Huu ni ustawi au ubeberu wa kiutamaduni?

KAMA kijana naweza kujiita wa makamu hivi sasa, niliyekulia katika mazingira ya utanzania halisi yale ya kutaabika, kuhangaika, kuvuja jasho na kupatikana na kila aina ya madhila.

Mazingira yaliyojikita katika utamaduni wa kushangaza kidogo ambayo kila kitu, kuanzia watu hadi wanyama kuheshimu wakubwa.

Kwetu sisi 'shikamoo' au salamu ya kawaida basi inaweza ikatawanyika kuanzia na kusalimia hadi mifugo, wajomba, shangazi mababu na hata kukumbushana mambo ya miaka iliyopita.

Salamu hizi mara nyingi huendana na kushikana mikono na hata wakati mwingine kukumbatiana.

Hapa jijini Dar es Salaam ni jambo la kawaida kabisa watu kupishana bila hata kusemezana hata neno moja na kisha kudai au kudhani wamesalimiana.

Na inapokuja kwa watoto ndiyo mbaya zaidi sababu wengi hawana hata habari hata kama wakubwa wanapita, wawapo kwenye daladala wanataka wao ndiyo wapishwe na anayethubutu kuwagusa huibuka na maneno ya kila aina huku wakisaidiwa na 'wanaharakati wa haki za watoto.

Bila shaka wazee waliopoteza uhai wao miaka ya mwanzoni mwa 1970 wangefufuka leo hii wangelipata taabu kubwa kuweza kumeza mabadiliko ya tamaduni zilivyo sasa.

Yawezekana kabisa hii inatokana na ujio wa wakoloni waliokuja kwa staili tofauti lakini wa karibu zaidi wakiwa ni Wamisionari na wakoloni makatili ambao siyo tu walitawala kisiasa kwa kutumia mabavu Afrika bali pia kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

Nakumbuka nyakati hizo wakubwa au waliozishuhudia sherehe nyingi za Krismasi duniani, mkubwa aliposhikwa mkono na mdogo basi alibakia akitarajia kusalimiwa.

Na hii ilijionyesha hata kwa wadogo kiumri kwa wenzao wadogo zaidi yao.

Namna ya kusalimiana ilikuwa imejijenga kabisa kisaikolojia sababu mtu akishajihisi kuwa mdogo kuliko mwingine basi moja kwa moja atatoa salamu ya 'shikamoo' na mkubwa atajibu 'marahaba'.

Au kwa wengine 'Assalam Alleykum' na mwingine hujibu 'Wa alleykum salam'. Zikimaanisha amani iwe juu yako na mwingine akijibu iwe pia juu yako.

Tangu tamaduni za magharibi zianze kuingia nchini kwa fujo kupitia njia kuu za televisheni, intaneti, utandawazi na vinginevyo kama hivyo mambo yamebadilika, lakini baadhi yamebakia kuwa yale yale. Silaumu na wala sipingi.

Hebu fikiria kuporomoka kwa maadili kunavyoingia kwa kasi mtoto hamjui baba. Hii ina maana wapo wanaojamiiana na wazazi wao hivyo hivyo kwa wazazi wa kike!

Sisemi hivi sababu ni dikteta au nina wivu sana, lakini nakumbuka enzi hizo masuala haya hatukupata kuyasikia sana kwa wingi, labda sababu hakukuwa na mawasiliano ya vyombo vya habari.

Siku hizi umeingia utamaduni wa kujenga mahusiano ya jinsia moja yaani madume kwa madume na wanawake kwa wanawake. Na hii inasambaa kwa kasi isiyokuwa ya kawaida!

Hali hii inatishia ndoa zinakuwa siyo kitu cha kukimbilia. Zinakuwa kama fasheni au aina fulani ya hovyo ya mahusiano. Vijana sasa wanataka mahusiano ya kimikataba.

Unapofiwa Dar ni kama wapi sijui. Makamera ya Video, sare kibao, gharama kibao, miziki tena ile ya blast na mengine kedekede.

Sitozungumzia mavazi sababu huo ni mjadala mzito nimeamua nigusie tu haya mawili matatu yanayoitikisa 'brain' yangu.

Tunapoiga tamaduni za kigeni ni muhimu tukawa wachaguzi na wenye welewa mpana ili kuepuka kuwa watu wa kuokota okota hovyo hata visivyofaa.

Comments

boniphace said…
Hizo ndoa kaka kuna watu wanapinga kabisa kutaka kusikia kuwa kuna ushoga Afrika. Lakini tutafika hadi lini, ni kweli kuwa ushoga unatokana na hali ya maumbile au ni tabia ya watu kutaka mali kwa kujiuza? Kuficha mambo kunanikera maana kuna kwamisha kupatikana tiba maridhawa ya jambo kabla ya madhara hayajatamalaki.
Jeff Msangi said…
Charahani,
Kinachonisikitisha mimi ni kwamba wakati sisi tunayaachia maadili na tamaduni zetu wenzetu hawa wa magharibi,hususani hapa Canada wanatuomba watu kama mimi tuwafundishe kwamba tuliwezaje.Wamegundua kwamba walipo sipo na hawatofika wanakotaka kwenda.Unauonaje huu mkorogo wa kijamii?
Vempin Media Tanzania said…
Makene

Hilo unalosema ni kweli huku kwetu hali ya usiri imepita kikomo na ndiyo maana tunayayuka taratibu, tunakokwenda siko tutafikia mahala tutaharibikiwa halafu sijui ndiyo wataunda tume ya kuchunguza chanzo au vipi.

Usiri bwana ni noma sana ndiyo maana hawa wenzetu pamoja na kuwa na mabaya yao lakini hili la kuweka wazi linawasaidia kidogo. Siyo sana.

Jeff, wewe una experience na haya mambo si unaona bwana utumbo tunaouendekeza afadhali umetoa mfano wa huko Canada. Hapa kila kinachokuja kinamezwa kizima kizima

Popular posts from this blog

JESHI LA MAGEREZA NCHINI WAJADILIANA NA NHC NAMNA YA KUENDELEZA MAKAZI MAKAO MAKUU DODOMA

Baraza Jipya la Mawaziri