Friday, December 21, 2018

MKURUGENZI MKUU NHC AHIMIZA UKUSANYWAJI WA MALIMBIKIZO YA WADENI WA NHC

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akitembelea eneo la Buhare, Musoma mkoani Mara zilipojengwa nyumba za gharama nafuu za Buhare mkoani Mara, kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara, William Genya na Kaimu Mkuu wa Ukaguzi wa Ndani wa Shirika la Nyumba la Taifa, Abdallah Migila.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akitembelea jengo la Mukendo Commercial Complex lililopo mtaa maarufu wa Mukendo mjini Musoma mkoani Mara, kushoto kwake ni Kaimu Meneja wa NHC Mkoa wa Mara, Clifford Massau. Jengo la Mukendo la awamu ya kwanza limepangishwa lote na sasa awamu ya pili ya jengo hilo inakamilishwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akitembelea eneo la Buhare, Musoma mkoani Mara zilipojengwa nyumba za gharama nafuu za Buhare mkoani Mara, kushoto kwake ni Kaimu Meneja wa NHC mkoa wa Mara Clifford Masau, Kaimu Mkurugenzi wa Ubunifu, Margareth Minja, Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara, William Genya.

Nyumba za gharama nafuu za Buhare mkoani Mara zinavyoonekana.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akifuatilia maelezo ya Mhandisi anayesimamia ujenzi wa jengo la Mukendo Comercial Complex kutoka kampuni ya Kiure Engineering leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akitoa maelekezo kwa Mhandisi anayesimamia ujenzi wa jengo la Mukendo Comercial Complex kutoka kampuni ya Kiure Engineering leo.




Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za NHC mkoa wa Mara alipofika leo kumalizia awamu ya pili ya ziara yake kwa mikoa ya kanda ya ziwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akiwasili katika ofisi za NHC mkoa wa Mara na kukaribishwa na mmoja wa watendaji wa Shirika mkoani Mara alipofika leo kumalizia awamu ya pili ya ziara yake kwa mikoa ya kanda ya ziwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa ofisi za NHC mkoa wa Mara alipofika leo kumalizia awamu ya pili ya ziara yake kwa mikoa ya kanda ya ziwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akiagana na Nyabugumba Jonathan wa ofisi za NHC mkoa wa Mara alipofika leo kumalizia awamu ya pili ya ziara yake kwa mikoa ya kanda ya ziwa


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akitembelea kushuhudia ujenzi unaoendelea wa jengo la Mukendo Comercial Complex  linalojengwa na mkandarasi kampuni ya Kiure Engineering kwa niaba ya NHC.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akitembelea nyumba za gharama nafuu za Buhare mkoani Mara.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akitembelea kushuhudia ujenzi unaoendelea wa jengo la Mukendo Comercial Complex  linalojengwa na mkandarasi kampuni ya Kiure Engineering kwa niaba ya NHC.




Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akitembelea eneo la Buhare, Musoma mkoani Mara zilipojengwa nyumba za gharama nafuu za Buhare mkoani Mara. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akitembelea eneo la Buhare, Musoma mkoani Mara zilipojengwa nyumba za gharama nafuu za Buhare mkoani Mara.





Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akitembelea jengo la Utawala la Chuo Cha Kilimo la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililopo Butiama mkoani mara. Jengo hilo linajengwa na NHC kama utekelezaji wa sera ya huduma kwa jamii.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akielekeza jambo alipokuwa akitembelea eneo la Buhare, Musoma mkoani Mara zilipojengwa nyumba za gharama nafuu za Buhare mkoani Mara.
Jengo la Utawala la Chuo Cha Kilimo la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililopo Butiama mkoani mara. Jengo hilo linajengwa na NHC kama utekelezaji wa sera ya huduma kwa jamii.
Picha ya pamoja mbele ya Jengo la Utawala la Chuo Cha Kilimo la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililopo Butiama mkoani mara. Jengo hilo linajengwa na NHC kama utekelezaji wa sera ya huduma kwa jamii.
Picha ya pamoja mbele ya Jengo la Utawala la Chuo Cha Kilimo la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere lililopo Butiama mkoani mara. Jengo hilo linajengwa na NHC kama utekelezaji wa sera ya huduma kwa jamii.

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&


Akizungumza wakati akiwa katika ofisi za NHC mkoa wa Mara, Dk Banyani alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kujitambulisha na kuwaeleza wafanyakazi mwelekeo mpya wa Shirika la Nyumba la Taifa kwa sasa ambao ni kujikita kwenye kuwafikia wananchi na kuwajengea nyumba za gharama nafuu.


"Tumefanya kazi kubwa sana huko nyuma kwa kujenga haya majengo makubwa ya ghorofa ili kuwafika wananchi wa viwango vyote, lakini sasa tunajikita zaidi kuwafikia wananchi wengi zaidi,älisema.


Alisisitiza wafanyakazi kila mmoja atekeleze wajibu wake ili kuliimarisha shirika liende mbele kwa kushirikiana na kuzingatia maadili ya Shirika yaliyopo kwenye mpango mkakati wa Shirika.


"Tujenge ari mpya ya kufanya kazi kwa kujiekeza na kujiandaa na mabadiliko wakati wowote, kitu pekee kisichobadilika ni mabadiliko yenyewe, lakini maisha ya binadamu na shughuli zake yanabadilika,"alisema.

Aliagiza kwamba popote panapotakiwa kujengwa nyumba basi inabidi tutafiti kwa kina na kufahamu mahitaji yao ili tuweze kujenga nyumba bora, siyo kuwakadiria wananchi. 


Pia alitaka madeni ya extenants na madeni mengine yote ya malimbikizo yafuatiliwe kwa kina ili kuweza kuwa na ufanisi katika Shirika, kwani ofisi isiyokusanya kodi ni sawa na ofisi siyofanya kazi.


Kuhusu matengenezo, alisema utaratibu mpya wa matengenezo utazingatia zaidi ufanisi na uwajibikaji na matengenezo yatazingatia vigezo kadhaa ikiwamo vyanzo vya uharibifu kama umesababishwa na mpangai au yale yaliyosababishwa na hali ya hewa au mazingira mengine.

Eneo la Buhare ni kubwa sana lenye mita za mraba za ukubwa 135,2 wakati eneo lililojengwa nyumba ni mita za mraba 10 tu.

No comments: