Monday, August 04, 2008

Hafla ya kuzaliwa rasmi Zain



Baadhi ya wasanii wa kikundi cha sanaa za maonyesho cha Umoja kutoka Afrika Kusini, wakicheza wakati wa hafla ya kubadilisha jina la kibiashara la Celtel kuwa Zain kwenye Uwanja wa Karimjee, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Sunday, August 03, 2008

Nasreem Karim Miss Vodacom


Miss Vodacom Tanzania 2008 Nasreem Karim akifurahia ushindi na mshindi wa pili Sylvia Mashuda (shoto) na wa Tatu Pendo Laizer muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa Taji hilo kwa Mwaka huu.

Hawa jamaa Wazee wa Ngwasuma wakisakata rhumba



Braza Chammeleone naye alikuwapo


Hawa hapa wakaingia Top Five

Twanga nao walikuwapo

Hebu cheki walivyopendeza




Jengo jipya ndani ya Dar


Jengo la Uhuru Heights limesanifiwa kuwa jengo refu nchini mahsusi kwa ajili ya biashara na makazi. Kivutio hicho cha jengo kimebeba nembo ya mwenge wa uhuru ambao uliwekwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro

Jengo hilo la Uhuru Heights ni mradi muhimu kwa ajili ya kuifanya mitaji ya biashara na lipo sehemu nzuri kwenye Barabara ya Bibi Titi Mohammed katikati ya jji eneo la Upanga na Oyster Bay. Jengo hili litajengwa mbele ya bahari na litaweza kutoa fursa kwa watu kutazama na kupata upepo wa bahari ya Hindi na litakuwa na vifaa vilivyotengenezwa kwa ubora unaokubaliaka duniani.

Eneo litakapojengwa ni zuri na litavutia kibiashara. Ghorofa tano ndani ya jengo zitakuwa ni kwa ajili ya ofisi zenye ukubwa tofauti. Usanifu wa jengo na umaliziaji wa hali ya juu kutawezesha na kukidhi uendeshaji wa shughuli kama vile kuunganishwa na Intaneti iliyo na kasi kubwa, maegesho na ulinzi kwa saa 2.

Jengo hili litakuwa na ghorofa 25 litakuwa ni eneo la kuvutia, likiwa na burudani na mambo mengine ya kuvutia katika maisha ya jamii. Duka la nguo za mitindo yaaina mbalimbali litakuwa kwenye mwanzo wa jengo chini na kwenye ghorofa ya kwanza na litaonyesha mitindo mbalimbali inayopongoza kwa ubora duniani. Ghorofa ya pili itakuwa na mgahawa ambao utakuwa ni wa kipekee utakaokuwa na mchanganyiko wa vyakula kutoka tamaduni mbalimbali na utahudumia wateja kutoka mataifa mbalimbali sanjari na ukumbi mkubwa wa chakula.
Ukumbi wa burudani utakuwa na eneo la michezo mbalimbali ya watoto na ukumbi wa michezo.

Kwenye maeneo ya makazi ya jengo hilo kutakuwa na bwawa la kuogelea na sehemu ya kufanyia mazoezi ya viungo (gym) kwa ajili ya wanawake na wanaume, eneo lamichezo kwa ajili ya watoto na ukumbi wa sherehe ambao unaweza kuchukua watu 100 hadi 120

Friday, August 01, 2008

Watoto wagomea nauli mpya



MAMIA ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari jijini Dar es Salaam jana waliandamana hadi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro kupinga ongezeko la nauli yao kutoka Sh50 hadi Sh100.

Wanafunzi hao walihoji sababu za serikali kuwaongezea nauli wakati imeshindwa kuwafilisi watuhumiwa wa ufisadi na kutumia fedha walizoiba kununua magari kwa ajili yao.

Katika maandamano hayo yaliyoanza majira ya saa 5:00asubuhi wanafunzi hao wakiwa na mabango walipinga kulipa nauli hiyo na kushinikiza serikali iwakubalie waendelee kulipa Sh50.

Baadhi ya mabango yalisomeka: "Wafilisiwe Chenge, Mkapa, Karamagi na Yona tuletewe mabasi ya shule, J.K utawala umekushinda, Tulipe Sh100 kwa lipi uliloboresha?".

Hatimaye Chacha Wangwe azikwa



ALIYEKUWA Mbunge wa Tarime (Chadema), Chacha Wangwe amezikwa jana kwenye makaburi ya kijijini kwao Kimakorere baada ya familia kuridhika na uchunguzi wao uliofanyika na daktari wao.

Wangwe alizikwa jana majira ya saa 12 jioni huku kukiwa na hali tata, wakati baadhi ya ndugu wakigoma na wengine kukubali.

Mazishi hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa nchini ambao pia walikuwapo katika uchunguzi uliofanyika kabla.

Akizungumza kabla ya mazishi kwa niaba ya familia muda mfupi baada ya kutoka ndani ya chumba cha uchunguzi, Prof Samwel Wangwe alisema jana kuwa uchunguzi walioutaka familia umekamilika na kwamba sasa wameridhika kuwa mbunge huyo alikufa kwa ajali na si vinginevyo. Habari ya Fredrick Katulanda.

Kapteni Mazula afariki dunia


Rubani mkuu wa atc kepteni george mazula amefariki dunia nyumbani kwake mtaa wa nyumbu, mikocheni, dar leo asubuhi baada ya kusumbuliwa na matatizo ya kupumua.

msemaji wa familia, dk. charles lugora, amesema kwamba marehemu kepteni mazula alikuwa nchini india kiasi cha wiki tatu zilizopita alikokwenda kupatiwa matibabu ya athma na ali;porejea alikuwa anaendelea vyema hadi hali ilipobadilika ghafla asubuhi ya leo ambapo alifariki dunia milango ya saa nne unusu asubuhi.

Dr. Lugora amesema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake na ratiba kamili itatolewa kesho.

marehemu mazula aliyefariki akiwa na umri wa miaka 59, ameacha mke na watoto wawili (brian na george). mtoto wake wa tatu, walter, aliuwawa huko marekani septemba 2006, ambapo yeye na mchumba wake vonetha nkya waliuwawa kikatili na watu wasiojulikana.

mola aiweke roho ya marehemu pahala pema peponi,

Msiba wa Wangwe noma

Jamaa wako na mabango wakielezea hisia zao.
Panoja na kuwapo kwa polisi lakini vijana wanaleta vurugu nyingi kiasi kwamba tumepata taarifa kuwa kuna wengine wanaletwa kw amagari nadhani sasa siasa inakolea msibani!!!!!

MTUHUMIWA WA “KUFUTA MADENI” YA MIKOPO AKIRI KOSA, AHUKUMIWA KIGOMA

KIGOMA, Septemba 4, 2026 — Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma imemhukumu Nicholaus Komba Mahitana maarufu kama Abdallah Mahimbo baad...