Waziri
 wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye 
Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akikabidhi tuzo ya mshindi wa pili ya mwajiri bora wa mwaka 2018 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Omari Makalamangi katika 
hafla ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha 
Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba. 
Waziri
 wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye 
Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akikabidhi tuzo ya mshindi wa pili ya
 mwajiri bora wa mwaka 2018 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa 
Shirika la Nyumba la Taifa, Omari Makalamangi katika 
hafla ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha 
Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba. 
 Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa 
Shirika la Nyumba la Taifa, Omari Makalamangi akiwa na maafisa Rasilimaliwatu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Godlove Godwin na Neema Msita katika 
hafla ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha 
Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba.
 Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Omari Makalamangi akiwa na maafisa wa Shirika la Nyumba la Taifa, Abeld Joram na Neema Msita katika hafla ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Omari Makalamangi akiwa na maafisa wa Shirika la Nyumba la Taifa, Abeld Joram na Neema Msita katika hafla ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Omari Makalamangi akiwa na maafisa Rasilimaliwatu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Godlove Godwin na Neema Msita katika hafla ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akikabidhi tuzo ya mshindi wa pili ya mwajiri bora wa mwaka 2018 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Omari Makalamangi katika hafla ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba.
Tuzo mbili za mshindi wa pili za Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 za Mwajiri bora wa ndani na mwajiri bora katika sekta ya umma katika hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Omari Makalamangi akiwa ameshikilia tuzo ya mwajiri bora baada ya kuipokea kutoka katika hafla ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba.
Mwakilishi
 wa Tanzania Cigarette Company (TCC), akipokea Tuzo ya Mwajiri Bora wa 
Mwaka 2018 baada ya kampuni hiyo kuibuka washindi afasi ya tatu katika 
hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa
 Mlimani City, tarehe 14 Disemba mgeni rasmi akiwa Waziri wa Nchi Ofisi 
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. 
Jenista Mhagama (MB).
Mwakilishi
 wa Tanzania Breweries Limited (TBL), Bi. Lilian Makau akipokea Tuzo ya 
Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 baada ya Kampuni hiyo kuibuka washindi nafasi
 ya pili katika hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania 
(ATE) katika ukumbi wa Mlimani City, tarehe 14 Disemba mgeni 
rasmi akiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, 
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB).
Wafanyakazi
 wa Geita Gold Mine (GGM) wakifurahiya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 
2018 pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, 
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) baada ya 
kampuni hiyo kuibuka washindi nafasi ya kwanza kwenye 
hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa
 Mlimani City, tarehe 14 Disemba 2018.
…………………………………………………………….
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE),
 Disemba 14 2018 kimeandaa Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 
zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City. Tangu 
kuanzishwa kwake mwaka 2005, tuzo hizo zimejikita katika kutambua 
waajiri wenye misingi bora ya usimamizi wa guvu kazi na rasilimali watu 
kwa lengo la kuwawezesha kutimiza wajibu wao kikamilifu na kupelekea 
kukuza uzalishaji wa kibiashara. 
Tuzo hizo zilihudhuriwa na wadau 
mbali mbali wakiwemo Mh. Jenista Mhagama, Mh. Anthony Mavunde, Mhe. 
Stella Ikupa, Mkuu wa Mkoa DSM, Mhe. Paul Makonda, Balozi wa Norway 
nchini, Bi. Elisabeth Jacobsen, Balozi wa Denmark nchini, Bw. Einer H. 
Jensen na Balozi wa China nchini Nd. Wang Fe, pamoja na taasisi mbali 
mbali ikiwemo TUKTA na ILO.
Tuzo hizo zinazofanyika kila 
mwaka zimasaidia kuhamasisha wanachama kuchukulia masuala ya ajira na 
usimamizi wa rasilimali watu kama misingi muhimu katika kumwezesha 
mwajiri kuwana wafanyakazi wenye uwezo na ueledi ili kukidhi mahitaji ya
 ushindani katika biashara.
Sherehe ya utoaji tuzo 
iliyohudhuriwa na Mhe. Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi Ofisi ya 
Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akiwa 
Mgeni Rasmi, zimekuwa maarufu hapa nchini katika muktadha wa biashara 
hasa kwa kuhamamasisha makampuni makubwa na madogo na ya ukubwa wa kati 
kuhusu umuhimu wa kuzingatia misingi bora ya kufanya biashara nchini.
