Benki ya Taifa ya Biashara (NBC)
imezindua rasmi Kiwango cha kwanza cha sehemu yake ya pili ya Hati
Fungani ya NBC Twiga, yenye thamani ya shilingi bilioni 27.2, ikiwa ni
hatua muhimu ya kuimarisha sekta ya biashara ndogo na za kati nchini.
Hatua
hii ya kimkakati ya benki hiyo inatajwa kuwa inalenga kuthibitisha
jitihada za benki hiyo katika kurahisisha upatikanaji wa mitaji miongoni
mwa wafanyabiashara hususani wajasiriamali ili kukuza maendeleo ya
kiuchumi nchini.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na benki hiyo mwishoni mwa wiki, hati
fungani hiyo ya miaka mitano tayari imeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la
Dar es Salaam (DSE).
“Fedha
zitakazopatikana kupitia Hati Fungani hii ya NBC Twiga zitatumika
kuwezesha mikopo rafiki kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati ambao
kimsingi tunawatambua kama uti wa mgongo wa uchumi wetu kama taifa,’’
alisisitiza Bw Theobald Sabi, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, katika taarifa
hiyo.
Bw Sabi
alisisitiza kuwa kwa kuboresha upatikanaji wa mitaji hiyo muhimu kwa
wajasiriamali, benki ya NBC inadhamiria kufungua uwezo mkubwa wa ukuaji
kwa biashara hizo, hivyo kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla
nchini.
“Malipo ya
riba kwa wawekezaji yatafanywa kila nusu mwaka wakati wote wa hati
fungani hii itakayohitimishwa mwezi Oktoba, 2029. Jambo la msingi pia ni
kufahamu kwamba mapato yatokanayo na hati fungani hii hayatozwi kodi ya
zuio (withholding tax), na hivyo kuongeza mvuto wake kwa wawekezaji wa
ndani na kimataifa,” aliongeza.
Akizungumza
kuhusu faida zinazoambatana na hati fungani hiyo, Bw Sabi alionesha
kuridhishwa na mchango wake katika kuimarisha sekta ya ujasiriamali
nchini. “Hati Fungani hii ya miaka mitano itaimarisha si tu sekta ya
ujasirimali —ambayo inawaajiri watu wengi katika nchi—bali pia itapanua
upatikanaji wa mitaji na kufungua fursa mpya za ukuaji wao,”
alisisitiza.
Maoni ya
Bw Sabi yanaakisi dhamira ya NBC ya kuendeleza maendeleo ya uchumi
endelevu kupitia ujumuishaji wa kifedha na msaada wa biashara
zinazochipukia.
Uzinduzi
wa Hati Fungani hiyo unakuja kama muitikio chanya kutoka kwa Mfuko wa
Dhamana za Sarafu za Ndani za Kiafrika (ALCB Fund) ambao ni mpango wa
Umajumui wa Afrika (Pan-Africanism) unaolenga kuwekeza katika hati
fungani za kampuni na mashirika kupitia sarafu za ndani.
Hivi
karibuni, Mfuko wa ALCB ulifanya uwekezaji mkubwa wa fedha kiasi cha sh
bilioni 27.2 (takribani Dola za kimarekani milioni 10) katika hati
fungani hiyo ya NBC Twiga, hatua iliyoonesha imani ya mfuko huo katika
kuuunga mkono mikakati ya kifedha ya NBC.
Katika
hatua inayoongeza imani na matarajio zaidi ya mpango huo, uwekezaji huo
wa Mfuko wa ALCB umewezeshwa kupitia ruzuku kutoka kwa Mfuko wa
Kubadilisha Sarafu (TCX) iliyotolewa kupitia Kituo chake cha Bei za
Uundaji wa Soko la Umoja wa Ulaya. Kituo hiki kinakusudia kuhamasisha
matumizi ya sarafu za ndani katika fedha za maendeleo, jambo ambalo ni
muhimu katika kukuza utulivu wa kiuchumi na ukuaji nchini.
“Hati
Fungani ya NBC Twiga inatarajiwa kuchochea ukuaji wa mabadiliko,
ikinufaisha wajasiriamali na uchumi kwa ujumla, na hivyo kufungua
milango kwa siku nzuri zijazo katika mzunguko wa kifedha nchini.’’
“Tunapoendelea
na mpango huu, tunabaki imara katika dhamira yetu ya kuimarisha mifumo
ya uchumi wa Tanzania, kuhakikisha kwamba wajasiriamali wanapata msaada
stahiki ili kuweza kustawi na kuchangia katika ajenda ya maendeleo ya
kitaifa,” alihitimisha.
Sunday, January 05, 2025
Benki ya NBC Yazindua Hati Fungani ya Sh Bilioni 27.2 Kuwezesha Wajasiriamali Nchini
Mkurugenzi Mtendaji Benki ya NBC - Theobald Sabi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Dkt Kikwete Akoshwa na Ushiriki wa Wadau Binafsi Kwenye Miradi ya Maendeleo, Aipongeza Benki ya NBC
Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) akikabidhi tuzo maalum kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa pil...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment