maji ya Ruvu Chini na Juu na maeneo ya Segerea na Ubungo.

Wednesday, January 29, 2014

JK AFURAHISHWA NA HUDUMA ZA NMB KATIKA MPANGO WA KILIMO WA STAKABADHI GHALANI

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa kitengo cha Masuala ya Kilimo katika Benki ya NMB Bw. Robert Pascal alipotembelea banda lao leo baada ya kufungua kongamano la kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es salaam leo.
  Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo ya jinzi mpango wa Stakabadhi Ghalani ulivyo na manufaa kwa mkulima toka kwa Mkuu wa kitengo cha Masuala ya Kilimo katika Benki ya NMB Bw. Robert Pascal alipotembelea banda lao leo baada ya kufungua kongamano la kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa kitengo cha Masuala ya Kilimo katika Benki ya NMB Bw. Robert Pascal akitoa maelzo kwa Rais Kikwete juu ya mafanikio ya benki hiyo katika mpango wa Stakabadhi Ghalani ambao amesema unaendeshwa kwa mafanikio makubwa.

DROO KUBWA YA MILIONI 50/- YA MIMI NI BINGWA YAKARIBIA‏


Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akisisitiza jambo wakati akichezesha droo ya kumi ya promosheni ya Mimi ni Bingwa liyofanyika jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Muwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Bw. Emmanuel Ndaki.
Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akizungumza na mmoja wa washindi wa promosheni ya Mimi ni Bingwa aliyepatikana katika droo ya kumi ya promosheni  hiyo iliyochezeshwa jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es salaam na kumtangaza Msemwa George Makuzi kama mshindi wa tiketi mbili za kwenda Old Trafford.

1.     Droo kubwa ya milioni 50/- ya Mimi ni Bingwa yakaribia
2.     Airtel yajipanga kwa droo kubwa ya milioni 50/- ya ‘Mimi ni Bingwa’
WAKATI washindi wa tiketi wa awamu ya kwanza ya promosheni ya ‘Mimi ni Bingwa’ wakitarajiwa kuwasili nchini Alhamis, kampuni hiyo ya simu imechezesha droo nyingine na kumchagua mkazi wa jijini Dar es Salaam, Msemwa George Makuzi kuwa mshindi wa tiketi mbili za kwenda Old Trafford katika wiki ya kumi ya droo hiyo.
Akizungumza mara baada ya droo hiyo, Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde alisema kilele cha promosheni hiyo kinakaribia, ambacho tutashuhudia mshiriki wa ‘Mimi ni Bingwa’akiondoka na kitita cha shilingi milioni 50 katika droo kubwa itakayohusisha kila aliyejisajili katika promosheni hiyo.
“Tukiwa tunafikia kilele cha promosheni ya ‘Mimi ni Bingwa’, nataka niwahakikishie wateja wote wa Airtel kuwa washiriki wapya bado wanakaribishwa kutokana na kuwa mshindi wa pesa taslim ya milioni 50 atapatikana kupitia droo ya bahati nasibu.
“Kupitia droo hii kubwa, ndiyo tutajua ni nani ataondoka na zawadi kubwa ya ‘Mimi ni Bingwa’. Kutokana na vigezo na masharti ya promotion hii, kila namba iliyosajiliwa kwa ajili ya promosheni, hata kama mshiriki alijibu swali moja tu, ataingia katika droo kubwa.
“Hii sasa ni nafasi kwa wateja wa Airtel ambao hajajisajili kwenye promosheni kujisajili kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno “BINGWA” kwenda namba 15656, na kujibu maswali mengi iwezekanavyo, na unaweza kuwa mshindi wa zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 au zawadi nyingine za milioni 1 kila siku na milioni 5 kila wiki kwa wiki zilizobaki,” alisema Jane.
Alisema kuwa ‘Mimi ni Bingwa’ imeonyesha mafanikio makubwa kwa kuwa imepokelewa vizuri na wateja waliojisajili kwa wingi na kujikusanyia pointi kwa kujibu maswali mengi yaliyorahisi yanayoulizwa.
Jane aliongeza kuwa Airtel itaendelea kuanzisha promosheni na kampeni mbali mbali zinazolenga kuwazawadia wateja wake pamoja na kuyabadilisha maisha yao na kuwa washiriki mahiri wa kuubadilisha uchumi wa Tanzania. 
Alibainisha kuwa washindi wote wa tiketi za safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford watasafiri kabla ya mwisho wa mwezi wa Februari, huku akiongeza kuwa mkakati ni kuwawezesha washindi kwenda Uingereza katika awamu tatu tofauti.
Katika droo hiyo ya wiki ya kumi, Bi Hawa Mohammed Hussein kutoka Tanga na Godlove William Kayonga kutoka Mara walijishindia shilingi milioni 5 kila mmoja na washindi wengine 12 kujinyakulia shilingi milioni 1 kila mmoja.
Washindi wengine wa tiketi za ‘Mimi ni Bingwa’ ni pamoja na Edwin Edmund Kajimbo kutoka Iringa, Michael Joseph Shirima kutoka Kinondoni jijini Dar es Salaam, Bw. Shaibu Rashid Dege, Mtendaji wa kijiji cha Nang’olo wilayani Kilwa – mkoani Lindi, Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Joseph Steven Mambo kutoka Kawe jijini Dar es Salaam, Emmanuel Mahenge Jacob kutoka Njiro in Arusha, Rashid Jacob Kagombola kutoka Bukoba mkoani Kagera, Harrison Wilson Mwambogolo kutoka Kigogo jijini  Dar es Salaam na Salma Farid Mughery kutoka Dar es Salaam.

