Monday, May 08, 2006

Zuma amepakwa mafuta!!!!

Ile kadhia ya kubaka iliyodumu muda wa miezi kadhaa iliyomkumba Makamu wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ambaye ni mtu muhimu anayeangaliwa na baadhi ya Waafrika Kusini kama mrithi wa Thabo Mbeki ya imemalizika baada ya Jaji Willem van der Merwe kutoa maamuzi kuwa yule mwanamama aliyedai kubakwa na Zuma alifanya vile kwa ridhaa yake. Lakini bado kuna suala la rushwa na mengineyo. Vijana wa ANC wengi wao mategemeo yao ni yeye hebu bonya hapa Mashtaka ya ubakaji yaliyokuwa yakimsibu Bwana Zuma,yaliweka ufa mkubwa ndani ya chama tawala cha ANC,ambapo kiongozi huyo alionekana kupewa nafasi kubwa ya kuwa Urais mara Rais wa sasa Thabo Mbeki atakapong’atuka.
Jaji Merwe,akisoma hukumu iliyokuwa ikitangazwa na kuoneshwa moja kwa moja katika radio na televisheni, alieleza kwamba Bwana Zuma pamoja na mwanamke aliyekuwa mlalamikaji,walikubaliana kwa hiyari yao kufanya mapenzi nyumbani kwa Zuma mwezi wa Novemba mwaka jana.
Wanaharakati wa mapambano dhidi ya ukimwi walikuwa wanatokwa na machozi baada ya kutolewa hukumu hiyo.
Wakati kesi hiyo ikiendela wanaharakati hao,walimshutumu Zuma kwa kutoa ushahidi kwamba hakutumia kondom wakati alipozini na mwanamke aliyekuwa amemshtaki,huku Zuma akifahamu kuwa mwanamke huyo alikuwa mwathirika wa ukimwi.

5 comments:

mwandani said...

Kashinda, lakini elimu yake juu ya ukimwi inanipa utata. Ati alidai baada ya ngono na dada yule mwenye virusi alitawadha na maji ili asiambukizwe virusi.

baada ya yote kashfa zilizomuandama huyu mzulu nadhani zimempaka madoa sana hata akitaka kugombea urais baadaye.

mzee wa mshitu said...

Hili umesema kweli ndugu yangu hivi kwa akili ya kawaida ya kuweza kuchambua mambo na kukaa mavikao yote yale ya kutaka amani ya Burundi na mengine mengi kumbea anatawadha baada ya kutoka kufanya ngono bila kondomu ili eti asiamukizwe??? Itabidi atumie nguvu nyingi sana sijui!

John Mwaipopo said...

Zuma ni miongoni mwa charismatic leaders. Na kama mtu mwingine yeyeto hasa Afrika suala la kufanya mapenzi nje ya ndoa sio tatizo sana. Wengi hatuna elimu tosha kama Zuma isipokuwa yeye tunamnyooshea vidole sana kwa sababu ni kiongozi. Wale viongozi wetu ambao tunaogopa kuwasema kwa sababu ya kuogopa mkong'oto, ambao wanavizia vibinti pale mabibo hostel ama kuwatanguliza mahotelini kufanya uanahizaya huu vipi.

Patamu hapo hata kiongozi kondomu haina raha kwake. Makubwa haya. Basi tuombe tu kuwa alitoka 'salama' baada ya kutawaza nanihii. Halafu vipi tumshauri kuhusu kupima maana asije kuwa anaringa kwani amepima?


Upande wa siasa atashindwa tu kwa sababu nyingine ikiwemo hiyo ya kubwia mlungula. Hata akibainika mwema tayari kuna doa. Lakini akishinda kikwazo hiki, cha ngono (zembe) sio kikwazo inapokuja Afrika. Mifano tunayo Tanzania. Viongozi wa Afrika wakihusishwa na ngono ndio sifa kuu. Au hamjui kuwa hata Bongo yanatokea haya. Naogopa mkong'oto mie.

Alamsik Binuur

Mija Shija Sayi said...

Sasa nimegundua kwamba kuna viwango na viwango vya ashki katika miili ya binadamu. Kiwango cha ndugu yetu Zuma nadhani kiko juu kunaweza kushikilia tano bora duniani! Kaka yangu Charahani hata wewe hapa nisaidie kweli mtu unaweza kupagawa kiasi ukashindwa hata kufanya maamuzi ya wapi na wapi uingie?

mzee wa mshitu said...

Mwaipopo afadhali hata yeye huyo Zuma angekuwa salama, lakini sijui , haiwezekani kwa akili ya kawaida mtu unayejua ana ngoma na we ukachomeka hapo hapo. Hapa kuna mashaka ndugu yangu.
Juu ya hawa wanaovizia vibinti aisee hiyo ni noma kabisa na ni wachache mno ambao hawana tabia hiyo ingelikuwa wote wanabainika kama Zuma basi nusu ya wakulu wetu wangekuwa na kesi.
Dada Mija umenichekesha hiki kiwango cha Zuma cha ashki ni balaa kinatisha yaani inawezekana huyu zikimpanda anaweza kuparamia hata mti!