Wednesday, November 02, 2016

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY WAJIPANGA KUADHIMISHA JUMANNE YA KUTOA (GIVINGTUESDAY) KWA KUWASAIDIA WATOTO NDANI YA SHULE YA WALEMAVU YA UHURU MCHANGANYIKO



Foundation for civil society ambao ni asasi huru imetangaza kutumia utaratibu wa JUMANNE YA KUTOA (GIVINGTUESDAY) utaratibu ambao unatumika duniani kote kwa ajili ya kuhamasisha watu na jamii kuwa na moyo wa kujitolea kwa ajili ya wahitaji ambapo asasi hiyo imetangaza kuadhimisha siku hiyo hapa nchini kwa kuwasaidia watoto wenye ulemavu wanaosoma katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko ikiwa ni mara ya kwanza kwa Asasi hiyo kuadhimisha siku hiyo muhimu.
Akizungumza na mtandao huu katika mahojiano maalum leo Martha Olotu ambaye ni Busness,Development and Partinaship Manager wa Asasi hiyo amesema kuwa FCS inalenga kutumia Utaratibu wa Jumanne ya Kutoa kwa namna ya kuhamasisha Moyo wa kujitolewa kwa wenye Uhitaji,ikiwa ni Jitihada za ulimwengu ambazo zilizinduliwa Rasmi Tangu mwaka 2012 na shirika la New York’s 92nd streat Y kwa ushirikiano na UN Foundation,Lengo likiwa ni kuweka siku maalum kwa ajili kuheshimu na kuadhimisha ukarimu katika kutoa,ambapo kwa sasa siku hii imekuwa ikiadhimishwa na nchi nyingi Duniani ikihusisha makampuni Binafsi,watu binafsi,familia na asasi za kiraia.



Akizungumzia maadhimisho hayo ambayo yatafanyika Tarehe 29 mwezi wa November Karin Rupia Ambaye Ni Resource Mobilization Executive Kutoka katika asasi hiyo amesema kuwa shirika hilo litakabidhi michango iliyotolewa, na kujiunga kufurahi na watoto kwenye shughuli kama kupima afya za watoto hao,kuchora na watoto,kucheza na watoto kusafisha watoto pamoja na kuwasomea watoto hao wa shule ya msingi Uhuru mchanganyiko.

Kwa maelezo zaidi Juu ya siku hiyo unaweza kutizama HABARI24 TV kwenye Youtube account yetu hapo.

BENKI YA AFRIKA MASHARIKI YAIKOPESHA NHC BILIONI 65 KUENDELEZA UJENZI WA MRADI WA 711 KAWE

01
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (East Africa Development Bank) Bi Vivienne Yeda mara baada ya kusaini mkataba wa mkopo wa Dola za Kimarekani Milioni 30 sawa na shilingi Bilioni 65 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa majengo ya 711 Kawe jijini Dar es salaam, Hafla ya kutiliana saini mkataba huo  imefanyika katika makao makuu ya shirika hilo Upanga jijini Dar es salaam kushoto ni  Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria NHC Bw.Martin Mdoe. (PICHA NA JOHN BUKUKU WA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)1
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (East Africa Development Bank) Bi Vivienne Yeda mara baada ya kusaini mkataba wa mkopo wa Dola za Kimarekani Milioni 30 sawa na shilingi Bilioni 65 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa majengo ya 711 Kawe jijini Dar es salaam, Hafla ya kutiliana saini mkataba huo  imefanyika katika makao makuu ya shirika hilo Upanga jijini Dar es salaam kushoto ni  Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria NHC Bw.Martin Mdoe.
2
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (East Africa Development Bank) Bi Vivienne Yeda wakisaini mkataba wa mkopo wa Dola za Kimarekani Milioni 30 sawa na shilingi Bilioni 65 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa majengo ya 711 Kawe jijini Dar es salaam kushoto ni  Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria NHC Bw.Martin Mdoe.
3
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba na  Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (East Africa Development Bank) wenye  mkopo wa thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 30 sawa na shilingi bilioni 65 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa majengo ya 711 Kawe jijini Dar es salaam, Katikati ni Michael Mwalukasa Mkurugenzi wa Nyumba  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na kushoto ni  Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria NHC Bw.Martin Mdoe.
4
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba na  Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (East Africa Development Bank) wenye  mkopo wa thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 30 sawa na shilingi Bilioni 65 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa majengo ya mradi wa 711 Kawe jijini Dar es salaam, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki East Africa Development Bank Bi. Vivienne Yeda  na kushoto ni Michael Mwalukasa Mkurugenzi wa Nyumba  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
5
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akibadiliana jambo na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki East Africa Development Bank Bi. Vivienne Yeda na Bw. David Shambwe Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara.
8
Maafisa  wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Kutoka kulia ni Tuntufye Mwambusi Meneja Masoko, Chediel Msuya, Hindu Said Afisa Hazina na Richard Ndeona Meneja wa Hazina.
9
Baadhi ya Maofisa kutoka Benki ya East Africa Development Bank (EFDB) wakiwa katika hafla hiyo.
10
Wakurugenzi wa Vitengo Shirika la Nyumba la Taifa NHC wakiwa katika hafla hiyo.

