
Mpango huu wa utoaji wa chakula unathibitisha ukweli ulio wazi lakini mara nyingi hupuuzwa: haki ya elimu haiwezi kutenganishwa na haki ya lishe. Pale ambapo serikali au jamii hazioni chakula shuleni kama sehemu ya sera ya elimu, tunakuwa tumewatupa watoto wengi pembezoni mwa ndoto zao.
Mwamalili ni kielelezo cha kile kinachowezekana tukiamua kama taifa kwamba hakuna mtoto atakayekosa elimu kwa sababu ana njaa. (Picha na Yahya Charahani)Toa maoni yako.
5 comments:
Mzee wa mshitu tupe taarifa zaidi kuhusu elimu ya hapo huko nyuma na sasa imeongezeka vipi na tazama na sababu zingine hasa makazi ya vijiji hivyo na watu wake isiwe shule inatumika kama sehemu ya kukimbia njaa hali inayoweza kuwafanya watoto hao kutokusoma kwa umakini na badala yake kuwaza muda wa maakuli tu.
Yaani ina maana hawa Oxfam wameshindwa kabisa kutengeneza japo ka-karo ili watoto wagawiwe chakula kwenye mazingira bora zaidi?Hapo nje vumbi vipi?Au ni kwanini wazazi wasijitolee nguvu wakajenga wao karo?nikisema karo namaanisha sink.
Jamani wana-shinyanga tumezidi bado tuko nyuma mno!! Vipi Charahani mwenzangu wewe ni Mwanza au Shinyanga?..hebu tufanyeni jamani tuuokoe mkoa wetu.
Makene umesema kweli kabisa watoto wa huku wamegeuza shule sehemu ya kukimbia njaa wazazi nasikia mitaa ya huko wanawalazimisha watoto kwenda shule wakijua watapata msosi kwa maana hiyo kiwango cha elimu bado kitaendelea kuwa cha chini hata wakifanya hivi sababu taarifa nilizo nazo kata nzima kilipo kijiji hicho ina shule moja tu ya sekondari.
Jeff unadhani kama wameshindwa kuandaa mazingira mazuri mpaka mfadhili akaja wataweza kweli kujenga karo, kwanza hiyo shule ina walimu tisa tu kwa madarasa yote.
Mija afadhali Shinyanga ipo mikoa hapa nchini hata shule za namna hii ni dili, mimi nimewahi kuishi Shinyanga lakini si mtu wa huko tunapaswa tupiganie maisha ya hawa vijana wetu kwani hali ni chafu.
NJAA HII HAISAHAULIKI!
Mh! Hii njaa ilikuwa kali sana, ilikuwa bila kugawa chakula kwa wanafunzi basi hakuna mahudhurio mazuri. Hali ilikuwa mbaya sana katika Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga. Tuombe Mungu baa hili lisirudie.
Karibuni kwangu 'http://jadili.blogspot.com'
Post a Comment