Friday, December 28, 2012

Waziri Dk. Fenella Mukangara Amtembelea RC Kanali Mstaafu Fabian Massawe


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kulia) akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera  Kanali Mstaafu Fabian Massawe mara baada ya kumtembelea ofisini kwake jana mjini Bukoba. Waziri Dk. Mukangara yupo mkoani humo kwa ajili ya kuangalia jinsi  fedha za mkopo kutoka mfuko wa vijana  zilivyoweza kuwasaidia vijana kujikwamua kimaisha.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kushoto) akimsikiliza  Mkuu wa Mkoa wa Kagera  Kanali Mstaafu Fabian Massawe alipomtembelea ofisini kwake jana mjini Bukoba. Waziri Dk. Mukangara yupo mkoani humo kwa ajili ya kuangalia jinsi  fedha za mkopo kutoka mfuko wa vijana  zilivyoweza kuwasaidia vijana kujikwamua kimaisha.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kushoto ) akiongea na viongozi wa mkoa wa Kagera (hawapo pichani)jana  mjini Bukoba jinsi  Serikali inavyoangalia uwezekano wa kuongea mkopo kwa SACCOS zinazolenga shughuli za maendeleo ya vijana  kutoka shilingi milioni tano hadi kumi kutokana na mahitaji ya fedha hizo kuwa makubwa. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi.
Baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kagera wakimsikiliza  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (hayupo pichani) wakati akiongea nao kuhusu umuhimu wa kuwafuatilia vijana kwa ukaribu katika Kata na kuweza kuwafundisha na kuwashirikisha  katika miradi ya maendeleo,Picha na Anna Nkinda – Maelezo

Thursday, December 27, 2012

TAARIFA KUTOKA JWTZ KUHUSU MTU ALIYEJITAMBULISHA KUWA ASKARI JESHI KATIKA MKUTANO WA CHADEMA SIMANJIRO MKOANI MANYARA

 
Mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kambi ya Monduli, Arusha akiwa na wabunge wa Chadema, Godbless Lema na Joshua Nassari baada ya kumaliza mkutano wa hadhara katika mji mdogo Mererani, Simanjiro mkoani Manyara.---

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeshitushwa na kusikitishwa kuona taarifa ya mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa JWTZ wa Kambi ya Monduli, Arusha, iliyochapishwa katika gazeti la Mwananchi la Desemba 24, 2012 akiwa amevaa sare za JWTZ.
Baada ya kuona habari hii JWTZ linafanya uchunguzi wa kina ili kutambua kama mtu huyo ni askari wa kweli au la. Kimsingi, JWTZ linafanya uchunguzi wa kumtambua mtu huyo kama kweli ni askari wake kwa sababu zifuatazo; kwanza Jina la mtu huyo halijaandikwa, pili kikosi halisi cha mtu huyo hakijaandikwa kwani eneo la Monduli lina vikosi vingi na hakuna kikosi kiitwacho Monduli.
Lakini pia inatia shaka kuwa mavazi yale siyo yale yanayotumika kwa wanajeshi wa JWTZ hivi sasa, kuna tofauti kati ya jampa (jacket) na suruali kama ilivyooneshwa katika picha hiyo.
Aidha, jampa la sare hiyo pia lina tofauti katika sehemu za mikono, jambo ambalo linatia shaka kama ni sare halisi ya JWTZ. Ilikuwa rahisi kumtambua mtu huyo kwa kuangalia uso, lakini mtu huyo anayedaiwa kuwa ni askari alifunika paji la uso ili asitambulike.
Pamoja na hali hiyo ilivyojitokeza, JWTZ linashughulika kumtambua mtu huyo kwa kutumia mbinu mbalimbali. JWTZ litakapobaini ukweli huo, hatua za kinidhamu zitachukuliwa kutokana na Kanuni za Majeshi ya Ulinzi kwani, Sheria nambari nne (4) ya mabadiliko ya nane (8) katika Katiba ya Nchi ya mwaka 1992 ibara ya 147(3), mwanajeshi yeyote hatakiwi kujihusisha katika masuala ya kisiasa.
Kama ilivyoelezwa hapo juu, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwa kuchapishwa kwa picha hiyo kwani hakuna tija wala faida kwa wananchi wa Tanzania zaidi ya kuwatia hofu kuwa Vyombo vya Ulinzi navyo vinashabikia mambo ya siasa, wakati Katiba ya nchi imekataza jambo hilo.
JWTZ linawaomba wananchi waliangalie jambo hili kwa makini, kwa usalama wa nchi yetu.