Tuesday, November 01, 2016

WADAU WA HABARI WALIVYOSHIRIKI KUTOA MAONI KUHUSU MUSWADA WA SHERIA ZA HABARI


Jovina Bujulu.

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inatarajia kuwasilisha Bungeni Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari. Muswada huu utatoa mwelekeo na dira ya tasnia ya Habari katika utendaji kazi wake.

Kabla ya kuwasilisha muswada huu Bungeni Serikali ilipokea maoni kutoka kwa wadau wa habari, vyama visivyokuwa vya Kiserikali (NGO’s) na taasisi mbali mbali kuhusu namna na jinsi wanavyotaka muswada wa habari uwe mwongozo wa tasnia ya habari.Miongoni mwa wadau ambao walifikisha maoni Serikalini ni pamoja na Baraza la Habari Tanzania ( MCT), Tanzania Citizens Information Bureau (TCIB), Tanganyika Law Society, Sikika pamoja na Nation Organization for Legal Assistance (NOLA).

Wadau wengine ni Jukwaa la Wahariri (TEF), Kituo cha Haki za Binadamu (LHCR), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Tanzania Human Rights Defenders (THRDs), Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) na Taasisi ya Wanahabari Nchi za Kusini Mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN). 

Baadhi ya mambo yaliyowasilishwa Serikalini na wadau hao mnamo Machi, 31, 2016 ni pamoja na kuimarisha utendaji wa vyombo vya habari nchini, kuendeleza weledi katika taaluma ya habari na kulinda usalama wa wanahabari.

Mapendekezo yao kwa kiasi kikubwa ndiyo yaliyopo katika muswada wa sheria inayopendekezwa ambao umewasilishwa ili ujadiliwe katika kamati ya Bunge na Huduma za Jamii. Kamati hii na wadau inakutana mjini Dodoma kwa sasa.Baadhi ya mambo yaliyomo katika muswada huu ni pamoja na kuunda Bodi ya Ithibati, ambayo itatoa ithibati na vitambulisho kwa wanahabari,kusimamia kanunu za maadili ya wanahabari na kuishauri Serikali katika suala la elimu na mafunzo kwa wanahabari.

Kwa kuangalia baadhi ya maoni yaliyopendekezwa na wadau, na masuala yaliyomo katika muswada huu wa sheria inayopendekezwa, yote yameegemea katika kuipa tasnia hadhi kwa kuzingatia vigezo vya weledi, maadili na elimu kwa wanahabari.Aidha, wadau waliwasilisha kuwa uwepo uhuru wa vyombo vya habari na kwamba wanahabari wawe huru kutafuta, kuchunguza na kuchapisha habari bila kuingiliwa. 

