SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LAKABIDHI MASHINE ZA KUFYATULIA TOFALI KWA JESHI LA MAGEREZA

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na huduma kwa jamii Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Yahya Charahani (mwenye shati jeusi) akikabidhi mashine za kufyatulia tofali kwa Afande Hassan Lindenge wa Jeshi la Magereza na Afande Lwesya wakati wa kukabidhi mashine za kuengenezea matofali ya kisasa yanayoendana na hali ya udongo na miamba ya eneo husika. Mashine hizo zitatumika na Jeshi la Magereza kufyatua matofali yatakayotumika katika ujenzi wa majengo mbalimbali ya jengo hilo.

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi mashine za kisasa za kufyatua matofali kwaajili ya kusaidia kusukuma mbele shughuli mbalimbali za ujenzi za jeshi la Magereza  nchini.
Mashine hizo zilikabidhiwa kwa Kamanda Hassan Lindege wa Bohari Kuu ya Magereza kwenye ofisi za NHC Temeke kwenye hafla fupi na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na huduma kwa jamii Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Yahya Charahani.
Katika hafla hiyo Kamanda Lindenge alilishukuru Shirika la Nyumba la Taifa kwa kuwezesha utoaji wa mashine hizo kwani zitasaidia kwenye shughuli mbalimbali za ujenzi wa jeshi hilo na akaahidi kupeleka wataalamu wa jeshi hilo kwenye mafunzo ya ufyatuaji tofali kwa taasisi ya NHBRA.
Akikabidhi Mashine hizo Charahani kwa Kamanda Lindenge alisema mashine hizo zitawasaidia Jeshi la Magereza kujenga nyumba za gharama nafuu kwa kutumia matofali yanayoingiliana bila kutumia udongo yatakayofyatuliwa kwa kutumia mashine hizo za kisasa.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Kaimu Meneja wa NHC Temeke, Injinia Renald Kazoba alisema mashine hizo ambazo ni bora kabisa za gharama nafuu zikitumika vyema zitaweza kuwazalishia Jeshi la Magereza matofali mengi sana na hivyo kuwapunguzia gharama za ujenzi na kuongeza ubora wa kazi.

 Kaimu Meneja wa NHC Temeke, Injinia Renald Kazoba akionyesha namna mashine hizo zinavyofanya kazi.
 Kaimu Meneja wa NHC Temeke, Injinia Renald Kazoba akitoa maelezo ya  namna mashine hizo zinavyofanya kazi.

 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na huduma kwa jamii Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Yahya Charahani(mwenye shati jeusi) akikabidhi mashine za kufyatulia tofali kwa Afande Hassan Lindenge wa Jeshi la Magereza wakati wa kukabidhi mashine za kuengenezea matofali ya kisasa yanayoendana na hali ya udongo na miamba ya eneo husika. Mashine hizo zitatumika na Jeshi la Magereza kufyatua matofali yatakayotumika katika ujenzi wa majengo mbalimbali ya jengo hilo.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na huduma kwa jamii Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Yahya Charahani (wa pili kulia) wakati wa kukabidhi mashine za kuengenezea matofali ya kisasa yanayoendana na hali ya udongo na miamba ya eneo husika. Wanaosikiliza ni Kaimu Meneja wa NHC Temeke, Injinia Renald Kazoba na Afande Hassan Lindenge na Afande Lwesya wa Jeshi la Magereza.

Comments