Friday, April 07, 2006

Mzee wa fikra pevu atinga mtandaoni

Haya tena kumekucha nawaleteeni mwanablogu mwingine ambaye anatoka katika hiki kijiji chetu cha Mwananchi kama anavyopenda kutuita bwana Mwaipopo. Si mwingine bali ni Absalom Kibanda, ambaye nadhani wengi mnamfahamu. Yeye si mgeni sana katika anga hizi, lakini ameamua kuibuka tena.

Kwa wasiomfahamu huyu ni mtu mmoja makini katika uchambuzi wa masuala ya kisiasa, kijamii na kitaaluma. Pamoja na hayo yote pia ni mwanamichezo matata sana kwa hiyo pia masuala ya michezo hayamsumbui hata kidogo. Makene, Ndesanjo, Reginald, Mpoki na wengineo wengi wanamfahamu hivyo namleta kwenu.

Anuani yake ni absalomkibanda.blogspot.com. Mtaniwia radhi masuala ya kublogu bado yananipiga chenga sijaweza kulink moja kwa moja hivyo welcome

10 comments:

boniphace said...

Kumekucha Mwananchi, huyu inabidi kuwa makini sana maana makala zake nazifahamu, zitakuwa kali kama mwale sii ule wa mARK mSAKI bali zilijaza hoja makini. Karibu Kidanda.

Mzee wa Mshitu andika anuani yake ya blogu kwenye maoni kisha tutamtangaza na sisi

mzee wa mshitu said...

Makene anuani yake ni absalomkibanda.blogspot.com nadhani nimeiandika kama sikosei. Halafu hebu nifundishe namna ya kuweka picha yangu katika kiboksi kama ya kwako ili nami nipate kuonekana nimejaribu mara kadhaa nashindwa si unajua ugeni wa blogu.

John Mwaipopo said...

Charahani naona sasa umekuwa balozi mzuri wa Makene. Kazi unayofanya hapa mwanachi ya kila kukicha kutuchomolea mwanablogu mpya inatukuka. tunafurahi sana tunapopata sehemu ya kusemea maneno mbadala, yale ambayo nyinyi wahariri huwa mnayaweka kapuni.

Hata hivyo kibanda karibu sana tena sana kabisa. Nimekukosa siku nyingi kiasi sasa si hapa kiu yangu (sio ya Castle) inakatika huku naiona hivi-hivi (Kipembe-pembe, kama mnafuatilia luninga za bongo)

Sasa nina pendekezo. Muunde katimu hivi ka soka au kikapu. Ka soka katapendeza zaidi. Jina msiwe na wasiwasi. Vipi kuhusu " Mwananchi Communications Bloggers United" (kautani hivi).

Golini Makene, Mpoki Bukuku (2)Charahani (3), Miruko (4), Kibanda (5), Mwavizo (6), Abdi Sultani(7) (Huyu mwambieni afungue ya kwake kwani nimekosa stori za ulabuni), Ndesanjo (8), Freddy macha(9). Wengine Makene jazia

John Mwaipopo said...

Charahani jaribu kuangalia hapo
http://help.blogger.com/bin/answer.py?answer=776.

Kisha soma taratibu utaelewa tu kupandisha picha yako. Unatakiwa uwe nayo tayari kama kwenye desktop hivi (iwe ya ukubwa wa wastani hivi). Anza kama unataka ui-upload kama posting ya kawaida. Ukisha i-upload utakwenda kubadilisha HTML. Huko utaikuta URL ya picha ambayo utaicopy kama walivyonyesha kwenye mfano wao na kuipaste utakaporudi kwenye ‘edit profile’ (Baada ya kucopy URL utaghairi kuuplolad picha na kurejea edit my profile).

Lakini utaelewa mwenyewe utakapofata kiunganishi hapo juu. Inakuwa ngumu kuielwa mwanzoni lakini ni "rahithi thana”

mzee wa mshitu said...

Mwaipopo

Hiyo baabkubwa na sasa tukishamaliza hii tutawaleta kwenu wanablogu kina mama itakuwa BAMBOOCHA (usichangae haka ni kamsemo kameanzishwa na fanta orange katika promosheni zao kakiwa na maana babu kubwa).

Aisee nitafuatilia huu muongozo wa kuweka picha nikifanikiwa nitafurahi sana sababu hiki kitu ni mojawapo ya vinavyoninyima usingizi.

Reggy's said...

Charahani ongera kwa kazi kubwa ya kutuletea mbuyu. mambo sasa yameiva alamsiki

mzee wa mshitu said...

Mwaipopo ahsante sana kwa msaada wako hatimaye nimeweza kuingiza picha yangu mtandaoni hakika ilikuwa shghuli pevu na sasa nasonga mbele. Huraaa

John Mwaipopo said...

Nimeona. Sasa walau tukikutana Dar ama Mbeya tutaweza kutambuana kama Mark Msaki alivyomtambua Miruko kule Dodoma.

mzee wa mshitu said...

Reginald
huu mbuyu (Kibanda) niliouleta hakuna shaka utatujaza yaliyo weledi, hongera kwa kupitisha azimio la Dodoma hakika mmefanya kazi inayoonekana, huraaaah!

Mwaipopo

Ni kweli ndugu yangu sasa tunasonga mbele twaweza fahamiana kwa kuonana tu barabarani sasa maana mambo ya kuwa kama akina anonimous hayapendezi bwana!

Ndesanjo Macha said...

Ndio Charahani, Mwananchi pale mambo yanawaka moto. Inafurahisha kuona kuwa hawataki kusubiri mapinduzi haya yawapite. Mbele kwa mbele....
Naona umeuliza jinsi ya kuweka kiungo ndani ya habari, kama pale ulivyotaja anuani ya blogu ya ndugu yetu Kibanda. Soma maelezo mafupi ya kufanya hivyo kwenye anuani hii:
http://tinyurl.com/jnf9q