 Imetolewana Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
 Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
 SLP 9203,
Simu: 0764 742161

DIAMOND, DIMPOZ WAFANYA KUFURU USIKU WA X-MAS DAR LIVE

 
Watu weweee: Kila mmoja akiwa na shauku ya kumpa mkono Diamond.
 
...Leka dutigite: Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Diamond wakiwapagawisha mashabiki kwa wimbo wa Leka dutigite.
Ommy Dimpoz 'on da stage'!
 
Dimpoz na wasanii wake wakiwasha moto kuwakumbuka wapendwa wao waliotangulia mbele ya haki.
 
...Dimpooo...zzz: Umati ukipiga yowe wakati Ommy Dimpoz akifanya kufuru stejini.
 
...Platnumz hewani: Diamond akiwa amebebwa juu na madansa wake.
 
...Nataka kulewa, zikinipanda nimwage radhi.
...Nataka kulewa, lewa...: Diamond akiimba wimbo wake wa Nataka Kulewa.
 
...Nature ua... Nature ua... Nature ua..: Ndivyo Juma Nature alivyokuwa akienda sambamba kwa staili hiyo na mashabiki.
...Wanaume Halisi wakiendeleza libeneke ndani ya Dar Live.
 
Vannesa Mdee akipelekeshana puta na Dimpoz stejini.
KR Muller akigonga mvinyo ndani ya mask.
 
...Zitto kazini: Siyo siasa tu, hata mistari mi mkali.
Kikosi cha Diamond Platnumz kazini.
 
Dimpoz na Vannesa Mdee wakimwaga nyuki stejini.
Manjonjo ya madansa wa Dimpoz.
 
Diamond akiwachizisha mashabiki.
Madansa wa Dimpoz wakionyesha umahiri wao.
 
...Wakizidi kukonga nyoyo za mashabiki.
 
Zitto Kabwe akicheza kwenye kiti baada ya kunogeshwa na swagga za Dar Live.
 
Platnumz na dansa wake kama 'The Wacko Jacko'.
 
Shughuli pevu ya Diamond na madansa wake.
 
...Waacheni watoto waje kwangu: Ndivyo allivyokuwa akichombeza Diamond wakati akitaka kumchukua mtoto huyu.
Platnumz akiipagawisha meza ya wageni waalikwa.
 
Waalikwa wakionyesha nyuso za tabasamu wakiongozwa na Mwasiti (wa pili kulia) na Prodyuza aliyetengeneza wimbo wa Leka dutigite, Tudi (wa tatu kushoto).
 
Prodyuza na Mwanamuziki mkongwe, Ally Mohammed 'Baucha' akikamua stejini.
 
...Nimpende naniii... Nimpende...: Wapambe "Wemaaaaaaaaaaaaa!"
 
Madansa wa Extra Bongo wakinogesha zaidi burudani za X-Mas ndani ya Dar Live.
 
Mpiga gitaa la besi wa Extra Bongo, Hosea Mgoachi akijiachia na shabiki jukwaani.
 
Pozi la Platnumz.
---
Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' na Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' usiku wa kuamkia leo wameweka historia kwa kufanya shoo ya aina yake ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam. Wasanii hao walisindikizwa na mkali Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi, Msanii mkongwe Ally Baucha pamoja na Bendi ya Extra Bongo. Shoo hii imeletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Serengeti Premium Lager na Vodacom - Wajanja wa Kujirusha.PICHA ZOTE : RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY / GPL

Monday, December 24, 2012

MEYA JERRY SILAA ASHIRIKI KATIKA KAMPENI YA USAFI KATIKA KATA YA GONGO LA MBOTO


Pichani Juu na Chini ni Mstahiki Meya wa Ilala na Diwani wa Kata ya Gongo la mboto, Jerry Silaa akiwa na baadhi ya wakazi wa Kata hiyo wakifanya kazi ya usafi katika eneo la Stendi ya Mabasi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhimiza usafi na kuhifadhi mazingira katika jiji la Dar es Salaam iliyozinduliwa na makamu wa Rais mwanzoni mwa mwezi huu.