Suala hili lipo katika muswada wa sheria inayopendekezwa na kwamba hakuna mwandishi ayekatazwa kutafuta na kuchapisha habari ila muswada lakini uhuru huo sio kigezo cha kuingilia sheria nyingine.Wadau hao pia walipendekeza sheria ijayo itoe fursa kwa Serikali kuendelea kusajili vyombo vya habari bila kuweka masharti , jambo ambalo lipo pia katika sheria inayopendekezwa kwamba Serikali itaendelea kusajili kwa kuzingatia kanunu, sheria na taratibu zilizopo.

Kuhusu suala la ulinzi na usalama wa waandishi , wadau walipendekeza kuwa wamiliki wa vyombo vya habari wawe na wajibu wa kuzingatia usalama wa wanahabari wanapokuwa kazini ,suala ambalo limo katika muswada wa sheria inayopendekezwa ambapo inamtaka kila mwajiri kuweka Bima na hifadhi ya jamii kwa kila mtu aliyeajiriwa katika chombo cha habari husika.

Kutokana na tasnia ya habari kukosa taasisi inayosimamia wanahabari na vyombo vya habari, muswada wa sheria hii umekuja wakati muafaka kwani endapo itapitishwa itakuwa mkombozi wa wanahabari na tasnia yenyewe. Aidha sheria hii itawapa wanahabari mwelekeo wa kazi na kujua ni mahali gani wanakosea na jinsi ya kujisahihisha. Hii ni kutokana na kuwepo kwa Baraza Huru la Habari ambalo litaandaa na kuidhinisha kanuni za maadili ya wanahabari.

Kwa wadau wa habari, ambao kwa muda mrefu wamekuwa na kiu ya kupata chombo ambacho kitaelekeza na kuongoza tasnia hii, huu ni wakati muafaka kwao kuiunga mkono muswada wa sheria hii ili upitishwe kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.Tumeona manufaa mengi ya elimu na weledi kwa wanahabari,kwa kuwepo kwa mfuko wa mafunzo ya habari, usalama wao kwa kuwataka waajiri wao kuwawekea bima. Kwa kupitisha sheria hii wanahabari watatekeleza wajibu wao kwa weledi na ufanisi zaidi.

