Sunday, December 26, 2010

Rais Kikwete amteua Jaji Mkuu mpya


TAARIFA YA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Jaji Mohamed Chande Othman kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, kuanzia tarehe 28 DIsemba, 2010.

Jaji Othman anachukua nafasi ya Jaji Augustino Ramadhani anayestaafu kwa mujibu wa sheria tarehe 27 DIsemba, 2010.
Kwa sasa Jaji Othman ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa na pia ni mtaalamu binafsi juu ya hali ya Haki za Binadamu huko Kusini mwa Sudan, hadi mwezi Agosti 2011.

Jaji Othman alizaliwa tarehe 1 Januari, 1952, ana shahada ya kwanza ya Sheria (LLB) ya Chuo Kikuu cha Dar-Es-Salaam na Shahada ya Uzamili (MA) kutoka katika Chuo Kikuu cha Webster, Geneva-Uswisi.

Amewahi kuwa Makamu wa Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Rwanda huko Arusha na amewahi kushika nafasi sawa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali huko Timor Mashariki.

Jaji Othman pia, amewahi kufanya kazi ndani na nje ya nchi katika Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa kama vile Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) na Shirika la Msalaba Mwekundu.

Jaji Othman ataapishwa kesho tarehe 27 Disemba, 2010 katika viwanja vya Ikulu saa 4:00 asubuhi.

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi
Ikulu
Dar es Salaam
26 Disemba, 2010

Makazi mapya ya Spika Makinda

Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akisikiliza maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa makazi ya Spika kutoka kwa Maafisa wa Bunge pamoja na wakandarasi kutoka Wakala wa Ujenzi (TBA).. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge.

Jengo la Makazi ya Spika linavyoonekana kwa sasa

Thursday, December 23, 2010

Profesa Ndullu akabidhi fedha mpya kwa JK



The Governor of Bank of Tanzania Prof. Benno Ndulu, today presented the new Tanzanian shilling currency note to President Dr. Jakaya Kikwete at Dar es Salaam State House this evening. The New Currency Note will be in circulation from January next year and they will be used alongside with the current bank notes. In the Picture The Central Bank Governor Prof. Ndulu (left) presents a special album with new Tanzanian shilling currency notes to President Dr. Kikwete while the Minister for Finance Mustafa Mkullo,(right) looks on.

Wednesday, December 22, 2010

Michuano ya Netball

Mfungaji wa Morogoro Zuhura Twalibu akimiliki mpira dhidi ya wachezaji wa Mwanza wakati wa mechi ya nusu fainali ya kombe la Taifa la netiboli iliyofanyika viwanja vya shule ya sekondari Filbert Bayi Kibaha mkoani Pwani jana. Picha na Silvan Kiwale

Mfungaji wa Morogoro Zuhura Twalibu akiwa kwenye hekaheka ya kufunga huku akiwa kwenye ulinzi wa wachezaji wa Mwanza. Mfungaji wa Morogoro Zuhura Twalibu (kulia) akifunga goli wakati wa mechi
ya nusu fainali ya kombe la taifa la netball dhidi ya Mwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa Filbert Bayi Kibaha mkoani Pwani jana. Picha zote za Silvan Kiwale.

Tuesday, December 21, 2010

Mary apata shahada ya uzamivu



Mkuu wa United Graduate College and Seminary, Clyde Rivers,(kulia) akimkabidhi Shahada ya Uzamivu ya Masuala ya Jamii katika Kuthamini Utu, Mary Mwanjelwa, (wapili kushoto) kutoka kushoto ni askofu,Dkt,Arthun Kitongo wa Association of Evangelicals in Africa, Joe Mzunda na Prof Nathan Kabara.

Saturday, December 18, 2010

Mariam Mohammed ndiye mshindi Bongo Star Search



Mwanadada Mariam, aliyejipatia umaarufu katika BSS 2010 kwa umahiri wake wa kuimba miondoko ya Taarabu, usiku wa kuamkia leo ametangazwa kuwa mshindi wa shindano hilo liliofanyika katika ukumbi wa Mlinami City jijini Dar es salaam na kushudiwa na Waziri wa habari, Michezo na Vijana, Emmanuel Nchimbi.
Pichani, Mariam akishangilia ushindi wake baada ya kukabidhiwa zawadi yake ambayo ni shilingi za bongo milioni 30 na zawadi nyingini kibao! kwa taarifa zaidi ingia http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/marim-ndiye-mshindi-bss-2010

Monday, December 13, 2010

Kifo hakina huruma kimemchukua Dk Remmy




Mwanamuziki mkongwe na kipenzi cha watu wengi nchini, Ramazani Mtoro Ongala au maarufu kama Dokta Remmy amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Mbezi.

Habari zilizopatikana katika eneo la msiba leo asubuhi zinasema msiba wa mwanamuziki huyo utakuwapo nyumbani kwake Sinza kwa Remmy jijini Dar es Salaam. Taarifa zaidi za mipango za mazishi tutawaleteeni baadaye.

Dk Remmy Ongala ni mmoja wa wanamuziki waliojipatia umaarufu nchini Tanzana tangu miaka ya 1980 kutokana na umahiri wake katika masuala ya muziki.

Ongala, mwanamuziki mwenye asili ya Kikongo, alizaliwa mwaka 1947 Kisangani huko Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo (DRC), wakati huo ikijulikana kama Zaire, na ndiko alikoanza kujihusisha na muziki wa dansi.

Alisema kwamba alianza kuupenda muziki tangu akiwa mtoto kwa sababu ni moja ya fani iliyokuwa damuni, pia anaamini Mungu ndiye aliyempatia kipaji mpaka kufikia kupendwa na wapenzi wengi wa muziki.

Mnamo mwaka 1964 ndio alianza rasmi masuala ya muziki akiwa DRC na bendi ya Grandmike.

Mwaka 1967 alijiunga na kundi lingine lililojulikana kama Sakses Bantu ambalo pia lipo hukohuko DRC.

Ongala alikuja nchini katika miaka ya 1970 na kufanikiwa kuendelea na muziki ambapo alianzisha bendi yake ya Super Matimila na kutoa albamu kadhaa kama "Kilio cha Samaki" na nyinginezo.

Mkongwe huyu anakumbukwa na nyimbo zake zilizotikisa ulimwengu wa muziki wa dansi kama 'Mambo kwa Soksi', 'Kifo Hakina huruma', 'Mambo Mbele kwa mbele' na nyinginezo nyingi zilizomfanya ajipatie umaarufu nchini na nje ya nchi.

MAKATIBU WAKUU WAKAGUA AICC MAANDALIZI YA MWISHO MKUTANO WA IPU, ARUSHA

Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali pamoja na Kamati ya Wataalamu ya Maandalizi ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), wamefan...