KATIBU MKUU WA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI DOROTHY MWANYIKA AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA KUU NHC
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa kinachofanyika leo jijini Dar es Salaam kinachojadili kwa mapana masuala ya utendaji kazi, maslahi ya wafanyakazi, utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka 10 wa Shirika na kujadili bajeti ya Shirika na utekelezaji wake. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi na Kushoto kwake ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi, Mecktilda Mihayo na Wa kwanza Kushoto ni Naibu Katibu wa Baraza la Wafanyakazi, Adolf Kasegenya.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika akishiriki wimbo wa pamoja wa wafanyakazi maarufu kama "Solidarity Forever"na Viongozi wa Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Felix Manyama Maagi (wa pili kushoto) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, kushoto ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Adolph Kasegenya na kulia ni Katibu wa Baraza, Mecktilda Mihayo wakazi wa kikao cha baraza hilo kinachofanyika kwa siku mbili makao makuu ya
Shirika hilo Kambarage House.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika akisindikizwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Felix Manyama Maagi (katikati) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, kulia ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Adolph Kasegenya baada ya ufunguzi wa kikao cha baraza hilo kinachofanyika kwa siku mbili makao makuu ya Shirika hilo Kambarage House.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika akisindikizwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Felix Manyama Maagi (katikati) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, kulia ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Adolph Kasegenya baada ya ufunguzi wa kikao cha baraza hilo kinachofanyika kwa siku mbili makao makuu ya Shirika hilo Kambarage House.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika akisindikizwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Felix Manyama Maagi (katikati) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, kulia ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Adolph Kasegenya baada ya ufunguzi wa kikao cha baraza hilo kinachofanyika kwa siku mbili makao makuu ya Shirika hilo Kambarage House.
Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika na baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika akisindikizwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Felix Manyama Maagi (katikati) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, baada ya ufunguzi wa kikao cha baraza hilo kinachofanyika kwa siku mbili makao makuu ya Shirika hilo Kambarage House.
HOTUBA YA KATIBU MKUU WIZARA
YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI, DOROTHY MWANYIKA KWENYE UFUNGUZI WA
KIKAO CHA BARAZA KUU LA WAFANYAKAZI LA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC), JIJINI
DAR ES SALAAM TAREHE 14/05/2018.
Ndugu Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Wafanyakazi, Felix Manyama Maagi,
Ndugu
Wakurugenzi wa Shirika,
Ndugu
Wajumbe wa Baraza,
Ndugu Wageni
Waalikwa,
Ndugu
Wanahabari,
Mabibi na
Mabwana.
Nianze kwa kueleza faraja
yangu kwa mapokezi yenu mliyonipa na kuishukuru Menejimenti ya Shirika kwa
kunipa heshima ya kuja kuwafungulia kikao hiki cha Baraza Kuu la Wafanyakazi.
Nawashukuru kwasababu tukio hili la leo linanipa fursa ya kukutana na watendaji
wakuu na wawakilishi wa wafanyakazi kutoka mikoa yote ya Shirika kwa mara ya
kwanza tangu niteuliwe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara yetu. Hivyo, ni fursa kwangu
kuweza kufikisha ujumbe kwa wafanyakazi na umma juu ya Shirika letu.
Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe, kwanza kabisa naomba nitumie fursa hii kuwapa pole wote mliosafiri safari ndefu
ya kuja hapa Dar es Salaam. Tumshukuru Mungu kwa kuwawezesha kufika hapa salama
salimini.
Pili, Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe, nimeelezwa kwamba ajenda
za kikao Baraza hili zimejielekeza katika masuala ya utendaji wa Shirika.
Aidha, nimeelezwa kuwa kikao chenu kitapitia mizania ya hesabu za Shirika kwa
mwaka wa fedha 2018/2019, pamoja na kujadili taarifa za utekelezaji wa kazi
mlizozipanga kuendana na Mpango Mkakati wenu. Naupongeza sana utaratibu huu
maana unaleta mezani utekelezaji wa majukumu ya kazi na kuanisha changamoto
mnazokumbana nazo kwa nia ya kuzipatia ufumbuzi sahihi kwa pamoja.
Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe, Sina haja ya kusisitiza umuhimu wa
ajenda zote hizi zilizoko mbele yenu, kwani naamini wajumbe wote wa Baraza hili
mnatambua umuhimu wake. Hivyo ni matarajio yangu kuwa ajenda hizi, ambazo
zinagusa uhai na maendeleo ya Shirika letu, mtazijadili kwa kina ili hatimaye
muweze kutoka na maazimio ya msingi yatakayoliwezesha Shirika hili kuongeza
tija na kukidhi matarajiyo ya umma wa Watanzania ambayo kwa sasa yako juu sana
kutokana na imani mliyowajengea.
Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe, Baraza hili ni jukwaa muhimu sana
mahala pa kazi kwani ni kiunganishi kati ya Menejimenti na Wafanyakazi. Ni
matumaini yangu kuwa mtaendelea kushirikiana ili kuleta ufanisi kwa Mamlaka na
Taifa kwa ujumla. Hata hivyo ikumbukwe kuwa Serikali inazingatia sana suala la
taasisi zake kuwa na mabaraza ya Wafanyakazi kwani yalianzishwa kisheria kwa
madhumuni ya kuishauri Serikali katika ngazi za idara, taasisi na Wizara kuhusu
usimamizi wa kazi na rasilimali watu, utekelezaji wa majukumu, kulinda haki na
wajibu wa waajiri na wafanyakazi, kutoa ushauri kuhusu kujenga hali bora za
kazi, maslahi ya Wafanyakazi na kusimamia haki na ustawi katika sehemu za kazi.
Wajibu wa mabaraza haya kama vyombo vya ushauri na usimamizi ni kuhakikisha
kuwa waajiri na watumishi wanatambua wajibu na haki zao, pia wanazingatia
maadili ya utumishi wao ili kuleta matokeo ya utendaji wa kazi yenye tija,
staha na upendo.
Kadhalika, niwapongeze kwa
kutengeneza na kisha kuufanyia mapitio Mpango Mkakati wa miaka kumi ambao mkiufanyia
kazi na kuutekeleza kwa wakati mtaleta mabadiliko makubwa katika sekta ya
nyumba hapa nchini. Nimesoma Mpango Mkakati huo kwa makini na kuyapitia malengo
yote sita mliyojiwekea.
Nataka niwaambie kuwa
malengo haya siyo mepesi, ni mazito na yanahitaji uwajibikaji wa hali ya juu
ili kuweza kuyatekeleza kwa ufanisi la sivyo yatabaki kwenye makaratasi. Hivyo,
nitoe rai kwenu kuwa muweke mbele maslahi ya Shirika na ushirikiano mkubwa ili
muyafikie malengo yenu. Wakati nikiwapongeza kwa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa
kutekeleza Mpango Mkakati huu wa miaka kumi (2015/16-2024/25), ni vema mkajua
kuwa Serikali imewapa dhamana kubwa ya kuleta mabadiliko makubwa katika sekta
ya nyumba. Shirika lina changamoto ya kuhakikisha kuwa linakuwa na uwezo wa
kifedha ili kuweza kutekeleza mikakati ya ujenzi wa nyumba hizi hasa nyumba za
gharama nafuu. Niseme tu kuwa Wizara inaungana nanyi katika kuhahakikisha kuwa
yale yote ambayo yanahitaji msukumo wa Wizara yanatekelezwa ili kuweza kufikia
malengo mliyojiwekea kwa wakati.
Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe, Nipende kuwakumbusha kwamba Serikali
ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati, katika ujenzi wa uchumi wa viwanda ili
kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu. Lengo kuu la Mpango huo ni kuiwezesha
Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati inayoongozwa na viwanda ifikapo mwaka
2025. Ni dhahiri, Shirika la Nyumba mtachochea azma hii ya viwanda kwa kuongeza
kasi ya ujenzi wa nyumba na tija katika ujenzi.
Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe, kupitia hotuba yangu, napenda
kuwahamasisha muendeleze ushirikiano na mabenki kutoa elimu ya mikopo ya nyumba
ili kuwawezesha watanzania wengi zaidi kutumia fursa zilizopo za mikopo ya
benki kununua nyumba zinazojengwa na Shirika. Itakuwa fahari kubwa kwa
mwananchi kumiliki majengo ya ofisi, biashara na makazi katikati ya miji na
Halmashauri zetu zinazojengwa na NHC.
Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe, sitaki kuwachosha hata kabla
hamjaanza kazi nzito iliyoko mbele yenu. Hivyo, naomba niishie hapa kwa
kuishukuru tena Menejimenti kwa kunialika kuja kufungua kikao chenu hii leo.
Aidha, naomba nimalizie kwa kuwatakia wajumbe wote safari njema mtakaporejea
majumbani na sehemu zenu za kazi.
Baada ya kusema haya sasa
napenda kutamka kuwa kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi kwa mwaka 2018,
kimefunguliwa rasmi. Asanteni sana kwa kunisikiliza.
Comments