MKUTANO WA UZINDUZI WA KAMPENI ZA UDIWANI KWA CCM KATA YA NDULI

 

 Kada  wa  CCM Frederick Mwakalebela  na Simon Belege  kushoto  wakiwa katika mkutano  huo
Na  Francis Godwin Blogu
CHAMA cha mapinduzi ( CCM) wilaya ya Iringa mjini kimezindua kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Nduli jimbo la Iringa mjini huku katibu wa CCM wilaya hiyo Hassan Mtenga amemtaka mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi kumbana mbunge mchungaji Peter Msigwa ili kuonyesha mamilioni ya shilingi ambayo anadai yalitolewa na mfanyabiashara Sabodo kwa ajili ya kusaidia maji wananchi wa jimbo la Iringa wakiwemo wa Nduli. Mbali ya katibu huyo kumwagiza meya kufuatilia fedha hizo ili kujua kazi ambayo zilifanya pia Meya Mwamwindi ameueleza umati mkubwa wa wananchi waliofika katika mkutano huo kazi chache ambazo anazitambua alizozifanya mbunge Msingwa kwa miaka yake miwili akiwa mbunge.

Imedaiwa  mfanyabiashara  Sabodo mwaka  jana  alinukuliwa na  vyombo vya  habari akijitolea fedha  za uchimbaji  wa visima  vya maji kwa  wabunge wote  wa majimbo wa  CHADEMA kama njia ya  kumaliza kero  ya  maji majimboni mwao ila  hadi sasa jimbo la  Iringa mjini eneo la  Kigonzile  kata  hiyo ya  Nduli wananchi  wake  wanashida kubwa ya maji.

 Mwamwindi alitaja kazi hizo kuwa ni pamoja na kugawa mipira kata zote 16 isipo kuwa Nduli,kupeleka vitanda visizo chakavu katika Hospitali ya wilaya ya Iringa mjini (Frelimo) vitanda ambavyo hadi sasa havitumiki ,pamoja na kutoshindwa kushiriki vikao vya baraza la madiwani kwa miaka miwili kabla ya kulalamikiwa na kazi nyingine ambayo amekuwa akiifanya ambayo haina faida kwa wana Iringa ni kupigania ujangili wa Twiga na Tembo hali akijua jimboni kwake hakuna hifadhi ya wanyama. Pia Mwamwindi alipongeza jitihada zinazofanywa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) kwa kujenga kituo cha polisi kusaidia ufunguzi wa Hospital ya wilaya , kusaidia kusomesha yatima, kuwezesha wanawake kiuchumia na kazi nyingine nyingi.

 Hata hivyo alisema mbali ya kuwa katika mfuko wa jimbo kuna kiasi cha Tsh milini 30 ambazo zimetolewa na Rais Jakaya Kikwete ila wajumbe wa mfuko huo wamekuwa wakishindwa kukutana kutoa maamuzi juu ya fedha hizo kutokana na mbunge kuonyesha kuwazunguka na kugoma kukaa vikao. 
Mwamwindi alisema kuwa serikali ya CCM katika kata hiyo ya Nduli pekee imefanikisha kusogeza maendeleo kwa wananchi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa daraja katika kijiji cha Kigonzile pamoja na kufikisha usafiri wa daladala ambapo toka nchi ipate uhuru wananchi hao kwa sasa wanapata usafiri , pia kwa nduli ujenzi wa shule ya sekondari pamoja na kupeleka mradi kubwa wa maji unaogharimu zaidi ya Tsh milioni 70 mradi ambao mbunge wao amekuwa hauungi mkono kutokana na kususa siku ya uzinduzi.

