Monday, May 12, 2025

MWILI WA HAYATI CLEOPA DAVID MSUYA WAWASILI KATIKA UWAJA WA KIMATAIFA WA KILIMANJARO (KIA)










Leo, Jumatatu tarehe 12 Mei 2025, majira ya saa 2:22 asubuhi, ndege maalum iliyobeba mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais (Mstaafu),
Hayati Cleopa David Msuya, imewasili salama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Mapokezi ya mwili huo yamefanyika kwa heshima zote za kitaifa, yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, familia ya marehemu, pamoja na wananchi waliokusanyika kuonyesha upendo na heshima zao kwa kiongozi huyu mahiri na mzalendo wa dhati kwa Taifa la Tanzania.

Hayati Msuya atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika ujenzi wa Taifa, uongozi wa mfano, busara na utumishi uliotukuka kwa zaidi ya miongo minne. Uongozi wake ulitambulika kwa hekima, uvumilivu na uzalendo usiotetereka.

Ratiba kamili ya shughuli za kuaga na maziko itatolewa rasmi na Serikali kupitia vyombo vya habari na vyanzo halali vya mawasiliano.

πŸ•Š️ Tutamkumbuka daima kwa alama ya uzalendo na uadilifu aliotuachia.

Mungu ailaze roho ya Hayati Cleopa David Msuya mahali pema peponi. Amina.

No comments:

BILIONI 51 KUTUMIKA UJENZI WA BARABARA, MASOKO NA STENDI JIJINI ARUSHA

Mradi wa Uendelezaji wa Miji na Majiji Tanzania (TACTIC) unatekeleza miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 51 katika Jiji la Arusha ikiwa...