BENKI YA EXIM YA INDIA YAIPATIA SERIKALI YA TANZANIA MKOPO WA MASHARTI NAFUU KUSAIDIA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI KATIKA MIJI 23 YA TANZANIA
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi Amina Kh. Shaaban kwa
pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Exim ya India, Bw. David Resquinha
wakisaini kwa niaba ya Serikali zao Mkataba wa Mkopo wenye masharti
nafuu wa Dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi
ya maji katika miji 23 ya Tanzania.
Bi. Shaaban na Bw. Resquinha wakibadilishana mkataba huo mara baada ya kusaini
Picha ya pamoja
Serikali
ya India kupitia Benki ya Exim imeipatia Serikali ya Tanzania mkopo
wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 500, sawa na shilingi
Trilioni 1.14 za Tanzania, kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji
katika miji 23 ya Tanzania.
Hafla
ya uwekaji saini wa mkataba huo imefanyika leo tarehe 10 Mei, 2018 mjini
New Delhi, India ambapo Bi. Amina Kh. Shaaban, Naibu Katibu Mkuu,
Wizara ya Fedha na Mipango na Bw. David Resquinha, Mkurugenzi Mkuu wa
Benki ya Exim walisaini kwa niaba ya Serikali zao..
Miji
itakayonufaika na Fedha za mkopo huu ni Muheza, Makambako, Kayanga,
Njombe, Manyoni, Songea, Sikonge, Chunya, Kasulu, Kilwa Masoko, Rujewa,
Mugumu, Geita, Makonde, Wangingómbe, Handeni , Singida mjini, Kiomboi,
Mpanda, Chemba, Mafinga, Urambo-Kaliua pamoja na miji ya Zanzibar.
Akizungumza
baada ya kusaini mkataba, Naibu Katibu Mkuu, Bi. Amina Kh. Shaaban,
amesema kuwa miradi hiyo ni muhimu kwa sababu itawezesha upatikanaji wa
huduma ya maji safi na salama katika miji husika hivyo kusaidia
kupunguza magonjwa ya mlipuko yanayotokana na maji yasiyo salama.
Aidha,
miradi itasaidia kufikiwa kwa malengo na mipango ya Taifa na Kimataifa
ya Maendeleo ikiwemo: Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mpango wa Taifa
wa Maendeleo wa Miaka Mitano awamu ya pili (FYDPII) , Mkakati wa Kukuza
na Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA III) na Malengo ya Maendeleo
Endelevu 2030 (SDG’s).
Vilevile,
amesema uamuzi wa Serikali wa kuboresha huduma za maji umelenga
kuwapunguzia Wananchi husususan Wanawake adha ya kutembea umbali mrefu
kutafuta maji, na hivyo kupata muda wa kutosha kufanya shughuli mbali
mbali za maendeleo.
Comments