 Huku kwa upande wake aliyekuwa mshindi wa kura za maoni katika mchakato wa ndani ya CCM mwaka 2010 Frederick Mwakalebela akiwataka vijana na wananchi wa kata ya Nduli kumchagua mgombea udiwani wa CCM Bw Benitho Mtove kuwa ndie atakayefanikisha maendeleo ya jimbo la Iringa na kata ya Nduli. 

Akihotubia huku akishangiliwa na umati wa wananchi waliofika katika mkutano huo Mwakalebela alisema bado anaheshimu jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya CCM chini ya rais Kikwete na kuwa ili kasi ya maendeleo iendelee kuwepo wananchi wa Nduli hawana budi kuchagua CCM na sio kuchangua mpinzani. 

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu aliwataka wananchi wa Nduli katika kumuenzi diwani aliyefariki duni Idd Chonanga kutobabaika na kauli za Msingwa na badala yake kuchagua diwani wa CCM. 

Hata hivyo mgombea huyo wa udiwani Bw Mtove ambae hakutaka kumzungumzia mbunge Msigwa wala mgombea wa Chadema udiwani katika kata hiyo ,alisema anahakika atafanya kazi ya kuwatumikia wananchi wa Nduli na kuomba tarehe 9 kumpa kura zote za ndio.

KAMPUNI YA REX ENERGY YATAMBULISHA TEKNOLOJIA MPYA YA KUHIFADHI NA KUSAMBAZA UMEME

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kusambaza vifaa vya umeme wa jua (solar) ya Rex Energy Bw Francis Kibhisa akizungumza na Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),kuhusiana na uzinduzi na utambulisho wa teknolojia  mpya yenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi na kusambaza Umeme,mkutano huo umefanyika mapema leo asubuhi kwenye makao makuu ya ofisi hizo zilizopo mtaa wa Makamba,Gerezani jijini Dar.
Pichani mbele kushoto ni Ofisa Mauzo wa kampuni ya Rex…
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kusambaza vifaa vya umeme wa jua (solar) ya Rex Energy Bw Francis Kibhisa akizungumza na Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),kuhusiana na uzinduzi na utambulisho wa teknolojia  mpya yenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi na kusambaza Umeme,mkutano huo umefanyika mapema leo asubuhi kwenye makao makuu ya ofisi hizo zilizopo mtaa wa Makamba,Gerezani jijini Dar.
Pichani mbele kushoto ni Ofisa Mauzo wa kampuni ya Rex Energy,Bwa.Medard Rweikiza pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,Bwa.Francis Kibhisa wakiwaonesha na kuwaeleza baadhi ya Waandishi wa Habari namna moja ya kifaa cha kisasa kabisa chenye uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme kwa kutumia Mwanga wa Jua (Solar).
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy,Bw.Francis Kibhisa akitoa ufafanuzi wa namna moja ya kifaa (pichani),kinachotumia teknolojia ya kisasa katika suala zima la kuzalisha umeme kwa kutumia mwanga wa jua (Solar Power) mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),Bwa.Francis alibainisha kuwa kifaa hicho kina uwezo wa kuwasha vifaa vya ndani kama vile taa,redio, friji, TV kwa wakati mmoja,na huuzwa kwa gharama nafuu.Pichani kulia ni Ofisa Mauzo wa kampuni ya Rex Enegy,Bw.Medard Rweikiza akisikiliza
Baadhi ya  Wafanyakazi wa Kampuni ya Rex Energy wakiwa katika picha ya pamoja mara baada kumaliza mkutano wao na Waandishi wa habari mapema leo asubuhi.

MAKUNGA, KIBANDA, MWIGAMBA WASHINDA KESI YA UCHOCHEZI

Theophil Makunga.
Absalom Kibanda.
Samson Mwigamba.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam  imetoa hukumu ya kesi ya makala iliyodaiwa kuwa ya uchochezi iliyokuwa inawakabili Meneja Uendeshaji Biashara wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Theophil Makunga, Mwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima ambaye sasa ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006), Absalom Kibanda  ambapo wameibuka kidedea baada ya ushahidi upande wa mashitaka kutojitosheleza. SOURCE: RADIO ONE STEREO

Msajili wa Hazina, Fitch Ratings watathmini mageuzi ya taasisi za umma

Na Mwandishi wa OTR Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) Jumanne, Agosti 11, 2026, ilifanya mazungumzo na  Fitch Ratings Ltd  amb...