Friday, January 26, 2018

KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI ATEMBELEA USA RIVER NA SAFARI CITY AFURAHISHWA NA MPANGILIO WA MIRADI HIYO

Katibu Mkuu akipata maelezo ya mradi wa Usa River Satellite City kutoka kwa Meneja wa Mradi, James Kisarika.
 
 Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mama Dorothy Mwanyika, ametembelea Miradi ya Safari City na Usa River Satellite City, iliopo katika Jiji la Arusha na kufurahishwa na mpangilio wa miradi yote miwili. Amehimiza uongozi wa NHC kusimamia miradi hiyo kuhakikisha kwamba matarajio ya wateja katika kuwekeza pesa zao kwa ununuzi wa viwanja na baadaye kujenga nyumba, yanatimia.
 Katibu Mkuu, Mama Dorothy Mwanyika akiongozana na Meneja wa Singida, Ndugu Nistas Mvungi na Meneja wa Arusha, Ndugu Bamanyisa, akipokelewa Safari City na Meneja wa Mradi, Ndugu James Kisarika.
 Katibu Mkuu akiongozwa na Meneja Mradi kuingia katika ofisi ya Mradi.
 Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu na viongozi aliofuatana nao,  kutoka ofisi ya Mkoa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Vitengovya Ardhi na Usajili wa Hati.
 Viongozi wa Shirika Mikoa ya Arusha na Singida pamoja na wa Wizara wakitafakari maswala yahusuyo maendeleo ya mradi wa Safari City.

 Meneja wa Mradi, James Kisarika, akitoa maelezo ya jumla kuhusu maendeleo ya Safari City.
 Katibu Mkuu na viongozi wengine akisikiliza mawasilisho kwa makini.


 Afisa Mipango Miji wa Shirika la Nyumba la Taifa, Devota Zephrine, akielezea mpangilio wa Mji wa Safari City.
                 
Katibu Mkuu akikagua nyumba za mfano.
Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Loreen Uronu, akielezea maendeleo ya mauzo ya viwanja Safari City.
 Viongozi wakiikiliza mawasilisho kwa makini.
 Mwanasheria wa Mradi, Neema Mapunda, akiwasilisha mada kuhusu utaratibu wa kusimamia usagi na ulinzi katika Mji wa Safari City ikiwa ni pamoja na kuanzisha umoja wa Wamiliki nyumba.
 Katibu Mkuu akitoa nasaha zake baada ya mawasilisho ya mradi. Alikiri kufurahishwa na mpangilio wa mradi na kuahidi kwamba Wizara ipo pamoja na Shirika katika uendelezaji huu na kwamba wadau kama TARURA washirikishwe pia katika ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami na kushirikisha watumiaji kwa njia ya "road tolls charges".
 Katibu Mkuu awasili Usa River Satellite City.


 Katibu Mkuu afurahia maelezo kuhusu mkakati wa uendelezaji mradi wa Usa River. Akiri uwekezaji wa Shirika katika mradi huo ni mzuri. Mradi unao miundo mbinu yote muhimu kama maji na umeme tayari na uko karibu kabisa na barabara kuu ya Arusha Kuelekea KIA na Moshi.
 Katibu Mkuu akizungumza na viongozi wote baada ya maelezo ya mradi.
 Katibu Mkuu akipata maelezo kuhusu hatua za uendelezaji wa mradi wa Usa River.
 Viongozi wa Shirika Mkoa na wa Wizara Kanda ya Kaskazini, wakifurahia mafanikio ya ziara ya Katibu Mkuu wa wizara ya Ardhi. Viongozi hao ni pamoja na Mameneja wa Arusha na Singida na  Kamishina Msaidizi wa Ardhi.
Picha ya pamoja. Mpango  wa uendelezaji mji wa Usa River utabakiza asilimia 95% ya miti yote ilopo kwa sada ili kuhakikisha mji unabakia kijani na wenye mandhari ya kipekee kabisa. Tunasema karibu tena Katibu Mkuu.
Post a Comment