Mkutano wa 5 wa Bunge la 11 Waanza Leo Mjini Dodoma

bunge-tzDODOMA: Mkutano wa tano wa Bunge la 11 umeanza leo mjini Dodoma, Novemba mosi ambapo pamoja na mambo mengine wabunge watajadili miswada miwili ikiwemo mswada wa sheria za huduma ya habari wa mwaka 2016.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai ameeleza kuwa mswada mwingine utakaojadiliwa ni mswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali pamoja na wabunge kutoa ushauri kwa serikali kuhusu vyanzo vya mapato na vipaumbele vya bajeti ya mwaka 2017/18 ambayo itajadiliwa siku tatu mfululizo.
ndugaiSpika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai.
Mh. Ndugai amesema katika mkutano wa tano wabunge pia wataishauri serikali kuhusiana na mkataba wa makubaliano wa ushirikiano kiuchumi na ulaya.
Miongoni mwa yaliyojiri
  • Swali kutoka kwa mbunge Juma Nkamia na swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge Freeman Mbowe kuhusu pesa zilizoahidiwa na serikali kuzipa milioni 50 kila kijiji.
  • Waziri kasema fedha hizo zipo na wanafanya utaratibu kuweza kufika na kutumiwa kulingana na makusudio.
  • Ugawaji TZS mil 50/- kila kijiji zinasubiri kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri ambalo litajadili mfumo utakaotumika.
  • Waziri Mhagama: Katika bajeti ya 2016/17, serikali imetenga kiasi cha TZS bilioni 59.5 kwa ajili ya kugawa fedha kwa kila kijiji.
  • Naibu Waziri wa Afya Kigwangala: Hakuna shehena ya madawa iliyozuiliwa ,dawa zipo na zinapatikana kwa asilimia 100% kote nchini.
Swali: Mpwapwa vijiji vingi vina tatizo la maji, serikali ina mpango gani kuchimba visima?
Jibu: Serikali imetenga bilioni 1.58 kujenga visima Mpwapwa na kukarabati miundombinu iliyopo
Swali: Serikali ina mpango gani waliosababisha watumishi hewa
Majibu(Kairuki): Serikali imechukua hatua kwa watumishi 1663 waliobainika kusababisha watumishi hewa kwa vyombo vya usalama na mamlaka zao za kinidhamu.
Nyongeza (Maida): Nawapongeza serikali wanavyojitahidi, katika uhakiki ni hasara kiasi gani serikali imepata mpaka tarehe tajwa? Serikali inaweza kuwapa adhabu ya kurudisha fedha zilizopotea?
Majibu (Kairuki): Hadi sasa watumishi hewa 19,629 wameondolewa ambao kama wangebaki wangeisababishia serikali hasara ya bilioni 19 kila mwezi. Kwa ambao mashauri yao yapo mahakamani wametakiwa kulipa faini au kurudisha fedha na watakaoshindwa kufungwa jela.
Swali la Nyongeza: Serikali inapaswa ijazie nafasi kwa watumishi wapya ikiwemo wanafunzi wanaomaliza lakini hadi leo mikopo haijatoka.
Majibu (Stella Manyanya): Kama inavyosisitizwa, pesa za mikopo Tshs bilioni 80 zimeshatolewa na kilichotuchelesha ni uhakiki, fedha inayotolewa ni kwa wale wenye uhitaji kupita wenzao. Wale wote wanaostahili kupata mikopo watapata na ndani ya wiki hii tutakuwa tumefikia mahali mazuri zaidi. Serikali inashughulikia mambo mengi katika sekta ya elimu na siyo mikopo pekee, kwa hiyo pesa nyingine zinatumika kwenye mambo mengine kama vile ujenzi wa mabweni, maabara na miundombinu mingine.
Mwenyekiti wa Bunge: Pamoja na majibu mazuri tunaomba tamko la serikali kuhusu mikopo ya wanafunzi
Swali (Waitara): Serikali ina mpango gani wa dharura wa kupunguza gharama za upimaji ardhi ili wananchi wengi
Jibu: Upimaji hufanywa na wapimaji wa serikali na binafsi waliopewa leseni. Laki tatu kwa hecta moja ya shamba au kiwanja kimoja ambapo kabla ilikuwa laki 8 kwa hekta. Vifaa vya upimaji ni gharama kubwa sana hivyo wapimaji wengi kukodi kwa gharama kubwa, kukabiliana na ongezeko, serikali kusogeza huduma kwenda kwenye kanda.
Nyongeza (Waitara): Nilimuita mpimaji chini ya ekari mbili ikawa Milioni 5, naomba maelekezo. Migogoro mingi ni kwa sababu sehemu kubwa haijapimwa, mpango wa kusogeza huduma kuna bajeti imetengwa?
Jibu (Naibu Waziri): Laki tatu kwa hekta ndio gharama sahihi baada ya bunge hili kuzipunguza, kama manispaa ina tozo tofauti inategemea halmashauri hiyo wamekubaliana nini!
Bashe: Kata za Nzega mjini zilikuwa zipelekewe umeme kwa fedha za MCC na miradi imefutwa, waziri anawaambia nini?
Jibu: Miradi yote iliyokuwa chini ya MCC itapelekwa na pesa za REA ikiwemo kata za jimbo la mheshimiwa Bashe.

WAZIRI JAFO AONYA UDANGANYIFU KWENYE MTIHANI KIDATO CHA NNE INAYOANZA LEO


wanafunzi wa kidato cha nne wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo mara baada ya kukagua maandalizi ya mtihani wa kidato cha nne unaofanyika Leo. 

Naibu waziri ofisi ya Rais Tamisemi selemani jafo akiagana na wanafunzi wa  shule ya sekondari msalato mara baada ya kuzungumza nao.

Naibu waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo, amefanya ziara kwenye shule mbalimbali mjini Dodoma kuangalia maandalizi kwa ajili ya mtihani wa kidato cha nne unaoanza Leo nchini.