Tuzo hizo ambazo kwa mwaka 2017 
ziliboreshwa kwa kuongezewa vipengele 12 vipya vya Hali nzuri kwa 
Wafanyakazi (Employee Wellness), Kuvutia na kutunza wafanyakazi wenye 
ujuzi (Attraction and Retention), Mahusiano Mazuri Mahali pa Kazi 
(Industrial Relations), Kujali kazi na maisha nje ya Kazi (Work Life 
Balance), Mwajiri anayekubalika na Kufahamika (Employer Branding), 
Usimamizi wa Wafanyakazi kwa kuzingatia Umri (Managing an Aging 
Workforce), Uwekezaji katika Teknolojia (Technology Investment), Tuzo 
kwa ajili ya Sekta Binafsi (Private Sector Award), Tuzo kwa Sekta ya 
Umma (Public Sector Award), Tuzo kwa Ajili ya Mashirika ya Kijamii ( 
Civil Society Award) na Tuzo ya Mwajiri Mzawa (Indigenous Employer 
Award) , zitaendelea na vipengele hivyo vipya kwani vinatoa fursa kwa 
wanachama kufanyia kazi vipengele hivyo kwa lengo la kuboresha mazingira
 ya kazi na ajira kulingana na mahitaji ya waajiri nchini.
Akizumgumza na wageni waalikwa 
Mgeni Rasmi, Mhe. Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri 
Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu alisema kwamba 
serikali inatambua mchango wa waajiri kutoka sekta zote na itaendelea 
kushirikiana nao pamoja na Vyama vya Wafanyakazi na wananchi kwa ujumla 
katika kutimiza azma ya nchi yetu kujitegemea. 
Mhe. Jenista Mhagama aliongeza 
kuwa serikali chini ya uongozi wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungazo wa 
Tanzania, Dr. John Joseph Magufuli imebeba jukumu la kuboresha 
miundombinu katika nyanja za usafirishaji wa anga, reli na maji, afya, 
nishati, elimu na mawasiliano ambayo kwa kiasi kikubwa zinaongeza 
uzalishaji wa nchi kupitia waajiri wa sekta binafsi na umma.
Aidha Mh. Mhagama alipongea Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa shughuli zake mbali
ikiwemo Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka, Mkutano Mkuu wa Kwanza wa
 Uongozi kwa Mwaka2018, Mwanamke wa Wakati Ujao inayofanyika kwa 
ushirikiano na Shirikisho la Vyama vya
Waajiri nchini Norway (NHO) kutoa mafunzo kwa wanawake ili waweze kushika za juu za
uongozi katika makampuni na taasisi mbali mbali ambapo tangu kuasisiwa kwake mwaka 2016, wanawake 66 wamehitimu mafunzo hayo.
 
Akiongea na wageni waalikwa, Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Jayne
Nyimbo Taylor alishukuru serikali ya awamu ya tano kwa juhudi zake katika kuboresha
mazingira ya kufanya biashara nchini kama punguzo la tozo 
inayolipwa na waajiri kwa ajili ya kukuza ujuzi mahali pa kazi maarufu 
kama “Skills Development Levy (SDL)” kutoka 6% mpaka kufikia 4.5% huku 
akiiomba serikali kuipunguza tozo hiyo hadi kufikia 2%. 
Pamoja na mapendekezo hayo, Bi. 
Jayne Nyimbo pia aligusia changamoto mbali mbali zinazowakabili waajiri 
kama ufuatiliaji wa vibali vya kufanya kazi nchini, utaratibu wa malipo 
ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ambapo sekta binafsi wanalipa 1%
 huku waajiri wa umma wanalipa 0.5% ya mshahara anaolipwa mfanyakazi, 
aina mikataba ya ajira pamoja na tozo na faini zinazotozwa na Mamlaka ya
 Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA).
Aidha kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania(ATE), Dkt.
Aggrey K. Mlimuka, alitoa shukrani zake za dhati kwa Mgeni 
Rasmi, Mhe. Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu 
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, wageni waalikwa na 
wadau mbali mbali waliofanikisha Tuzo ya Mwajiri wa Mwaka 2018. “Naomba 
nikushukuru tena Mhe. Mgeni Rasmi, na Washiriki wote kwa kuja kujumuika 
na sisi katika utoaji wa Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018, na naamini 
kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa kushikiana na TUCTA pamoja na Serikali
 hasa tunapoendelea kujenga nchi yetu kuelekea uchumi wa kati ifikapo 
mwaka 2025. Naomba kutumia fursa hii pia kuwashukuru na kuwapongeza 
wanachama wote walioshiriki katika zoezi hili hasa kwa kujaza dodoso ili
 kupata fursa ya kulinganisha utendaji wa makampuni yao na ya wengine.” 
Alisema Dkt. Mlimuka.
“Naomba kuhitimisha salamu zangu kwa kuwatambua uwepo wa baadhi ya wanachama na
wadau wetu kwa michango yao ambayo imetuwezesha kufanikisha 
utoaji wa tuzo hii ambao ni wafuatao.” Alimalizia Dkt. Mlimuka. Kuhusu 
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ni 
chombo pekee cha waajiri
 








No comments:
Post a Comment