Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)
Selemani Jafo akiwa ameshika orodha ya wafanyabiashara wa soko la
Magomeni akisisitiza wapewe kipaumbele baada ya soko kukamilika.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)
Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya Kinondoni.
Wananchi
wa Magomeni wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo(hayupo pichani).
Muonekano wa soko la Kisasa linalojengwa Magomeni
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)
Selemani Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kukamilisha
ndani ya muda ujenzi wa soko Jipya la Kinondoni na kuwapa kipaumbele
wafanyabiashara 693 waliopo hivi sasa.
Jafo
ametaka wafanyabiashara hao wawe wa kwanza kumpatia maeneo ya Biashara
bila kunyanyaswa baada ya ujenzi wa soko hilo jipya la kisasa
kukamilika.Akizungumza
alipotembelea soko hilo leo, Waziri Jafo amesema kuna kasumba
imejengeka ambapo masoko yanapojengwa wale waliokutwa sokoni kabla ya
ujenzi huwa watatupwa nje na badala yake watu wengine wapya wenye fedha
ndio hupatiwa.
"Nataka
hawa wananchi waliopo sasa hapa sokoni ndio wawe watu wa kwanza
kukabidhiwa maeneo ya biashara baada ya ujenzi kukamilika," amesisitiza
Jafo.Waziri
Jafo amemwagia sifa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia kwa kuwa
ndiye aliyewasilisha kilio cha wanafanyabishara wa Magomeni na serikali
imekisikia na kuamua kupeleka fedha.
Pia
amewapongeza viongozi wa wilaya ya Kinondoni kwa mshikamano mkubwa chini
ya Mkuu wa wilaya yao Ally Hapi na kwamba chini ya Mkuu huyo wilaya
hiyo imetulia sana na inasonga mbele na hakuna migogoro ya viongozi inayoweza kurudisha nyuma maendeleo.
Aidha, Waziri Jafo amempongeza pia kwa kuanza utekelezaji wa utoaji wa mikopo kwa Vijana na wanawake bila Riba.Halmashauri
ya wilaya ya Kinondoni imepata Kiasi cha Sh.Bilioni 9 kwa ajili ya
ujenzi wa soko hilo kutoka serikali kuu katika mpango wa utekelezaji wa
miradi ya kimkakati.
Comments