Katika ziara yake kwenye Shule ya sekondari Jamhuri, Kiwanja cha ndege na Msalato, Jafo amewaonya walimu na wanafunzi hao nchini kuepukana na vitendo vya udanganyifu.

Akizungumza na walimu na wanafunzi katika shule hizo, Jafo amesema katika mtihani huo hawatarajii kuwepo na udanganyifu kwa kuwa wamejifunza kupitia mtihani wa darasa la saba ambapo kumekuwepo na tabia ya walimu kujificha chooni ili kuwasaidia wanafunzi.
Amesema shule zitakazofanya fanya hivyo zitakuwa zimepoteza thamani yake.

Ameeleza hatarajii mitihani hiyo ifanyike kinyume na kuwataka walimu wasisubutu kufanya udanganyifu wowote na kuziingiza shule zao kwenye kashfa.Jafo ame sema mara nyingi mitihani hiyo inapofanyika kumekuwa na wizi wa mitihani na kutofuatwa kwa taratibu za mitihani.

Akizungumza na wanafunzi, Jafo amewataka kujiepusha na vitendo hivyo kwa kuwa vitawafanya wafutiwe mitihani na kupoteza malengo yao kwenye maisha.

Hata hivyo amewahakikishia walimu kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kuboresha mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia na kuwataka kuwajibika ipasavyo.

JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU 200 KWA MAKOSA MBALMBALI

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro akionyesha panga ambazo wamezikamata katika operesheni  jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro akionyesha gari la Polisi likiwa linabeba mzigo wa bangi uliokatwa na Polisi katika msako ulifanyika jijini Dar es Salaam. 


Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari juu ya operesheni walizozifanya hivi karibuni  jijini Dar es Salaam. 
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro akionyesha bunduki ambayo iliangushwa na wtu wanaodhaniwa kuwa majambazi  jijini Dar es Salaam. 
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro akionyesha kwa waandishi habari begi la bangi ambalo lilikuwa likiinga Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii. 



Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu zaidi ya 200 kwa tuhuma mbalimbali likiwemo kwa watu Raia wa China kutapeliwa dola za kimarekani 800 kwa kutumia jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. 

Akizungumza na waandishi wa habari , Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro amesema kukamatwa kwa watu hao imetokana na operesheni zinazoendelea katika jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wananchi na mali zao wanaishi kwa amani. 

Amesema katika waliokamatwa ni pamoja ni panya road saba waliomvamia Nyumbani kwa Askari wa Jeshi la Wananchi , Ladislaus Kaitaba. 

Katika tukio waliweza kukamata mtandao wa panya road kwa kutumia Ramadhani Ndabi (35)ambaye alichukua simu ya askari hiyo baada ya kupiga akapatikana na kuanza kutaja wenzie wanaofanya matukio. 

Aidha amesema kuwa wizi wa magari unaendelea lakini polisi waliweza kukamata gari lilokuwa likiuzwa kwa kujifanya wateja na ilipogundulika walioiba wakatoweka. 

Kamanda Sirro amesema kuwa bangi imekuwa ikiingzwa kwa njia nyingi na sasa watu wanatumia mabegi wakiwa wasafiri kumbe wanakuwa wameweka bangi.

RAIS DKT. MAGUFULI AANDALIWA DHIFA YA KITAIFA NCHINI KENYA

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mke wa Rais wa Kenya Mama Margaret Kenyatta katika dhifa hiyo.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akizungumza katika dhifa ya Kitaifa aliyomuandalia mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Nairobi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akigonganisha glass na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo huku akiwa amewashika mikono kwa pamoja Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Naibu Rais wa Kenya William Ruto na Mke wa Rais wa Kenya Mama Margaret Kenyatta katika dhifa hiyo ya kitaifa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mabalozi mbalimbali wa Kenya waliohudhuria katika dhifa hiyo ya Kitaifa. PICHA NA IKULU

RAIS SAMIA AZINDUA TUME YA UCHUNGUZI KWA AJILI YA KUIMARISHA AMANI, HAKI NA UWAJIBIKAJI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Wajumbe wa Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Wahusi...