Wednesday, May 21, 2025

Kamishna wa Uhifadhi – TANAPA ateta na Mzee Peter Mavunde katika Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani

Kamishna wa Uhifadhi - TANAPA Musa Nassoro Kuji akiteta na kufurahia jambo na Mzee Peter Mavunde Meya Msta. wa jiji la Dodoma (CCM), wakati walipohudhuria kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Chinangali vilivyopo jijini Dodoma jana Mei 20, 2025.



Dodoma, Mei 20, 2025 – Kamishna wa Uhifadhi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mhe. Musa Nassoro Kuji, alionekana akiteta na kufurahia jambo na Mzee Peter Mavunde, Meya Mstaafu wa Jiji la Dodoma (CCM), wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani yaliyofanyika jana katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Maadhimisho haya muhimu yamekusudia kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa nyuki katika kuhifadhi mazingira, kuongeza uzalishaji wa kilimo kupitia uchavushaji, na kuimarisha uchumi wa wananchi kupitia ufugaji wa nyuki.

Aidha, hafla hiyo imehudhuriwa pia na Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara, Bi. Massana Mwishawa, pamoja na Makamanda wa Kanda za Kusini, Mashariki, Kaskazini na Magharibi. Vilevile, Maadhimisho hayo yamepambwa na ushiriki wa Makamishna, Maafisa Waandamizi, pamoja na askari kutoka TANAPA.

TANAPA imepewa dhamana ya kusimamia na kuendeleza maliasili zote zilizopo ndani ya Hifadhi 21 za Taifa zinazopatikana katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Taifa za kuhifadhi urithi wa asili kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Shirika linaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha maliasili za nchi yetu zinatunzwa, kuendelezwa na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kimazingira.

No comments:

SERIKALI YATOA ZAIDI YA BILIONI 5.7 KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA ELIMU MKOANI KIGOMA

KIGOMA: Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mradi wa Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP), imetoa zaidi ya Shilin...