SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LAKABIDHI NYUMBA ZA MAKAZI 63 ZA IYUMBU SATELLITE CENTER KWA UHAMIAJI

Meneja wa Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa, Itandula Gambalagi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa na Kamishna wa Fedha, Ndugu Peter Chogero kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wakikabidhiana hati ya makabidhiano ya nyumba baada ya kukabidhi nyumba 63 kwa Jeshi la Uhamiaji.
 Picha ya pamoja ya uongozi wa Shirika la Nyumba na Uhamiaji baada ya makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.
 Picha ya pamoja ya uongozi wa Shirika la Nyumba na Uhamiaji baada ya makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.
Wafanyakazi na uongozi wa Jeshi la Uhamiaji wakiwa wameshika mfano wa ufunguo baada ya makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.
Mradi huu ambao ujenzi wake ulianza Desemba 2016 una ukubwa wa ekari 234 na ni moja ya sehemu ya mji uliopangiliwa kitaalamu kwa kuzingatia sheria na kanuni za mipango miji na utajengwa katika awamu tatu. Nyumba hizi 63 ambazo zimeshakamilika na kuanza kukaliwa zinakabidhiwa leo kwa Idara ya Uhamiaji.
Makabidhiano haya yamefanywa na Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa, Ndugu Itandula Gambalagi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC na Kamishna wa Fedha, Ndugu Peter Chogero kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.
Makabidhiano haya yanafanyika baada ya ahadi ya Shirika la Nyumba kwa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ya kujenga nyumba makao makuu ya nchi Dodoma.
Katika uzinduzi wa nyumba hizi, Mkurugenzi Mkuu wa NHC alimhakikishia Mh. Rais kwamba nyumba hizi zimekamilika na ziko tayari kwa kukaliwa.
Leo ni siku ya furaha kuona kwamba NHC inakabidhi nyumba kwa Uhamiaji ambaye ni mmoja wa wanunuzi wakubwa wa nyumba katika mradi huu.
Nyumba hizi ni bora kabisa zimejengwa kwa ustadi mkubwa. Ni wito wetu kwamba nyumba hizi watazitunza ikiwa na mazingira yake.
Mradi huu wa nyumba 300 ikiwa 150 zimekamilika ni kati ya miradi mingi ambayo NHC inatekeleza.

Comments