MKURUGENZI MKUU AAGIZA WAFANYAKAZI WA NHC KUCHAPA KAZI KWA BIDII ILI KUINUA MAPATO YA SHIRIKA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk Maulidi Banyani leo ameanza ziara ya kikazi mkoani Mwanza huku akiagiza wafanyakazi wa NHC kuchapa kazi kwa bidii na kuzingatia weledi ili kuinua mapato ya Shirika na kuwahudumia wananchi wengi kwa ufanisi zaidi. 

Akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza ameagiza NHC mkoa wa Mwanza kuchangamkia fursa kwa kujenga nyumba za kuishi wafanyakazi mkoani Simiyu ambao uko chini ya usimamizi wa mkoa wa Mwanza.

“Ninachoagiza ni ushirikiano baina ya wafanyakazi na miongoni mwa wafanyakazi nataka viongozi na wafanyakazi muwe na umoja.  Hivi karibuni nitawaita mameneja wote makao makuu tutajadiliana na kutoa msimamo.  tunataka kulirudisha Shirika kwa watu kwa maana ya kwamba kujenga nyumba za gharama nafuu,” amesema.

“Tunataka tujenge nidhamu ya utendaji tekeleza jukumu lako umalize mpaka mwisho tutapima ufanisi kwa siku.  Niwasihi sana mabadiliko yatakapoanza kila mtu acheze ngoma yake kwa kadri inavyowezekana. Siku nyingine tutazungumza mambo yetu ya ndani, siku hiyo mtakuwa huru.”

Pia alipata fursa ya kutembelea miradi 12 ya ubia, iliyokamilika ikiwa ni mitatu mmoja unaendelea na mingine aidha imefutwa au imesimama na akaagiza kwa wale walishindwa kutekeleza mikataba ya ubia wandikiwe barua za kuwataka walilipe Shirika kwa kulipotezea mapato shirika, kwenye miradi yenye kesi isubiri zimalizike na ile miradi ambayo imesimama ifanyiwe structure stability and analysis ili kuweza kuona ubora wake ili hatua zaidi zichukuliwe.

Akiwa katika mradi wa Buswelu aliagiza zifanyike jitihada ili nyumba zilizosalia kuuzwa katika awamu ya kwanza zifanyike jitihada ya kuziuza zimalizike zote na hata za awamu ya pili, lakini pia kuwe na mpango wa kuongeza stock ya mali za Shirika kwa kubakisha majengo mapya yaliyojengwa na Shirika kwa Shirika ili ziweze kuongeza thamani na kuendelea kupangishwa, 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk Maulidi Banyani akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk Maulidi Banyani akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Mwanza.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk Maulidi Banyani akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Mwanza (hawapo pichani).
Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Mwanza wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Dk Banyani.

 Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Mwanza wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Dk Banyani,

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk Maulidi Banyani akisaini kitabu cha wageni alipowasili ofisi za NHC Mwanza.
Jengo la ubia kati ya NHC na mbia lililopo katika kitalu nambari 45/1 T Mtaa wa Rwagasore.  
Mojawapo ya majengo ya ubia yaliyopo kwenye barabara ya Nyerere mkoani Mwanza.
Mojawapo wa maeneo ya Shirika la Nyumba la Taifa yaliyovunjwa nyumba ili kuendelezwa na mbia lakini baadaye mbia akashindwa na eneo likarejeshwa kwa NHC. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk Maulidi Banyani akiangalia ramani ya eneo kulikojengwa nyumba za makazi ya Buswelu wakati alipotembelea mradi wa nyumba za makazi za Buswelu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk Maulidi Banyani akitembelea eneo la mradi wa nyumba za makazi za Buswelu zilizopo mkoani Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk Maulidi Banyani akitembelea eneo la mradi wa nyumba za makazi za Buswelu zilizopo mkoani Mwanza.
 Nyumba za makazi za Buswelu zilizopo mkoani Mwanza zinavyoonekana.

 Mojawapo ya majengo ya ubia yaliyopo kwenye barabara ya Nyerere mkoani Mwanza.
 Mojawapo ya majengo ya ubia yaliyopo kwenye barabara ya Nyerere mkoani Mwanza.


 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk Maulid Banyani akitembelea eneo la mradi wa nyumba za makazi za Buswelu zilizopo mkoani Mwanza.




Nyumba za makazi za Buswelu zilizopo mkoani Mwanza


 

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk Maulidi Banyani na timu yake wakitembelea miradi ya nyumba za ubia jijini Mwanza hapo ni eneo la Rwagasore jijini Mwanza.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk Maulidi Banyani akitembelea eneo la mradi wa nyumba za makazi za Buswelu zilizopo mkoani Mwanza. 

Mmoja wa wabia wa NHC, Bw. Seif akimuonyesha jambo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk Maulid Banyani wakati akikagua jengo la ubia kati ya NHC na mbia huyo. 

Akitoa taarifa ya utekelezaji ya Mkoa wa Mwanza, Meneja wa NHC Mkoa wa Mwanza Joseph John alisema kuwa Mkoa wa Mwanza una nyumba 122, viwanja tupu 8, sehemu za JV ziko 12. Zilizokamilika 3, unaoendelea mmoja na mingine imesimama,  

Kuhusu hali ya ukusanyaji mapato ya kodi alisema mkoa umekusanya kiasi cha shilingi milioni 488, malimbikizo shilingi milioni 200 kwa wapangaji na extenant shilingi milioni 319, madeni mengine yataendelea kufuatiliwa. 

Kuhusu hali ya matengenezo alisema kuna uchakavu wa mapaa na matatizo ya mifumo ya maji taka, mapaa nyumba 16, mifumo ya maji taka 40, mabomba mabovu 80.




Comments