Mstahiki Meya wa Ilala na Diwani wa Kata ya Gongo la mboto,Jerry Silaa akizungumza na baadhi ya wakazi wa Kata hiyo wakati wa kufanya usafi katika eneo la Stendi ya Mabasi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhimiza usafi na kuhifadhi mazingira katika jiji la Dar es Salaam iliyozinduliwa na makamu wa Rais mwanzoni mwa mwezi huu.

Friday, December 21, 2012

Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) Yazindua kinywaji kipya kinachoitwa ZANZI

 
 "...hiki ndicho kinywaji kipya tulichokizindua leo..."
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL),David Mgwassa akisungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kinywaji kipya kinachoitwa ZANZI (kinachoonekana pichani) iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam leo.
  Meneja Masoko wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL),Joseph Chibehe akitoa ufafanuzi wa Kinywaji hicho kipya aina ya ZANZI ambacho kinapatikana katika ujazo wa 750ml na katika Pakiti zenye ujazo wa 100ml ambacho kitakuwa kikipatikana nchi nzima.Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya TDL,David Mgwassa na kulia ni Meneja Usafirishaji wa TDL,Bavon Ndumbati.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL),David Mgwassa (katikati),Meneja Masoko wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL),Joseph Chibehe na Meneja Usafirishaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL),Bavon Ndumbati wote kwa pamoja wakigonganisha glass kuashiria uzinduzi rasmi wa kinywaji hicho uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam.

Waziri Terezya Huvisa Azungumza na Waandishi wa Habari juu ya Vibali Vya Mazingira


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akiwaonyesha cheti cha Ukaguzi wa Mazingira ambacho hupatiwa Wamiliki wa Mahoteli na viwanda. Waziri Huvisa alikuwa akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini Kwake Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Cherles Kikwanga akitoa Ufafanuzi wa jambo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt.Terezya Huvisa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akitoa Ufafanuzi wa Vibali vya Mazingira kwa Mwandishi wa Gazeti la Jambo Leo Bw. Peter Ambilikile wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari leo Ofisini kwa Waziri Mtaa wa Luthuli Mijni Dar es Salaam.Picha na Ali Meja-Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira

Wasanii Wakongwe wa Muziki wa Dansi Wamtembelea Rais Jakaya Kikwete na Kumshukuru kwa kuwajali


Rais Jakaya kikwete akijadiliana jambo na Mwanamuziki Mkongwe kutoka Bendi ya Kilimanjaro Band Wana Njenje Bw Waziri Ally Muda mfupi baada ya ujumbe wa wasanii wakongwe wa muziki wa dansi pamoja na filamu kumtembelea  Ikulu jijini Dar es salaaam leo
 Mr Waziri Ally kutoka bendi ya kilimanjaro Band wana  Njenje akitoa salaam za shukrani na pongezi kwa niamba ya  ujumbe wa wasanii wakongwe wa muziki wa dansi pamoja na filamu uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaaam leo
Rais jakaya kikwete akimshukuru Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Dansi nchini King Kiki
 Picha juu Rais jakaya kikwete akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa wasanii wakongwe wa muziki wa dansi pamoja na filamu uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaaam leo
--
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo Desemba 21, 2012 amepokea ujumbe wa wasanii wakongwe wa muziki wa dansi pamoja na filamu uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaaam kwa kuwajali wasanii wa aina zote na hata kuamua kutoa tuzo kwa wasanii
ambapo mwaka huu amewatunuku Muhidin Maalim Gurumo na Hayati Marijani Rajabu.Picha na IKULU

WANAFUNZI 23 WA TANZANIA WATIKISA MISRI KWA NIDHAMU, WAZIRI MBARAWA AFARIJIKA

ALEXANDRIA, MISRI -Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa, amesema amefarijika na kujivunia heshima kubwa inayoletwa na wanafunzi 23 ...