SERIKALI KUONDOA KABISA MFUMO WA KIZAMANI WA MALIPO YA KODI

Mwakilishi wa Mfumo wa Malipo ya Kidijitali wa Serikali- Government Electronic Payment (GePG), Basil Baligumya akitoa semina kwa Menejimenti na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa  juu ya namna mfumo huo unavyofanya kazi  ambapo alisema Serikali imekusudia kuondoa kabisa mfumo wa kizamani wa malipo ya kodi za Serikali na kujikita katika mfumo huo wa kidijitali na kwamba hadi sasa taasisi za serikali takribani 260 zimejisajili kwenye mfumo huo ikiwemo Halmashauri, Brela, Tanesco, Dawasco na nyinginezo.

Mfumo huo wa serikali kwa ajili ya kulipia huduma zote za serikali, kumrahisishia mwananchi kulipa kupitia mitandao ya simu, unatengeneza namna ambayo inafanana katika kulipia huduma zote za serikali kwa taasisi zilizounganishwa ikiwemo halmashauri, huduma za umeme, maji. 

Mwakilishi wa Mfumo wa Malipo ya Kidijitali wa Serikali- Government Electronic Payment (GePG), Basil Baligumya akiendelea na semina juu ya mfumo huo unavyofanya kazi. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Manyama Maagi.
 Menejimenti na Maofisa mbalimbali wa Shirika la Nyumba la Taifa wakijifunza jinsi ya kutumia Mfumo wa GePG katika malipo ya Kodi za Serikali.
 
Comments