Thursday, January 30, 2025

Rais Samia Awapongeza Washiriki wa Uokoaji Ajali ya Kuporomoka kwa Jengo Kariakoo


















Dar es Salaam, 30 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amewaandalia halfa ya chakula cha mchana washiriki wa zoezi la uokoaji wa ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika eneo la Kariakoo. Hafla hiyo imefanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kuthamini na kutambua juhudi kubwa zilizofanywa na vikosi vya uokoaji, taasisi mbalimbali, na wananchi waliojitokeza kusaidia katika operesheni hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Samia amepongeza mshikamano na uzalendo ulioonyeshwa na wadau wote waliohusika katika uokoaji, akisema kuwa kazi yao imeokoa maisha na kuleta matumaini kwa waathirika wa ajali hiyo. "Mmetimiza wajibu wenu kwa weledi, ujasiri, na moyo wa kujitolea. Taifa linawatambua na kuwathamini kwa mchango wenu mkubwa," alisema Rais Samia.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa serikali, maafisa wa vikosi vya uokoaji, madaktari, wahudumu wa afya, pamoja na wananchi waliojitolea kusaidia katika tukio hilo. Katika hotuba yake, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa kuweka mikakati thabiti ya usalama wa majengo ili kuepusha ajali za aina hiyo kutokea tena nchini.

Aidha, hafla hiyo imepambwa na matukio mbalimbali, ikiwemo utoaji wa vyeti vya kutambua mchango wa washiriki wa uokoaji, hotuba za viongozi, na maonyesho mafupi ya picha zinazoonyesha juhudi za uokoaji.

Rais Samia amehitimisha hafla hiyo kwa kuwahakikishia waathirika wa ajali hiyo kuwa serikali itaendelea kutoa msaada wa karibu na kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa ili kuepusha majanga kama haya siku zijazo.

 

No comments:

Prof. Mfaransa Aja na Kitabu: Aiambia Dunia Kutalii Tanzania ni Tiba

Na Mwandishi Wetu Paris, Ufaransa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, akiwa nchini Ufaransa jana Julai 8, 2025 amek...